´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Kuwajeruhi Ahl-ul-Bid´ah Na Kanuni Za ´Adnaan ´Ar´uur

Muulizaji: Sisi tuna baadhi ya kanuni. Tulikuwa tunapenda kusikia kutoka kwako kama zinaafikiana na misingi ya Ahl-us-Sunnah. Kauli ya kwanza inasema "Tunasahihisha na wala hatujeruhi (Jarh)". Wasemaje kuhusiana nayo? ´Allaamah al-Fawzaan: Haina asli. Haina asli. Watu wa batili lazima kuwajeruhi. Muulizaji: Kanuni ya pili "Ukihukumu utahukumiwa, na ukilingania utapewa ujira". Wasemaje kwa kanuni hii? ´Allaamah al-Fawzaan: Imezushwa haina asli. Lazima kuwahukumu watu wa batili. Muulizaji: Kanuni ya tatu inasema "Katika uadilifu na Inswaaf ni kutaja mazuri na mabaya." Aliesema hivi, anatoa dalili kwa mfumo wa haki sawa kwa Hadiyth maarufu: "Kasema kweli lakini ni muongo." Wasemaje kuhusu hili? ´Allaamah al-Fawzaan: Hili ni batili pia. Maneno haya ni batili pia. Allaah Kataja mabaya ya washirikina na wala Hakutaja mazuri yao. Muulizaji: Je, lahusiana na Ahl-ul-Bid´ah pia? ´Allaamah al-Fawzaan: Kitu gani na Ahl-ul-Bid´ah? Muulizaji: Yaani yeye anasema pia kuwa katika uadilifu na inswaaf ni kutaja mazuri ya Ahl-ul-Bid´ah na... ´Allaamah al-Fawzaan: Wote ni sawa. Kulitajwa mabaya yao na hakukutajwa mazuri yao. Allaah Kataja mabaya ya maadui na wala Hakutaja mazuri yao. Je, hizi ni kanuni za ´Ar´uur? Muulizaji: Ndio. Ni kanuni zake. ´Allaamah al-Fawzaan: Ndio, zote hizi zimetupwa na ni batili. Kapigwa Radd katika vitabu vingi. Muulizaji: Kanuni ya nne "Inajuzu kusema kosa la mtu, na ni Haramu kumponda". Kanuni hii ni sahihi? ´Allaamah al-Fawzaan: Hii ndio kama ile "Tunasahihisha wala hatujeruhi". Ni mamoja. Muulizaji: Aliitolea dalili na kusema kwa nini Imaam Ahmad hakuhukumiwa kwa kufanya Takfiyr kwa mwenye kuacha Swalah na analaumiwa Sayyid Qutwub kwa baadhi ya ibara zake na kusema kuwa huyu anakufurisha jamii na wala halaumiwi Imaam Ahmad (Rahimahu Allaaah) ambaye kafanya Takfiyr kwa Ummah mzima? Wasemaje? ´Allaamah al-Fawzaan: Imaam Ahmad ni mwanachuoni kigogo. Anajua dalili na jinsi ya kuzitumia. Na Sayyid Qutwub ni mjinga hana elimu wala ujuzi. Wala hana dalili ya anayosema. Kumlinganisha Sayyid Qutwub na Imaam Ahmad hii ni dhuluma. Muulizaji: Anasema pia kuwa hajui yeyote alieongelea mambo ya mfumo katika uso wa ardhi leo kama Sayyid Qutwub na mengi aliyoandika ni sahihi. Alipoulizwa kuhusu madai yake haya akajibu kuwa "mambo ya mfumo" hapa anakusudia kupiga kura na mauaji na "zama" anakusudia karne khamsini zilizopita... ´Allaamah al-Fawzaan: Yeye hajui. Hajui kwa kuwa ni mjinga. Ama sisi tunajua - Alhamdulillaah - wanachuoni wa kabla ya Sayyid Qutwub na wa baada yake hawakubaliani na Sayyid Qutwub. Muulizaji: Anasema pia kuwa kuna ulinganio wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao ni kujeruhi watu kwa kosa au ibara ya utata na [... sauti haiko wazi... ]. Wasemaje kwa ibara hii? ´Allaamah al-Fawzaan: Ni maneno matupu. Makusudio yake ni kusapoti batili na kutetea watu wa batili. Muulizaji: Anasema pia mtu akiangalia sababu za makundi kufarakana ataona kuwa ni sababu za kitabia na si za ki-Itikadi wala ki-Manhaj. Je, hili ni sahihi? ´Allaamah al-Fawzaan: Sababu ni za ki-Itikadi na si za kitabia. Na anataka kuzisitiri. Muulizaji: Wasemaje kuhusiana na yeye? ´Allaamah al-Fawzaan: Sio mwanachuoni. Alikuja Saudi Arabia kikazi. Baadaye ndo akawa amejidhihirisha hivyo. Muulizaji: Nasaha yako ya mwisho vipi tuhudhurie Duruus zake au hapana? Anakuja Europe. Je, uwanasihi vijana wa ki-Salafiy kuhudhuria. ´Allaamah al-Fawzaan: Ninawanasihi vijana wa Ki-Salafiy kumkata na kutohudhuria Duruus zake na watu mfano wake. Duruus zake? ´Allaamah al-Fawzaan: Ninawanasihi vijana wa Ki-Salafiy kumkata na kutohudhuria duruus zake na watu mfano wake.

