´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh Kuhusu Vigawanyo Vitatu Vya Tawhiyd

´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh: Wakati Muislamu atapoangalia Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ataona ya kuwa Tawhiyd imeongelewa kwa mambo matatu: - Aina ya kwanza ni Tawhiyd ya kumpwekesha Mola kwa Matendo Yake, kwa Kuumba, Kuruzuku, Kuhuisha, Kufisha, Kuendesha na Kumiliki ulimwengu wote. Na ulimwengu wote ni wenye kunyenyekea Kwake. Hili ni jambo muhimu sana. Umpwekesha Allaah kwa Matendo Yake. Uitakidi ya kwamba hakuna Muumba na Mwenye Kuruzuku asiyekuwa Yeye, wala hana mshirika katika Kuumba na Kuuendesha Kwkae mambo. Bali Yeye Mwenyewe ndiye Mwendeshaji wa ulimwengu wote. Ulimwengu wote ni wenye kunyenyekea Kwake. إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ "Hakika Amri Yake Akitaka kitu chochote (kile), hukiambia: “Kun (Kuwa), nacho huwa".” (36:82) إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَـٰنِ عَبْدًا "Hakuna yeyote (yule aliyomo) katika mbingu na ardhi isipokuwa (Siku ya kufufuliwa) atamfikia Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) kuwa ni mja." (19:93) تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا "Zinamsabihi mbingu saba, na ardhi, na vilivyomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinamsabihi kwa Himdi Zake, lakini hamzifahamu tasbiyh zao. Hakika Yeye daima ni Haliyman-Ghafuwraa Mpole wa kuvumilia waja - Mwingi wa kughufuria)." (17:44) Na aina hii wameikubali watu wote ila tu watu wachache mno. Na wengi waliopinga aina hii wamefany hivyo kwa jeuri na kiburi. Kama Alivyosema Allaah kuhusu Fir´awn, Fir´awm huyu aliyesema: فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ "Akasema: “Mimi ni Mola wenu mkuu".” (79:24) Akasema tena: مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرِي "Sijui kama mnaye ilaah (Mungu) badala yangu." (28:38) Pamoja na hivyo Akasema Allaah: وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا ۚ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ "Wakazikanusha (kwa dhulma na majivuno) na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha (kuwa aliyokuja nayo Nabii Muwsaa ni ya kweli kutoka ni kwa Allaah). Basi tazama vipi ilikuwa mwisho wa mafisadi." (27:14) Hivyo, yaonesha ya kwamba Fir´awm alikuwa akikubali moyoni mwake ya kwamba Allaah ndiye Muumba na Mwenye Kuruzuku, lakini kutokana na kiburi chake na upotofu wake akaingia kwa aliyoingia: فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ "Basi aliwaghilibu (aliwachezea akili) watu wake, nao wakamtii. Hakika wao (wenyewe) walikuwa watu mafasiki." (43:54) Kumpwekesha Allaah kwa Matendo Yake, na kwamba kila kilichomo ndani ya ulimwengu ni kiumbe cha Allaah (´Azza wa Jalla) na Yeye ndiye Anakiendesha. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa): قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ "Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, hivi nyinyi mnamkufuru Yule Aliyeumba ardhi kwa siku mbili, na mnamfanyia washirika (waliolingana Naye)? Huyo Ndiye Mola wa walimwengu.” وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِن فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِّلسَّائِلِينَ "Na Akajaalia humo (ardhini) milima juu yake, na Akabariki humo, na Akakadiria humo (kwa viumbe vinavyoishi humo) kuti yake katika siku nne zilizo sawasawa kwa wanaouliza (kuhusu uumbaji Wake)." ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ "Kisha Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah) kuzielekea mbingu nazo ni moshi; Akaiambia (mbingu) na ardhi: “Njooni mkiwa mmetii (kwa khiari) au kukirihika.” (Mbingu na ardhi) Zikasema: “Tumekuja hali ya kuwa wenye utiifu".” فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِي كُلِّ سَمَاءٍ أَمْرَهَا "Akamaliza kuziumba mbingu saba katika siku mbili, na Akatia ilhamu katika kila mbingu amri yake." (41:09-12) Yeye ndiye wa Kwanza na hapakuwa kabla Yake kitu, na wa Mwisho hakuna baada Yake kitu, wa Dhahihiri na hakuna juu yake kitu, na wa Ndani na hakuna chini Yake kitu. Anajua kila kitu. يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ "(Allaah) Anajua khiyana za macho na yale (yote) yanayoficha vifua." (40:19) وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ "Na Kwake (Allaah) Pekee zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua. Na wala (haianguki) punje katika viza vya ardhi, na wala (hakianguki) kilichorutubika na wala (hakianguki) kikavu isipokuwa (kimeandikwa) katika Kitabu kinachobainisha (Lawhum-Mahfuwdhw)." (06:59) - Aina ya pili ni kumpwekesha Allaah kwa matendo ya waja. Waja wampwekesha Mola wao kwa matendo yao; kuanzia Du´aa, Swalah, kuchinja, nadhiri, kurejea, shauku, kuwa na khofu na kushtakia, kunyenyekea, yote hayo yafanyiwe Allaah Mmoja. Du´aa isiwe kwa yeyote isipokuwa Allaah, kwa kuwa Mwenye kuomba Anayemuomba ni Mwenye Uwezo, Yupo, Anasikia, Anaona n.k. Mambo haya hayamstahiki ila Allaah. Maiti na visivyoonekana vipi vitaombwa? Kwa kuwa havisikii Du´aa ya mwenye kuviomba, na lau watasikia hawatoweza kuwajibu. Na Siku ya Qiyaamah watawakanusha, kila mwenye kuabudiwa atamkanusha aliyemuabudu; kama Malaika, ´Iysa na wengineo. Kwa hivyo, kumpwekesha Allaah kwa matendo ya waja, kwa kumchinjia, kuangalilia Kwake. Tunapochinja tukusudie kujikurubisha kwa Allaah kwa kusema "Bismi Allaah". Tunapoomba tusimuombee Mtume, walii, mtu mwema, mtu asiyekuwepo, jini; bali tumuombe mtu aliye hai, mwenye kusikia, kuona, mjuzi na mwenye uwezo wa unachomuomba. Ama kumuendee maiti aliye ndani ya kaburi lake tangu miaka mia na kumwambia: "Ewe fulani niombee kwa Mola Wako", "tuombee", "mponye mgonjwa wetu", "tutatulie haja zetu", mambo gani haya? Yote haya yanatokana na kuwa na akili pungufu. Kama Alivyosema Allaah: وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ "Kwa yakini Tumeuumbia (Moto wa) Jahannam wengi katika majini na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi." (07:179) Kumpwekesha Allaah kwa matendo ya waja ndio ilikuwa Da´wah ya Mitume, kwa kuwa kila Mtume Aliyemtuma Allaah alianza kuwalingania watu wake kwa kusema: اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ "Mwabuduni Allaah (kwani nyinyi) hamna ilaah ghairi Yake." (07:59) Anawalingania katika laa ilaaha illa Allaah, anawalingania ya kwamba muabudiwa ulimwenguni ni Mmoja tu, na ndiye Mwenye Kustahiki. Na kuwa kila kinachoabudiwa na kuombwa hakina haki wala maana yoyote isipokuwa