´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy Kuhusu al-Halabiy Na Abul-Hasan Na Kanuni Zao

Hili linatia nguvu yale yaliyoandika Abul-Hasan Uingereza ili kuwaambatanisha vijana Salafiyyuun na ´Aliy Hasan na Saliym (al-Hilaaliy). Kadhalika linatilia nguvu ´Aliy Hasan al-Halabiy [sauti haisikiki] na kuwalazimisha na kuwaambia warejee kwao na wasirejee kwa wanachuoni wa Saudi Arabia.[1] Ni wajinga na hawakuichukua elimu kutoka kwa wanachuoni. Bali wamechukua elimu kutoka barabarani na kwenye magazeti. Hawakusoma kwenye vyuo vikuu na wala hawana vyeti. Nyoyo zao zimejaa chuki dhidi ya Manhaj ya Salaf na Salafiyyuun. Abul-Hasan amesoma wapi? ´Aliy Hasan amesoma wapi? Abu Ishaaq amesoma wapi? al-Albaaniy [sauti haisikiki]. Miongoni mwa wanafunzi wake wakubwa na mbora katika uhai wa Shaykh ni Muhammad Naswiyb ar-Rifaa´iy, ambaye Shaykh (al-Albaaniy) alimsusa kwa ajili ya suala limoja na akashauri watu wamsuse. Hii ilikuwa inahusiana na suala limoja tu hakumvumilia hata kwa muda mfupi. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba alimsusa kwa ajili ya suala limoja tu na akaamrisha kumsusa mpaka alipokufa. Kadhalika wakati alipovutana na baadhi ya Salafiyyuun, alikuwa karibu na kuwazingatia kuwa sio katika Salafiyyah na kusema Salafiy hamshambulii Salafiy mwingine ilihali mtu huyu amenishambulia. Ibn Baaz amewafanyia Tabdiy´ watu ambao wamefanya jambo dogo sana ukilinganisha na waliotumbukia ndani yake watu hawa. Alikuwa akionelea mtu mwenye kuwasifu watu wa Bid´ah basi huyo ni katika wao na ni katika walinganizi wao. Msimamo kama huu ametanguliwa kabla yake na maimamu. Mtu alikuwa akimsifia mmoja katika watu wa Bid´ah, basi anazingatiwa kuwa ni katika wao na ni mlinganizi wao. Ametanguliwa katika hilo na Ibn Taymiyyah, Ibn Khathiyr na wengineo. Ibn Baaz aliulizwa kuhusu mtu ambaye anawawaetetea watu wa Bid´ah. Akasema yeye ni katika wao bila ya sahaka yoyote kwa kuwa anaita katika madhehebu yao.[2] Allaah Amrahamu. ´Adnaan ´Ar´uur anasema kuwa Salafiyyah ni jambo la sawia na makundi yote haya ambayo yanataka [sauti haisikiki] na kuifikia ni katika Salafiyyah. Sisemi kuwa wao wako pamoja nyinyi, bali nasema kuwa ni katika wao. Abul-Hasan na yeye anakuja na kanuni zake “Mfumo mpana na wasaa” na ´Aliy Hasan anamsapoti kwa hilo. Kanuni nyingine “Hata ukiniletea mamia ya dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah na maneno ya Salaf, bado hainilazimu kitu”. Kanuni hizi ni chafu sana kabisa. Miongoni mwazo ni “Mfumo mpana na wasaa” ili watu wa Bid´ah wapate kuwa humo, “Haki hainilazimu kitu”, “Tunasahihisha na hatuwajeruhi watu”, “Ukihukumu wengine na wewe utahukumiwa” na nyinginezo.[3] Kuna mmoja wao anasema “Inatakiwa kuyaangalia upya mambo fulani” na ni kweli wameyaangalia upya na kuasisi kanuni na hawakutosheka na hayo tu. Katika kikao kimoja Makkah, kuna mmoja wao alisema – na alikuwa ni katika wanafunzi wangu – kwamba inatakiwa kuangalia upya misingi ya Salafiyyah. Akafanya hivo na hatimae akafikia makumi ya kanuni ambazo zote zilikuwa zinaharibu Manhaj ya Salaf. Alikuwa ni mtu wa Algeria. ---------------- (1) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/al-halabiy-juu-ya-wanachuoni-wa-saudi-arabia (2) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/mwenye-kuwasifia-au-kuwatetea-watu-wa-bid%C2%B4ah-ni-katika-wao (3) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/%C2%B4allaamah-al-fawzaan-kuhusu-kuwajeruhi-ahl-ul-bid%C2%B4ah-na-kanuni-za-%C2%B4adnaan-%C2%B4ar%C2%B4uur

