´Allaamah al-´Abbaad Kuhusu Waislamu Kuwaomba Msaada Makafiri

Waislamu hawawaombi msaada makafiri ikiwa kama hakuna haja ya kufanya hivyo. Jambo hili inakuwa ni maalum kwa Waislamu. Ama kukihitajika msaada kutokana na madhara makubwa na hayazimiki isipokuwa mpaka kwa kutaka msaada kwa wasiokuwa Waislamu katika ambao wanaweza kuzuia uadui na dhuluma hii, hakuna neno kufanya hivi. Hili ni mfano wa mtu ambaye anaishi na jirani ambaye ni myahudi au mnaswara. Kisha akavamiwa na majambazi wanaotaka kumuangamiza yeye na familia yake na mali yake, je, aombe kutoka msaada kwa jirani yake huyu? Ndio, aombe msaada hakuna neno kufanya hivyo wakati wa haja. Asiseme huyu kwa kweli ni kafiri na hawezi kunisaidia na badala yake mwache huyu adui afanye ya kufanya na wala asiombe msaada kwa kafiri. Hapana.

Waislamu hawawaombi msaada makafiri ikiwa kama hakuna haja ya kufanya hivyo. Jambo hili inakuwa ni maalum kwa Waislamu. Ama kukihitajika msaada kutokana na madhara makubwa na hayazimiki isipokuwa mpaka kwa kutaka msaada kwa wasiokuwa Waislamu katika ambao wanaweza kuzuia uadui na dhuluma hii, hakuna neno kufanya hivi.

Hili ni mfano wa mtu ambaye anaishi na jirani ambaye ni myahudi au mnaswara. Kisha akavamiwa na majambazi wanaotaka kumuangamiza yeye na familia yake na mali yake, je, aombe kutoka msaada kwa jirani yake huyu? Ndio, aombe msaada hakuna neno kufanya hivyo wakati wa haja. Asiseme huyu kwa kweli ni kafiri na hawezi kunisaidia na badala yake mwache huyu adui afanye ya kufanya na wala asiombe msaada kwa kafiri. Hapana.