ni upotofu na dhuluma. Wakakataa na kusema: أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ “Amewafanya miungu (wote) kuwa ni Ilaah Mmoja? (38:05) Sisi tulikuwa tunataka kuwepo waabudiwa ishirini au sabini. Husayn alikuwa anaabudu mungu wa saba. Alimuuliza Mtume una mungu wa ngapi? Akasema: "Saba, Mmoja Aliye mbinguni na sita ardhini." Akamuuliza: "Ni nani unayerejea kwake wakati wa matumaini na khofu?" Akasema: "Ni Yule Aliye mbinguni." Akamwambia: "Acha hao sita na umuabudu huyo Mmoja Aliye mbinguni, ntakufunza maneno: "Sema eeh Allaah niongoze na nikinge na shari za nafsi yangu." Hivyo, Muhammad aliwalingania waarabu katika laa ilaaha illa Allaah, kuitamka, kuifanyia kazi muqtadhwa yake, lakini waarabu walikuwa wanafahamu ukweli na maana ya laa ilaaha illa Allaah. Na kwa ajili ya hili ndio maana walikataa kuitamka. Allaah Anasema kuhusu wao: إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ "Hakika wao walipokuwa wakiambiwa: “Laa ilaaha illa Allaah” (Hapana ilaaha ila Allaah, walikuwa) hutakabari. Na (pia walikuwa) wanasema: “Je, tuache miungu yetu kwa ajili ya mshairi majnuni?!” (37:35-36) Huu ni uongo. Alikuwa mshairi mwendawazimu? Yaani watafuta hoja tu baada ya kukataa kusema laa ilaaha illa Allaah na kuleta muqtadhwa yake; kumtakasia Allaah ´Ibaadah kwa kuacha kila kinachoabudiwa badala ya Allaah na kumfanya ´Ibaadah zote Allaah asiyekuwa na mshirika katika hilo. - Aina ya tatu ni yale Aliyoyataja Allaah katika Kitabu Chake, kwa kutaja Sifa Zake na Majina Yake. Allaah Kajiita na Kujisifu Mwenyewe kwa Majina na Sifa, na Majina na Sifa zote hizi zinatolewa dalili na Qur-aan na Sunnah. Tunayaamini. Tunamsifu Allaah kuwa Yuko na Elimu, Rahmah, Anaghadhibika, Anaridhia, Anakasirika, Yuko juu, Huteremka; tunamsifu Allaah kwa yote haya. Tunamsifu kwa Kustawaa Kwake juu ya ´Arshi Yake, kuwa Kwake juu ya viumbe Vyake, Elimu yake Kamili, tunamwita kwa Majina Yake; Haliym, Qadiyr, Ghafuur, Rahiym, Rahmaan, Rahiym. Majina na Sifa zote za Allaah tunazikubali na kuziamini. Na tunamwachia Kauli Yake: لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ "Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye As-Samiy’ul-Baswiyr (Mwenye kusikia yote daima, Mwenye kuona yote daima)." (42:11) Tunamthibitishia Allaah Usikivu na Kuona, lakini Kusikia Kwake si kama kusikia kwa viumbe, wala Kuona Kwake si kama kuona kwa viumbe, bali [Sifa Zake] zinalingana na Utukufu na Ukubwa Wake: فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ "Basi msipigie mifano Allaah (kwani hakuna kinachofanana Naye kabisa!) Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui." (16:74) Sifa ambazo zinabadilishwa kuzisifu kwa uhakika wake, au zimekanushwa na kupingwa, zote hizo zimethibiti kwa njia ya upokezi na Ah-us-Sunnah wanazithibitisha kwa Utukufu na Ukubwa unaolingana na Allaah. Hawakuziharibu wala kuzifananisha na wala kuzipigia mifano, bali wamezithibitisha kutokana na kutolewa kwake dalili ya Kitabu na Sunnah. Aina hizi za Tawhiyd zipo ndani ya Qur-aan. Na watu wanaosema ya kwamba ni Ibn Taymiyyah na Ibn ´Abdul-Wahhaab (Rahimahumu Allaah) wao ndio walileta vigawanyo hivi, haya yote ni makosa. Soma Qur-aan ujione mwenyewe ukweli wa mambo.

