´Allaamah Zayd al-Madkhaliy Kuhusu Uombezi

Shafaa´ah, uombezi umegawanyika sehemu mbili: 1- Uombezi wenye kuthibitishwa (kukubaliwa). 2- Uombezi wenye kukataliwa. Uombezi wenye kuthibitishwa ni ule ambao umethibitishwa na Qur-aan kwa kuwa umeeneza masharti ya maombezi: 1- Idhini ya Allaah kwa muombeaji aombee. 2- Kumridhia Kwake muombewaji. Haitokuwa isipokuwa kwa watu wa Tawhiyd na watu wa imani. Kuwa kuwa kuna uombezi mbali mbali na sio uombezi mmoja tu. Kuna uombezi ambao wanapinga Ahl-ul-Bid´ah wad-Dhwalaal, kama Mu´tazilah na wengineo juu ya Waislamu waliotenda madhambi makubwa. Umethibiti kwa Qur-aan na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Uombezi wangu umefanywa kwa walio na madhambi makubwa katika Ummah wangu.” Ama uombezi wenye kukataliwa ni ule ambao wanaamini makafiri juu ya wale wanaowaabudu sawa waliohai au waliokufa. Siku ya Qiyaamah hawatowanufaisha kwa kitu, bali watajiweka nao mbali. Allaah Atawaingiza Motoni sawa aliekuwa akiabudu na aliekuwa akiabudiwa. Isipokuwa tu wale walioabudiwa pasina kuridhia, kama Mitume, Manabii, watu wema, watu hawa wako mbali na kuwa pamoja na wale wenye kuwaabudu. Lakini mawe, miti na kila mwenye kuabudiwa naye akawa radhi juu ya hilo, mwenye kuwaita watu wamuabudu pamoja na wenye kuwaabudu, wote hawa watakuwa Motoni. Mwandishi: Imaam Abu Ja´far al-Warraaq at-Twahaawiy al-Muswriy Chanzo: Sharh ´Aqiydat-it-Twahaawiyyah Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=960&size=2h&ext=.rm

Shafaa´ah, uombezi umegawanyika sehemu mbili:

1- Uombezi wenye kuthibitishwa (kukubaliwa).
2- Uombezi wenye kukataliwa.

Uombezi wenye kuthibitishwa ni ule ambao umethibitishwa na Qur-aan kwa kuwa umeeneza masharti ya maombezi:

1- Idhini ya Allaah kwa muombeaji aombee.
2- Kumridhia Kwake muombewaji.

Haitokuwa isipokuwa kwa watu wa Tawhiyd na watu wa imani. Kuwa kuwa kuna uombezi mbali mbali na sio uombezi mmoja tu. Kuna uombezi ambao wanapinga Ahl-ul-Bid´ah wad-Dhwalaal, kama Mu´tazilah na wengineo juu ya Waislamu waliotenda madhambi makubwa. Umethibiti kwa Qur-aan na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uombezi wangu umefanywa kwa walio na madhambi makubwa katika Ummah wangu.”

Ama uombezi wenye kukataliwa ni ule ambao wanaamini makafiri juu ya wale wanaowaabudu sawa waliohai au waliokufa. Siku ya Qiyaamah hawatowanufaisha kwa kitu, bali watajiweka nao mbali. Allaah Atawaingiza Motoni sawa aliekuwa akiabudu na aliekuwa akiabudiwa. Isipokuwa tu wale walioabudiwa pasina kuridhia, kama Mitume, Manabii, watu wema, watu hawa wako mbali na kuwa pamoja na wale wenye kuwaabudu. Lakini mawe, miti na kila mwenye kuabudiwa naye akawa radhi juu ya hilo, mwenye kuwaita watu wamuabudu pamoja na wenye kuwaabudu, wote hawa watakuwa Motoni.

Mwandishi: Imaam Abu Ja´far al-Warraaq at-Twahaawiy al-Muswriy
Chanzo: Sharh ´Aqiydat-it-Twahaawiyyah
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=960&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 4th, April 2014