Anayefanya Shirki Kwa Dhahiri Na Kwa Ndani Anaamini Kinyume

Allaah (Ta´ala) Anasema: مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ “Atakayemkufuru Allaah baada ya iymaan yake (atapata adhabu) isipokuwa yule aliyekirihishwa (kukanusha Dini ya Kiislamu) na huku moyo wake umetua juu ya iymaan (kwamba yeye ni Muumin; huyu hana makosa akitamka matamshi yenye kufuru). Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao (juu yao ni) ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kubwa. Hivyo kwa sababu wao wamefadhilisha maisha ya dunia kuliko ya Aakhirah; na kwamba Allaah Haongoi watu makafiri.” (16:106-107) Huyu ambaye anawatii makafiri kwa kuwachinjia masanamu yao na kushirikiana nao katika ´Ibaadah zao kwa kutaka mali na anasema ”Mimi naamini ya kwamba yale waliyomo ni batili, lakini nashirikiana nao kwa ajili ya kutaka mali, huyu anaingia katika kauli yake: ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ “Hivyo kwa sababu wao wamefadhilisha maisha ya dunia kuliko ya Aakhirah; na kwamba Allaah Haongoi watu makafiri.” (16:107) أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۖوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ Hao ni wale ambao Allaah Amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na masikio yao, na macho yao. Na hao ndio walioghafilika.” (16:107-108) Huyu hayakubaliwi maneno yake katika maudhui hii. Huu ni upotevu. Haitoshi kwake kusema mimi naamini kinyume, kwa kuwa mwenye kuhidhirisha ukafiri kwa kutamka maneno ya kikafiri au kwa kufanya kitendo cha kikafiri kwa khiyari yake mwenyewe na huku akijua kuwa ni ukafiri, pasina kutenzwa nguvu, basi ukafiri unamgusa. Kwa kuwa hana udhuru.

Allaah (Ta´ala) Anasema:

مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ
“Atakayemkufuru Allaah baada ya iymaan yake (atapata adhabu) isipokuwa yule aliyekirihishwa (kukanusha Dini ya Kiislamu) na huku moyo wake umetua juu ya iymaan (kwamba yeye ni Muumin; huyu hana makosa akitamka matamshi yenye kufuru). Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao (juu yao ni) ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kubwa. Hivyo kwa sababu wao wamefadhilisha maisha ya dunia kuliko ya Aakhirah; na kwamba Allaah Haongoi watu makafiri.” (16:106-107)

Huyu ambaye anawatii makafiri kwa kuwachinjia masanamu yao na kushirikiana nao katika ´Ibaadah zao kwa kutaka mali na anasema ”Mimi naamini ya kwamba yale waliyomo ni batili, lakini nashirikiana nao kwa ajili ya kutaka mali, huyu anaingia katika kauli yake:

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ
“Hivyo kwa sababu wao wamefadhilisha maisha ya dunia kuliko ya Aakhirah; na kwamba Allaah Haongoi watu makafiri.” (16:107)

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۖوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ
Hao ni wale ambao Allaah Amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na masikio yao, na macho yao. Na hao ndio walioghafilika.” (16:107-108)

Huyu hayakubaliwi maneno yake katika maudhui hii. Huu ni upotevu. Haitoshi kwake kusema mimi naamini kinyume, kwa kuwa mwenye kuhidhirisha ukafiri kwa kutamka maneno ya kikafiri au kwa kufanya kitendo cha kikafiri kwa khiyari yake mwenyewe na huku akijua kuwa ni ukafiri, pasina kutenzwa nguvu, basi ukafiri unamgusa. Kwa kuwa hana udhuru.