´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh:

Wakati Muislamu atapoangalia Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ataona ya kuwa Tawhiyd imeongelewa kwa mambo matatu:

– Aina ya kwanza ni Tawhiyd ya kumpwekesha Mola kwa Matendo Yake, kwa Kuumba, Kuruzuku, Kuhuisha, Kufisha, Kuendesha na Kumiliki ulimwengu wote. Na ulimwengu wote ni wenye kunyenyekea Kwake. Hili ni jambo muhimu sana. Umpwekesha Allaah kwa Matendo Yake. Uitakidi ya kwamba hakuna Muumba na Mwenye Kuruzuku asiyekuwa Yeye, wala hana mshirika katika Kuumba na Kuuendesha Kwkae mambo. Bali Yeye Mwenyewe ndiye Mwendeshaji wa ulimwengu wote. Ulimwengu wote ni wenye kunyenyekea Kwake.

إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ
“Hakika Amri Yake Akitaka kitu chochote (kile), hukiambia: “Kun (Kuwa), nacho huwa”.” (36:82)

إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَـٰنِ عَبْدًا
“Hakuna yeyote (yule aliyomo) katika mbingu na ardhi isipokuwa (Siku ya kufufuliwa) atamfikia Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) kuwa ni mja.” (19:93)

تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا
“Zinamsabihi mbingu saba, na ardhi, na vilivyomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinamsabihi kwa Himdi Zake, lakini hamzifahamu tasbiyh zao. Hakika Yeye daima ni Haliyman-Ghafuwraa Mpole wa kuvumilia waja – Mwingi wa kughufuria).” (17:44)

Na aina hii wameikubali watu wote ila tu watu wachache mno. Na wengi waliopinga aina hii wamefany hivyo kwa jeuri na kiburi. Kama Alivyosema Allaah kuhusu Fir´awn, Fir´awm huyu aliyesema:

فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ
“Akasema: “Mimi ni Mola wenu mkuu”.” (79:24)

Akasema tena:

مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرِي
“Sijui kama mnaye ilaah (Mungu) badala yangu.” (28:38)

Pamoja na hivyo Akasema Allaah:

وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا ۚ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ
“Wakazikanusha (kwa dhulma na majivuno) na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha (kuwa aliyokuja nayo Nabii Muwsaa ni ya kweli kutoka ni kwa Allaah). Basi tazama vipi ilikuwa mwisho wa mafisadi.” (27:14)

Hivyo, yaonesha ya kwamba Fir´awm alikuwa akikubali moyoni mwake ya kwamba Allaah ndiye Muumba na Mwenye Kuruzuku, lakini kutokana na kiburi chake na upotofu wake akaingia kwa aliyoingia:

فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ
“Basi aliwaghilibu (aliwachezea akili) watu wake, nao wakamtii. Hakika wao (wenyewe) walikuwa watu mafasiki.” (43:54)

Kumpwekesha Allaah kwa Matendo Yake, na kwamba kila kilichomo ndani ya ulimwengu ni kiumbe cha Allaah (´Azza wa Jalla) na Yeye ndiye Anakiendesha. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ
“Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, hivi nyinyi mnamkufuru Yule Aliyeumba ardhi kwa siku mbili, na mnamfanyia washirika (waliolingana Naye)? Huyo Ndiye Mola wa walimwengu.”

وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِن فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِّلسَّائِلِينَ
“Na Akajaalia humo (ardhini) milima juu yake, na Akabariki humo, na Akakadiria humo (kwa viumbe vinavyoishi humo) kuti yake katika siku nne zilizo sawasawa kwa wanaouliza (kuhusu uumbaji Wake).”

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ
“Kisha Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah) kuzielekea mbingu nazo ni moshi; Akaiambia (mbingu) na ardhi: “Njooni mkiwa mmetii (kwa khiari) au kukirihika.” (Mbingu na ardhi) Zikasema: “Tumekuja hali ya kuwa wenye utiifu”.”

فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِي كُلِّ سَمَاءٍ أَمْرَهَا
“Akamaliza kuziumba mbingu saba katika siku mbili, na Akatia ilhamu katika kila mbingu amri yake.” (41:09-12)

Yeye ndiye wa Kwanza na hapakuwa kabla Yake kitu, na wa Mwisho hakuna baada Yake kitu, wa Dhahihiri na hakuna juu yake kitu, na wa Ndani na hakuna chini Yake kitu. Anajua kila kitu.

يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ
“(Allaah) Anajua khiyana za macho na yale (yote) yanayoficha vifua.” (40:19)

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ
“Na Kwake (Allaah) Pekee zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua. Na wala (haianguki) punje katika viza vya ardhi, na wala (hakianguki) kilichorutubika na wala (hakianguki) kikavu isipokuwa (kimeandikwa) katika Kitabu kinachobainisha (Lawhum-Mahfuwdhw).” (06:59)

– Aina ya pili ni kumpwekesha Allaah kwa matendo ya waja. Waja wampwekesha Mola wao kwa matendo yao; kuanzia Du´aa, Swalah, kuchinja, nadhiri, kurejea, shauku, kuwa na khofu na kushtakia, kunyenyekea, yote hayo yafanyiwe Allaah Mmoja. Du´aa isiwe kwa yeyote isipokuwa Allaah, kwa kuwa Mwenye kuomba Anayemuomba ni Mwenye Uwezo, Yupo, Anasikia, Anaona n.k. Mambo haya hayamstahiki ila Allaah. Maiti na visivyoonekana vipi vitaombwa? Kwa kuwa havisikii Du´aa ya mwenye kuviomba, na lau watasikia hawatoweza kuwajibu. Na Siku ya Qiyaamah watawakanusha, kila mwenye kuabudiwa atamkanusha aliyemuabudu; kama Malaika, ´Iysa na wengineo. Kwa hivyo, kumpwekesha Allaah kwa matendo ya waja, kwa kumchinjia, kuangalilia Kwake. Tunapochinja tukusudie kujikurubisha kwa Allaah kwa kusema “Bismi Allaah”. Tunapoomba tusimuombee Mtume, walii, mtu mwema, mtu asiyekuwepo, jini; bali tumuombe mtu aliye hai, mwenye kusikia, kuona, mjuzi na mwenye uwezo wa unachomuomba. Ama kumuendee maiti aliye ndani ya kaburi lake tangu miaka mia na kumwambia: “Ewe fulani niombee kwa Mola Wako”, “tuombee”, “mponye mgonjwa wetu”, “tutatulie haja zetu”, mambo gani haya? Yote haya yanatokana na kuwa na akili pungufu. Kama Alivyosema Allaah:

وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ
“Kwa yakini Tumeuumbia (Moto wa) Jahannam wengi katika majini na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi.” (07:179)

Kumpwekesha Allaah kwa matendo ya waja ndio ilikuwa Da´wah ya Mitume, kwa kuwa kila Mtume Aliyemtuma Allaah alianza kuwalingania watu wake kwa kusema:

اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ
“Mwabuduni Allaah (kwani nyinyi) hamna ilaah ghairi Yake.” (07:59)

Anawalingania katika laa ilaaha illa Allaah, anawalingania ya kwamba muabudiwa ulimwenguni ni Mmoja tu, na ndiye Mwenye Kustahiki. Na kuwa kila kinachoabudiwa na kuombwa hakina haki wala maana yoyote isipokuwa ni upotofu na dhuluma. Wakakataa na kusema:

أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ
“Amewafanya miungu (wote) kuwa ni Ilaah Mmoja? (38:05)

Sisi tulikuwa tunataka kuwepo waabudiwa ishirini au sabini. Husayn alikuwa anaabudu mungu wa saba. Alimuuliza Mtume una mungu wa ngapi? Akasema:

“Saba, Mmoja Aliye mbinguni na sita ardhini.” Akamuuliza: “Ni nani unayerejea kwake wakati wa matumaini na khofu?” Akasema: “Ni Yule Aliye mbinguni.” Akamwambia: “Acha hao sita na umuabudu huyo Mmoja Aliye mbinguni, ntakufunza maneno: “Sema eeh Allaah niongoze na nikinge na shari za nafsi yangu.”