Hili linatia nguvu yale yaliyoandika Abul-Hasan Uingereza ili kuwaambatanisha vijana Salafiyyuun na ´Aliy Hasan na Saliym (al-Hilaaliy). Kadhalika linatilia nguvu ´Aliy Hasan al-Halabiy [sauti haisikiki] na kuwalazimisha na kuwaambia warejee kwao na wasirejee kwa wanachuoni wa Saudi Arabia.[1]

Ni wajinga na hawakuichukua elimu kutoka kwa wanachuoni. Bali wamechukua elimu kutoka barabarani na kwenye magazeti. Hawakusoma kwenye vyuo vikuu na wala hawana vyeti. Nyoyo zao zimejaa chuki dhidi ya Manhaj ya Salaf na Salafiyyuun. Abul-Hasan amesoma wapi? ´Aliy Hasan amesoma wapi? Abu Ishaaq amesoma wapi?

al-Albaaniy [sauti haisikiki]. Miongoni mwa wanafunzi wake wakubwa na mbora katika uhai wa Shaykh ni Muhammad Naswiyb ar-Rifaa´iy, ambaye Shaykh (al-Albaaniy) alimsusa kwa ajili ya suala limoja na akashauri watu wamsuse. Hii ilikuwa inahusiana na suala limoja tu hakumvumilia hata kwa muda mfupi. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba alimsusa kwa ajili ya suala limoja tu na akaamrisha kumsusa mpaka alipokufa. Kadhalika wakati alipovutana na baadhi ya Salafiyyuun, alikuwa karibu na kuwazingatia kuwa sio katika Salafiyyah na kusema Salafiy hamshambulii Salafiy mwingine ilihali mtu huyu amenishambulia.

Ibn Baaz amewafanyia Tabdiy´ watu ambao wamefanya jambo dogo sana ukilinganisha na waliotumbukia ndani yake watu hawa. Alikuwa akionelea mtu mwenye kuwasifu watu wa Bid´ah basi huyo ni katika wao na ni katika walinganizi wao. Msimamo kama huu ametanguliwa kabla yake na maimamu. Mtu alikuwa akimsifia mmoja katika watu wa Bid´ah, basi anazingatiwa kuwa ni katika wao na ni mlinganizi wao. Ametanguliwa katika hilo na Ibn Taymiyyah, Ibn Khathiyr na wengineo.

Ibn Baaz aliulizwa kuhusu mtu ambaye anawawaetetea watu wa Bid´ah. Akasema yeye ni katika wao bila ya sahaka yoyote kwa kuwa anaita katika madhehebu yao.[2] Allaah Amrahamu.

´Adnaan ´Ar´uur anasema kuwa Salafiyyah ni jambo la sawia na makundi yote haya ambayo yanataka [sauti haisikiki] na kuifikia ni katika Salafiyyah. Sisemi kuwa wao wako pamoja nyinyi, bali nasema kuwa ni katika wao.

Abul-Hasan na yeye anakuja na kanuni zake “Mfumo mpana na wasaa” na ´Aliy Hasan anamsapoti kwa hilo. Kanuni nyingine “Hata ukiniletea mamia ya dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah na maneno ya Salaf, bado hainilazimu kitu”. Kanuni hizi ni chafu sana kabisa. Miongoni mwazo ni “Mfumo mpana na wasaa” ili watu wa Bid´ah wapate kuwa humo, “Haki hainilazimu kitu”, “Tunasahihisha na hatuwajeruhi watu”, “Ukihukumu wengine na wewe utahukumiwa” na nyinginezo.[3] Kuna mmoja wao anasema “Inatakiwa kuyaangalia upya mambo fulani” na ni kweli wameyaangalia upya na kuasisi kanuni na hawakutosheka na hayo tu. Katika kikao kimoja Makkah, kuna mmoja wao alisema – na alikuwa ni katika wanafunzi wangu – kwamba inatakiwa kuangalia upya misingi ya Salafiyyah. Akafanya hivo na hatimae akafikia makumi ya kanuni ambazo zote zilikuwa zinaharibu Manhaj ya Salaf. Alikuwa ni mtu wa Algeria.

—————-
(1) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/al-halabiy-juu-ya-wanachuoni-wa-saudi-arabia
(2) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/mwenye-kuwasifia-au-kuwatetea-watu-wa-bid%C2%B4ah-ni-katika-wao
(3) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/%C2%B4allaamah-al-fawzaan-kuhusu-kuwajeruhi-ahl-ul-bid%C2%B4ah-na-kanuni-za-%C2%B4adnaan-%C2%B4ar%C2%B4uur