´Allaamah al-Luhaydaan Kuhusu Kauli Ya al-´Ar´uur Kushikamana Na Kamba Ya Allaah

Swali: Mtu mmoja maarufu, anayezingatiwa kuwa ni mlinganizi kwa mujibu wa watu wengi, amesema katika chaneli tarehe 12-03-2012/29-04-1433: “Allaah Mtukufu ameamrisha hili, ameamrisha umoja. Uovu uko wapi katika hili? Ametakasika Allaah! Anasema kuwaambia nyumati, walimwengu na wauumini: وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا “Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja.” (03:103) Hajasema shikamaneni na kundi fulani. Zingatia kwamba hajasema vilevile aminini na shikamaneni na Mtume fulani na msishikamane na Mitume wengine. Hili ni suala muhimu... Enyi watu mlioko kila mahala! Enyi waislamu mlioko kila mahala!” al-Luhaydaan: Huyu ni mlinganizi? Muulizaji: Haya ni maneno yake. Anajulikana katika TV. al-Luhaydaan: Kila kinachojulikana kinatolea dalili ya uzuri? Muulizaji: Swali linahusiana na hili. al-Luhaydaan: Ametakasika Allaah! Muulizaji: Tunaendelea na swali. al-Luhaydaan: Huu ni upotevu wa wazi kabisa. Muulizaji: [Anasema]: “Enyi Waislamu mlioko kila mahala! Enyi wakristo mlioko kila mahala! Aayah hii inasema: وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا “Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja.” (03:103) Ina maana hata mkristo anatakiwa kushikamana na kamba ya Allaah. Kadhalika myahudi. Namna hii ndio dini zitakuwa na umoja. Dini zitakuwa na umoja ikiwa zitashikamana na kamba ya Allaah sahihi. Bi maana kwa Injiyl ambayo imeteremka kwa ´Iysaa (´alayhis-Swalaat was-Salaam), Tawrat ambayo imeteremka kwa Muusa na Qur-aan ambayo imeteremka kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio kamba ya Allaah. Zote hizo ni kamba ya Allaah kwa kuwa vinatoka kwa Mola Mmoja. Tushikamane nazo. Ikiwa tutashikamana nazo kweli kweli tutakuwa tumeshikamana na yaliyoteremshwa katika vitabu vitatu, basi hapo tutakuwa tumeshikamana na kamba ya Allaah.” Ni yapi maoni yako kuhusu hili? Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Hakuna myahudi wala mnaswara anayejua kuhusu mimi kisha akanikanusha, isipokuwa ni katika watu wa Motoni.” Huku sio kushikamana kabisa na kamba ya Allaah. Vitabu vimefutwa. Hata kama ndani yavyo kuna sehemu ya mambo ya awali, vimegeuzwa. Mwenye kuita katika hili basi mtuhumuni Uislamu wake. Bi maana mwenye kuita katika Qur-aan, Injiyl na Tawrat kuwa kama marejeleo na kwa njia ya kwamba mtu haisihi Imani yake isipokuwa mpaka akitendea kazi moja katika hivyo. Tunamuomba Allaah afya.

Swali: Mtu mmoja maarufu, anayezingatiwa kuwa ni mlinganizi kwa mujibu wa watu wengi, amesema katika chaneli tarehe 12-03-2012/29-04-1433:

“Allaah Mtukufu ameamrisha hili, ameamrisha umoja. Uovu uko wapi katika hili? Ametakasika Allaah! Anasema kuwaambia nyumati, walimwengu na wauumini:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا
“Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja.” (03:103)

Hajasema shikamaneni na kundi fulani. Zingatia kwamba hajasema vilevile aminini na shikamaneni na Mtume fulani na msishikamane na Mitume wengine. Hili ni suala muhimu… Enyi watu mlioko kila mahala! Enyi waislamu mlioko kila mahala!”

al-Luhaydaan: Huyu ni mlinganizi?

Muulizaji: Haya ni maneno yake. Anajulikana katika TV.

al-Luhaydaan: Kila kinachojulikana kinatolea dalili ya uzuri?

Muulizaji: Swali linahusiana na hili.

al-Luhaydaan: Ametakasika Allaah!

Muulizaji: Tunaendelea na swali.

al-Luhaydaan: Huu ni upotevu wa wazi kabisa.

Muulizaji: [Anasema]:

“Enyi Waislamu mlioko kila mahala! Enyi wakristo mlioko kila mahala! Aayah hii inasema:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا
“Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja.” (03:103)

Ina maana hata mkristo anatakiwa kushikamana na kamba ya Allaah. Kadhalika myahudi. Namna hii ndio dini zitakuwa na umoja. Dini zitakuwa na umoja ikiwa zitashikamana na kamba ya Allaah sahihi. Bi maana kwa Injiyl ambayo imeteremka kwa ´Iysaa (´alayhis-Swalaat was-Salaam), Tawrat ambayo imeteremka kwa Muusa na Qur-aan ambayo imeteremka kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio kamba ya Allaah. Zote hizo ni kamba ya Allaah kwa kuwa vinatoka kwa Mola Mmoja. Tushikamane nazo. Ikiwa tutashikamana nazo kweli kweli tutakuwa tumeshikamana na yaliyoteremshwa katika vitabu vitatu, basi hapo tutakuwa tumeshikamana na kamba ya Allaah.”

Ni yapi maoni yako kuhusu hili?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Hakuna myahudi wala mnaswara anayejua kuhusu mimi kisha akanikanusha, isipokuwa ni katika watu wa Motoni.”

Huku sio kushikamana kabisa na kamba ya Allaah. Vitabu vimefutwa. Hata kama ndani yavyo kuna sehemu ya mambo ya awali, vimegeuzwa. Mwenye kuita katika hili basi mtuhumuni Uislamu wake. Bi maana mwenye kuita katika Qur-aan, Injiyl na Tawrat kuwa kama marejeleo na kwa njia ya kwamba mtu haisihi Imani yake isipokuwa mpaka akitendea kazi moja katika hivyo. Tunamuomba Allaah afya.