Anaposimama Mwanamke Wakati Anapokuwa Imamu

Mwanamke akiongoza wanawake wengine katika Swalah, Sunnah ni yeye kusimama katikati ya safu. Imepokelewa kutoka kwa ´Aaishah na Ummu Salamah. Ikiwa anaswali na mwanamke mwingine, atasimama upande wa kulia mwa huyo Imamu mwanamke. Ikiwa badala yake atasimama nyuma yake, kitendo hichi kinajuzu. Hakika mwanamke anaweza kusimama peke yake wakati anaposwali, jambo ambalo linatolewa dalili na Hadiyth ya Anas.[1] ------------------- (1) Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema: "Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama kwa ajili ya Swalah. Mimi na mtoto yatima mmoja tukasimama nyuma yake na nyuma yetu akasimama mwanamke. Kisha akaswali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Rakaa mbili pamoja na sisi." (al-Bukhaariy na Muslim)

Mwanamke akiongoza wanawake wengine katika Swalah, Sunnah ni yeye kusimama katikati ya safu. Imepokelewa kutoka kwa ´Aaishah na Ummu Salamah.

Ikiwa anaswali na mwanamke mwingine, atasimama upande wa kulia mwa huyo Imamu mwanamke. Ikiwa badala yake atasimama nyuma yake, kitendo hichi kinajuzu. Hakika mwanamke anaweza kusimama peke yake wakati anaposwali, jambo ambalo linatolewa dalili na Hadiyth ya Anas.[1]

——————-
(1) Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama kwa ajili ya Swalah. Mimi na mtoto yatima mmoja tukasimama nyuma yake na nyuma yetu akasimama mwanamke. Kisha akaswali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Rakaa mbili pamoja na sisi.” (al-Bukhaariy na Muslim)


  • Author: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (d. 620). al-Kaafiy (1/192)
  • Kitengo: Uncategorized , ´Ibaadah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 3rd, January 2014