´Allaamah al-Luhaydaan Kuhusu Usaamah bin Laadin

Ama yanayosemwa kuhusu Usaamah, sisi hatujui yaliyo baina yake yeye na Allaah. Lakini dhahiri ni kwamba ni mtu ambaye analingania katika shari na anaeneza ufisadi katika ardhi. Hatukuwa tukisikia kukiongelewa juu ya matunda yake ya kheri na tukayajua. Ama kuhusu propaganda na maneno yake, yanaonesha kuwa ni mjinga wakati anadhani kuwa ni mjuzi. Inawezekana kukawa nyuma yake pia wanaojaribu kuharibu nchi hii na nchi zingine za Kiislamu. Siwezi kusema kwamba nyuma yake kuna mashariki na magharibi, lakini ni lazima nyuma yake kuwepo watu waovu. Na si jambo la sawa kwamba ni mlinganiaji (Daa´iyah) au ni mtengenezaji. Na ikiwa mtu atasema kuwa ni miongoni mwa jumla ya wanaoeneza ufisadi, ndivyo inavyoonekana kwa nje.

Ama yanayosemwa kuhusu Usaamah, sisi hatujui yaliyo baina yake yeye na Allaah. Lakini dhahiri ni kwamba ni mtu ambaye analingania katika shari na anaeneza ufisadi katika ardhi.

Hatukuwa tukisikia kukiongelewa juu ya matunda yake ya kheri na tukayajua.

Ama kuhusu propaganda na maneno yake, yanaonesha kuwa ni mjinga wakati anadhani kuwa ni mjuzi.

Inawezekana kukawa nyuma yake pia wanaojaribu kuharibu nchi hii na nchi zingine za Kiislamu. Siwezi kusema kwamba nyuma yake kuna mashariki na magharibi, lakini ni lazima nyuma yake kuwepo watu waovu.

Na si jambo la sawa kwamba ni mlinganiaji (Daa´iyah) au ni mtengenezaji. Na ikiwa mtu atasema kuwa ni miongoni mwa jumla ya wanaoeneza ufisadi, ndivyo inavyoonekana kwa nje.