Anayepiga Vita Manhaj Ya Salaf Ni Lazima Apigwe Vita

Wabaya zaidi ambao tunakabiliana nao katika wakati huu ni waharibifu wanoajinasibisha na Salafiyyah na hawataki wazungumziwe watu. Yule anayekosea katika kosa limoja tu anasihiwe binafsi. Lakini tatizo liko kwa yule anayesema kuwa ni Salafiy na anapiga vita kanuni za mfumo wa Salaf. Hawataki uzungumze. Wanaeneza utata. Moja wapo ni kwamba huyu ni ndugu yetu. Ya pili ni kwamba mtu huyu aliwahi kuwa Salafiyyah mzuri. Ya tatu ni kwamba hili linawafarikanisha Salafiyyuun. Utata kama huu unaenezwa hivi sasa. Ni batili na ni wenye kurudishwa. Ni kweli mtu huyu ni ndugu yako na ni ndugu yangu. Ikiwa ameteleza katika kosa limoja anasihiwe na kusonga mbele. Ama ikiwa analingania katika kuvunja na kubomoa mfumo na kanuni za Salaf kwa kiasi cha kwamba anachukua vita vya Ahl-ul-Bid´ah wa asli dhidi ya Salafiyyuun, ni wajibu kusitishwa na kubainisha hali yake kwa watu ili wasidanganyike naye. Salaf-us-Swaalih wetu wamesema kuwa Sunniy anayekaa na Ahl-ul-Bid´ah ni mbaya zaidi kuliko Ahl-ul-Bid´ah. Wamesema namna hiyo juu ya yule anayekaa nao tu. Mtu asemeje kwa yule anayedai kuwa ni Sunniy na ni Salafiy na anawatetea Ahl-ul-Ahwaa´ au anatunga kanuni ili kuwatetea? Ninaapa kwa Allaah kuwa huyu ni katika wao. Haijalishi yule atayechukulia kwa ubaya. Hatutaki kwa yeyote malipo wala shukurani. Hatutaki kitu chochote cha kidunia. Hatutaki cheo chochote. Hatutaki nafasi yoyote. Hata hivyo kuhusu nasaha ni wajibu. Mzungumzaji: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy Chanzo: http://www.subulsalam.com/play.php?catsmktba=27985 Toleo la: 18-07-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Wabaya zaidi ambao tunakabiliana nao katika wakati huu ni waharibifu wanoajinasibisha na Salafiyyah na hawataki wazungumziwe watu. Yule anayekosea katika kosa limoja tu anasihiwe binafsi. Lakini tatizo liko kwa yule anayesema kuwa ni Salafiy na anapiga vita kanuni za mfumo wa Salaf. Hawataki uzungumze. Wanaeneza utata. Moja wapo ni kwamba huyu ni ndugu yetu. Ya pili ni kwamba mtu huyu aliwahi kuwa Salafiyyah mzuri. Ya tatu ni kwamba hili linawafarikanisha Salafiyyuun. Utata kama huu unaenezwa hivi sasa. Ni batili na ni wenye kurudishwa.

Ni kweli mtu huyu ni ndugu yako na ni ndugu yangu. Ikiwa ameteleza katika kosa limoja anasihiwe na kusonga mbele. Ama ikiwa analingania katika kuvunja na kubomoa mfumo na kanuni za Salaf kwa kiasi cha kwamba anachukua vita vya Ahl-ul-Bid´ah wa asli dhidi ya Salafiyyuun, ni wajibu kusitishwa na kubainisha hali yake kwa watu ili wasidanganyike naye. Salaf-us-Swaalih wetu wamesema kuwa Sunniy anayekaa na Ahl-ul-Bid´ah ni mbaya zaidi kuliko Ahl-ul-Bid´ah. Wamesema namna hiyo juu ya yule anayekaa nao tu. Mtu asemeje kwa yule anayedai kuwa ni Sunniy na ni Salafiy na anawatetea Ahl-ul-Ahwaa´ au anatunga kanuni ili kuwatetea? Ninaapa kwa Allaah kuwa huyu ni katika wao. Haijalishi yule atayechukulia kwa ubaya. Hatutaki kwa yeyote malipo wala shukurani. Hatutaki kitu chochote cha kidunia. Hatutaki cheo chochote. Hatutaki nafasi yoyote. Hata hivyo kuhusu nasaha ni wajibu.

Mzungumzaji: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
Chanzo: http://www.subulsalam.com/play.php?catsmktba=27985
Toleo la: 18-07-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 18th, July 2014