Muulizaji:
Sisi tuna baadhi ya kanuni. Tulikuwa tunapenda kusikia kutoka kwako kama zinaafikiana na misingi ya Ahl-us-Sunnah. Kauli ya kwanza inasema “Tunasahihisha na wala hatujeruhi (Jarh)”. Wasemaje kuhusiana nayo?

´Allaamah al-Fawzaan:
Haina asli. Haina asli. Watu wa batili lazima kuwajeruhi.

Muulizaji:
Kanuni ya pili “Ukihukumu utahukumiwa, na ukilingania utapewa ujira”. Wasemaje kwa kanuni hii?

´Allaamah al-Fawzaan:
Imezushwa haina asli. Lazima kuwahukumu watu wa batili.

Muulizaji:
Kanuni ya tatu inasema “Katika uadilifu na Inswaaf ni kutaja mazuri na mabaya.” Aliesema hivi, anatoa dalili kwa mfumo wa haki sawa kwa Hadiyth maarufu:
“Kasema kweli lakini ni muongo.”

Wasemaje kuhusu hili?

´Allaamah al-Fawzaan:
Hili ni batili pia. Maneno haya ni batili pia. Allaah Kataja mabaya ya washirikina na wala Hakutaja mazuri yao.

Muulizaji:
Je, lahusiana na Ahl-ul-Bid´ah pia?

´Allaamah al-Fawzaan:
Kitu gani na Ahl-ul-Bid´ah?

Muulizaji:
Yaani yeye anasema pia kuwa katika uadilifu na inswaaf ni kutaja mazuri ya Ahl-ul-Bid´ah na…

´Allaamah al-Fawzaan:
Wote ni sawa. Kulitajwa mabaya yao na hakukutajwa mazuri yao. Allaah Kataja mabaya ya maadui na wala Hakutaja mazuri yao. Je, hizi ni kanuni za ´Ar´uur?

Muulizaji:
Ndio. Ni kanuni zake.

´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, zote hizi zimetupwa na ni batili. Kapigwa Radd katika vitabu vingi.

Muulizaji:
Kanuni ya nne “Inajuzu kusema kosa la mtu, na ni Haramu kumponda”. Kanuni hii ni sahihi?

´Allaamah al-Fawzaan:
Hii ndio kama ile “Tunasahihisha wala hatujeruhi”. Ni mamoja.

Muulizaji:
Aliitolea dalili na kusema kwa nini Imaam Ahmad hakuhukumiwa kwa kufanya Takfiyr kwa mwenye kuacha Swalah na analaumiwa Sayyid Qutwub kwa baadhi ya ibara zake na kusema kuwa huyu anakufurisha jamii na wala halaumiwi Imaam Ahmad (Rahimahu Allaaah) ambaye kafanya Takfiyr kwa Ummah mzima? Wasemaje?

´Allaamah al-Fawzaan:
Imaam Ahmad ni mwanachuoni kigogo. Anajua dalili na jinsi ya kuzitumia. Na Sayyid Qutwub ni mjinga hana elimu wala ujuzi. Wala hana dalili ya anayosema. Kumlinganisha Sayyid Qutwub na Imaam Ahmad hii ni dhuluma.

Muulizaji:
Anasema pia kuwa hajui yeyote alieongelea mambo ya mfumo katika uso wa ardhi leo kama Sayyid Qutwub na mengi aliyoandika ni sahihi. Alipoulizwa kuhusu madai yake haya akajibu kuwa “mambo ya mfumo” hapa anakusudia kupiga kura na mauaji na “zama” anakusudia karne khamsini zilizopita…

´Allaamah al-Fawzaan:
Yeye hajui. Hajui kwa kuwa ni mjinga. Ama sisi tunajua – Alhamdulillaah – wanachuoni wa kabla ya Sayyid Qutwub na wa baada yake hawakubaliani na Sayyid Qutwub.

Muulizaji:
Anasema pia kuwa kuna ulinganio wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao ni kujeruhi watu kwa kosa au ibara ya utata na [… sauti haiko wazi… ]. Wasemaje kwa ibara hii?

´Allaamah al-Fawzaan:
Ni maneno matupu. Makusudio yake ni kusapoti batili na kutetea watu wa batili.

Muulizaji:
Anasema pia mtu akiangalia sababu za makundi kufarakana ataona kuwa ni sababu za kitabia na si za ki-Itikadi wala ki-Manhaj. Je, hili ni sahihi?

´Allaamah al-Fawzaan:
Sababu ni za ki-Itikadi na si za kitabia. Na anataka kuzisitiri.

Muulizaji:
Wasemaje kuhusiana na yeye?

´Allaamah al-Fawzaan:
Sio mwanachuoni. Alikuja Saudi Arabia kikazi. Baadaye ndo akawa amejidhihirisha hivyo.

Muulizaji:
Nasaha yako ya mwisho vipi tuhudhurie Duruus zake au hapana? Anakuja Europe. Je, uwanasihi vijana wa ki-Salafiy kuhudhuria.

´Allaamah al-Fawzaan:
Ninawanasihi vijana wa Ki-Salafiy kumkata na kutohudhuria Duruus zake na watu mfano wake. Duruus zake?

´Allaamah al-Fawzaan:
Ninawanasihi vijana wa Ki-Salafiy kumkata na kutohudhuria duruus zake na watu mfano wake.