´Allaamah Zayd al-Madkhaliy Kuhusu Kuhukumu Kinyume Na Shari´ah

Hukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah hili linahitajia ufafanuzi. Wanachuoni wamesema kuwa mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah akionelea kuwa ni bora [kuliko Shari´ah], basi amekufuru kufuru inayomtoa katika Uislamu. Kwa kuwa amefadhilisha hukumu isiyokuwa ya Allaah juu ya hukumu ya Allaah. Mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah akiamini kuwa kufanya hivyo kunajuzu, amekufuru kufuru inayomtoa katika Uislamu. Mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah akidai kwamba kuhukumu kwa Aliyoteremsha Allaah na kwa yale ambayo hakuteremsha Allaah ni sawa yote yako katika manzilah moja, amekufuru kufuru inayomtoa katika Uislamu. Mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah na yeye anaamini kwamba kuhukumu kwa hukumu ya Allaah ndio wajibu na iliyo faradhi na kwamba mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah ameasi, huyu ni mtenda dhambi kubwa au ni kufuru ya ´amali (kufuru ndogo) isiyomtoa katika Uislamu. Hii ndio tofauti kati ya kubadili na kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah. Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy Chanzo: Usuul-us-Sunnah Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=1004&size=2h&ext=.rm

Hukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah hili linahitajia ufafanuzi. Wanachuoni wamesema kuwa mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah akionelea kuwa ni bora [kuliko Shari´ah], basi amekufuru kufuru inayomtoa katika Uislamu. Kwa kuwa amefadhilisha hukumu isiyokuwa ya Allaah juu ya hukumu ya Allaah.

Mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah akiamini kuwa kufanya hivyo kunajuzu, amekufuru kufuru inayomtoa katika Uislamu.

Mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah akidai kwamba kuhukumu kwa Aliyoteremsha Allaah na kwa yale ambayo hakuteremsha Allaah ni sawa yote yako katika manzilah moja, amekufuru kufuru inayomtoa katika Uislamu.

Mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah na yeye anaamini kwamba kuhukumu kwa hukumu ya Allaah ndio wajibu na iliyo faradhi na kwamba mwenye kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah ameasi, huyu ni mtenda dhambi kubwa au ni kufuru ya ´amali (kufuru ndogo) isiyomtoa katika Uislamu. Hii ndio tofauti kati ya kubadili na kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah.

Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy
Chanzo: Usuul-us-Sunnah
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=1004&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Kukufurisha na Kuhukumu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 24th, March 2014