´Allaamah al-Waadi´iy Kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun, al-Qaradhaawiy, az-Zindaaniy, as-Saawiy Na Tamasha

Ninamjua mtu kutoka wakati wa al-Madiynah. Kama alisikia kunaongelewa kuhusu kitabu ar-Riyaadh au Hijaaz akaenda kukinunua. Kisha akaanza kufanya kazi kama mwalimu kwenye chuo kikuu Iymaan [San´aa´; Yemen]. Chuo kikuu hichi ni kama vyuo vikuu vingine vyote vinavyoongozwa na al-Ikhwaan al-Muslimuun. Je, wanaweza kuleta mwanafunzi mmoja aliyekhitimu ambaye amekuwa ni marejeleo? Hawawezi hilo. Hata mtu mmoja. Kila mwaka wanapokea mamilioni kama alama pekee ya taasisi hizi. Niliwauliza kuhusu tamasha (tamthili/filamu). Pamoja na hivyo wanasema ya kwamba wako katika Ahl-us-Sunnah. Nyinyi sio Ahl-us-Sunnah. Msiwadanganye watu. Wanachuoni wanasema kuwa tamasha ni haramu. Je, mmekwishaacha tamasha ambayo uharamu wake wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wamekubaliana juu yake? al-Qaradhwaawiy - Allaah Amkate ulimi wake - anashaji´isha wanawake katika tamasha.[1] Alipoambiwa ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy ya kwamba al-Qaradhwaawiy anasema: "Hatupigani vita na mayahudi kwa sababu ya ´Aqiydah. Tunapigana nao vita kwa sababu ya ardhi[2] [Palestina] akasema: "Nijuacho tu ni kwamba ni Mujaahid." Mujaahid? Ndio, anapigana vita (Jihaad) dhidi ya Ahl-us-Sunnah na kukimbiza watu na Sunnah na Ahl-us-Sunnah. Analingania katika upotevu. Tunaweza kusema pia kuwa ni Imaam, kiongozi. Lakini ni kiongozi mpotevu: وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ "Na Tukawafanya viongozi wanaoita (watu) motoni; na Siku ya Qiyaamah hawatonusuriwa." (28:41) Hali kadhalika Swalaah as-Saawiy mrithi wa Sa´iyd Hawaa. Kwa masikitiko makubwa Swalaah as-Saawiy! Ninakujua tokea Misri ukiwa mtu mnyenyekevu unayeshikamana na Sunnah. Hata hivyo, umepewa mtihani kwa pesa za Saudi Arabia ukawa mmoja katika walinganiaji wa al-Ikhwaan al-Muslimuun. -------------------- (1) al-Qaradhwaawiy kasema: "Kuna dharurah kwa mwanamke kushiriki katika tamasha". Gazeti la Kuwaiti al-Mujtamaa (2) Gazeti ar-Raayah (4696). Tarehe: 1415/Sha´abaan/24 Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy Chanzo: al-Burkaan, uk. 17-18 Toleo la: 22-05-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Ninamjua mtu kutoka wakati wa al-Madiynah. Kama alisikia kunaongelewa kuhusu kitabu ar-Riyaadh au Hijaaz akaenda kukinunua. Kisha akaanza kufanya kazi kama mwalimu kwenye chuo kikuu Iymaan [San´aa´; Yemen].

Chuo kikuu hichi ni kama vyuo vikuu vingine vyote vinavyoongozwa na al-Ikhwaan al-Muslimuun. Je, wanaweza kuleta mwanafunzi mmoja aliyekhitimu ambaye amekuwa ni marejeleo? Hawawezi hilo. Hata mtu mmoja. Kila mwaka wanapokea mamilioni kama alama pekee ya taasisi hizi. Niliwauliza kuhusu tamasha (tamthili/filamu). Pamoja na hivyo wanasema ya kwamba wako katika Ahl-us-Sunnah. Nyinyi sio Ahl-us-Sunnah. Msiwadanganye watu. Wanachuoni wanasema kuwa tamasha ni haramu. Je, mmekwishaacha tamasha ambayo uharamu wake wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wamekubaliana juu yake?

al-Qaradhwaawiy – Allaah Amkate ulimi wake – anashaji´isha wanawake katika tamasha.[1] Alipoambiwa ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy ya kwamba al-Qaradhwaawiy anasema: “Hatupigani vita na mayahudi kwa sababu ya ´Aqiydah. Tunapigana nao vita kwa sababu ya ardhi[2] [Palestina] akasema:

“Nijuacho tu ni kwamba ni Mujaahid.”

Mujaahid? Ndio, anapigana vita (Jihaad) dhidi ya Ahl-us-Sunnah na kukimbiza watu na Sunnah na Ahl-us-Sunnah. Analingania katika upotevu. Tunaweza kusema pia kuwa ni Imaam, kiongozi. Lakini ni kiongozi mpotevu:

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ
“Na Tukawafanya viongozi wanaoita (watu) motoni; na Siku ya Qiyaamah hawatonusuriwa.” (28:41)

Hali kadhalika Swalaah as-Saawiy mrithi wa Sa´iyd Hawaa. Kwa masikitiko makubwa Swalaah as-Saawiy! Ninakujua tokea Misri ukiwa mtu mnyenyekevu unayeshikamana na Sunnah. Hata hivyo, umepewa mtihani kwa pesa za Saudi Arabia ukawa mmoja katika walinganiaji wa al-Ikhwaan al-Muslimuun.

——————–
(1) al-Qaradhwaawiy kasema:
“Kuna dharurah kwa mwanamke kushiriki katika tamasha”. Gazeti la Kuwaiti al-Mujtamaa
(2) Gazeti ar-Raayah (4696). Tarehe: 1415/Sha´abaan/24

Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Chanzo: al-Burkaan, uk. 17-18
Toleo la: 22-05-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Qaradhwaawiy, Yuusuf
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 12th, January 2014