´Allaamah al-Luhaydaan Kuhusu Yuusuf Qaradhwaawiy Na al-Ikhwaan al-Muslimuun

Nimesikia maneno ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Barraak akimkosoa Yuusuf Qaradhwaawiy, ukweli ni kwamba alifanya kosa kubwa. Anakuja kujiingiza na kumuandikia Mfalme - Allaah Amuongoze. Alimuandikia na kumshukuru kwa hili na lile na kumuomba hili na lile. Kwa nini hajafikiria kukaa kwenye Msikiti wa Husayn na kuwakataza watu kufanya Shirki kubwa? Kwa kuwa huwezi kukuta al-Ikhwaan al-Muslimuun wakikataza Shirki kubwa. Isipokuwa tu wanakimbizana hukumu ya siasa iwe ya Kiislamu. Lakini huyu mtu kamuandikia Mfalme na kumuomba wanawake nao waweze kutembeza gari. Allaah Amlipe Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Barraak kwa aliyoyaandika na tunamuomba Allaah Amuongoze Yuusuf Qaradhwaawiy. Yuusuf Qaradhwaawiy alikuwa akienda Iran na nchi zingine akitaka kuwafanya Waislamu wawe kitu kimoja. Vipi atawafanya Waislamu wawe na Umoja kwenye njia moja wakati kuna wanaomtegemea Husayn, wakimuabudu na kumuomba msaada na wakiona kuwa kwenda kwenye kaburi lake ni bora zaidi kuliko hata kwenda Makkah? Muulizaji: Kuhusiana na Shaykh Yuusuf Qaradhwaawiy uhusiano wake na vyombo vya khabari na maandamano, baadhi ya watu wanauliza vipi mwanachuoni anaweza kumshambulia mwanachuoni mwingine mbele ya watu hadharani, Kwa nini asinasihiwi kwa siri au akaandikiwa kwa siri? Unasemaje kuhusu hawa watu? ´Allaamah al-Luhaydaan: Wakati niliongelea kuhusu maandamano kwenye [al-Masjid] al-Haraam na nikasema kuwa kufanya Khuruuj kwa Kiongozi kwa kufanya maandamano ni [kueneza] ufisadi katika ardhi. Na maandamano ya kwanza katika Uislamu ndio ilikuwa sababu ya ´Uthmaan bin Affaan (Radhiya Allaahu ´anhyu) kuuawa. Alisema (Qaradhwaawiy) kuwa al-Luhaydaan kakosea katika hili na kwamba ni lazima kufanywe maandamano ili kusimamisha dhuluma. Lakini kwa yule atayefahamu Manhaj ya al-Ikhwaan al-Muslimuun na akasoma vipi mtu atashikamana na al-Ikhwaan al-Muslimuun inapohusiana na haki na utiifu, mtu ataona kuwa hawako juu ya ´Aqiydah sahihi nzuri.

Nimesikia maneno ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Barraak akimkosoa Yuusuf Qaradhwaawiy, ukweli ni kwamba alifanya kosa kubwa. Anakuja kujiingiza na kumuandikia Mfalme – Allaah Amuongoze. Alimuandikia na kumshukuru kwa hili na lile na kumuomba hili na lile. Kwa nini hajafikiria kukaa kwenye Msikiti wa Husayn na kuwakataza watu kufanya Shirki kubwa? Kwa kuwa huwezi kukuta al-Ikhwaan al-Muslimuun wakikataza Shirki kubwa. Isipokuwa tu wanakimbizana hukumu ya siasa iwe ya Kiislamu. Lakini huyu mtu kamuandikia Mfalme na kumuomba wanawake nao waweze kutembeza gari. Allaah Amlipe Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Barraak kwa aliyoyaandika na tunamuomba Allaah Amuongoze Yuusuf Qaradhwaawiy.

Yuusuf Qaradhwaawiy alikuwa akienda Iran na nchi zingine akitaka kuwafanya Waislamu wawe kitu kimoja. Vipi atawafanya Waislamu wawe na Umoja kwenye njia moja wakati kuna wanaomtegemea Husayn, wakimuabudu na kumuomba msaada na wakiona kuwa kwenda kwenye kaburi lake ni bora zaidi kuliko hata kwenda Makkah?

Muulizaji:
Kuhusiana na Shaykh Yuusuf Qaradhwaawiy uhusiano wake na vyombo vya khabari na maandamano, baadhi ya watu wanauliza vipi mwanachuoni anaweza kumshambulia mwanachuoni mwingine mbele ya watu hadharani, Kwa nini asinasihiwi kwa siri au akaandikiwa kwa siri? Unasemaje kuhusu hawa watu?

´Allaamah al-Luhaydaan:
Wakati niliongelea kuhusu maandamano kwenye [al-Masjid] al-Haraam na nikasema kuwa kufanya Khuruuj kwa Kiongozi kwa kufanya maandamano ni [kueneza] ufisadi katika ardhi. Na maandamano ya kwanza katika Uislamu ndio ilikuwa sababu ya ´Uthmaan bin Affaan (Radhiya Allaahu ´anhyu) kuuawa. Alisema (Qaradhwaawiy) kuwa al-Luhaydaan kakosea katika hili na kwamba ni lazima kufanywe maandamano ili kusimamisha dhuluma. Lakini kwa yule atayefahamu Manhaj ya al-Ikhwaan al-Muslimuun na akasoma vipi mtu atashikamana na al-Ikhwaan al-Muslimuun inapohusiana na haki na utiifu, mtu ataona kuwa hawako juu ya ´Aqiydah sahihi nzuri.


  • Author: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • http://youtu.be/yZ32N9HGTUM
  • Kitengo: Uncategorized , al-Qaradhwaawiy, Yuusuf
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 19th, October 2013