Hivyo, Muhammad aliwalingania waarabu katika laa ilaaha illa Allaah, kuitamka, kuifanyia kazi muqtadhwa yake, lakini waarabu walikuwa wanafahamu ukweli na maana ya laa ilaaha illa Allaah. Na kwa ajili ya hili ndio maana walikataa kuitamka. Allaah Anasema kuhusu wao:

إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ
“Hakika wao walipokuwa wakiambiwa: “Laa ilaaha illa Allaah” (Hapana ilaaha ila Allaah, walikuwa) hutakabari. Na (pia walikuwa) wanasema: “Je, tuache miungu yetu kwa ajili ya mshairi majnuni?!” (37:35-36)

Huu ni uongo. Alikuwa mshairi mwendawazimu? Yaani watafuta hoja tu baada ya kukataa kusema laa ilaaha illa Allaah na kuleta muqtadhwa yake; kumtakasia Allaah ´Ibaadah kwa kuacha kila kinachoabudiwa badala ya Allaah na kumfanya ´Ibaadah zote Allaah asiyekuwa na mshirika katika hilo.

– Aina ya tatu ni yale Aliyoyataja Allaah katika Kitabu Chake, kwa kutaja Sifa Zake na Majina Yake. Allaah Kajiita na Kujisifu Mwenyewe kwa Majina na Sifa, na Majina na Sifa zote hizi zinatolewa dalili na Qur-aan na Sunnah. Tunayaamini. Tunamsifu Allaah kuwa Yuko na Elimu, Rahmah, Anaghadhibika, Anaridhia, Anakasirika, Yuko juu, Huteremka; tunamsifu Allaah kwa yote haya. Tunamsifu kwa Kustawaa Kwake juu ya ´Arshi Yake, kuwa Kwake juu ya viumbe Vyake, Elimu yake Kamili, tunamwita kwa Majina Yake; Haliym, Qadiyr, Ghafuur, Rahiym, Rahmaan, Rahiym. Majina na Sifa zote za Allaah tunazikubali na kuziamini. Na tunamwachia Kauli Yake:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye As-Samiy’ul-Baswiyr (Mwenye kusikia yote daima, Mwenye kuona yote daima).” (42:11)

Tunamthibitishia Allaah Usikivu na Kuona, lakini Kusikia Kwake si kama kusikia kwa viumbe, wala Kuona Kwake si kama kuona kwa viumbe, bali [Sifa Zake] zinalingana na Utukufu na Ukubwa Wake:

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
“Basi msipigie mifano Allaah (kwani hakuna kinachofanana Naye kabisa!) Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.” (16:74)

Sifa ambazo zinabadilishwa kuzisifu kwa uhakika wake, au zimekanushwa na kupingwa, zote hizo zimethibiti kwa njia ya upokezi na Ah-us-Sunnah wanazithibitisha kwa Utukufu na Ukubwa unaolingana na Allaah. Hawakuziharibu wala kuzifananisha na wala kuzipigia mifano, bali wamezithibitisha kutokana na kutolewa kwake dalili ya Kitabu na Sunnah. Aina hizi za Tawhiyd zipo ndani ya Qur-aan. Na watu wanaosema ya kwamba ni Ibn Taymiyyah na Ibn ´Abdul-Wahhaab (Rahimahumu Allaah) wao ndio walileta vigawanyo hivi, haya yote ni makosa. Soma Qur-aan ujione mwenyewe ukweli wa mambo.


  • Author: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh
  • http://youtu.be/6l93hM2Tth4
  • Kitengo: Uncategorized , Tawhiyd na ´Aqiydah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 19th, October 2013