Allaah Ndio Mwenye Kukadiria Kheri Na Shari

Leo inapitika katika ndimi za ´Awwaam maneno ya khatari sana katika mlango huu – yaani Qadar. Utaona mtu ambaye si msomi anasema: “Allaah Hakadirii isipokuwa kheri tupu”. Maana ya maneno haya ni kwamba Allaah Hakadirii shari. Shari inakadiriwa pia kama jinsi kheri inakadiriwa vilevile. Wao wanasema hivi kwa kurithi maneno haya. Ni maneno ambayo yanatakiwa kukataliwa. Inatakikana kwa wanafunzi kuwabainishia watu khatari yake. Kauli yao “Allaah Hakadirii isipokuwa kheri tupu” maneno haya ni batili. Yanasemwa na ´Awwaam katika watu na mfano wao. Allaah (Ta´ala) Ametueleza kwamba ni Yeye ndiye Amekadiria kheri na shari na kwamba Yeye ni ´Aziyz Al-Hakiym, na kwamba juu ya kila kitu ni Mjuzi. Haulizwi juu ya anachokifanya na wao (viumbe) ndio wataulizwa. Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy Chanzo: Usuul-us-Sunnah Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=1005&size=2h&ext=.rm

Leo inapitika katika ndimi za ´Awwaam maneno ya khatari sana katika mlango huu – yaani Qadar. Utaona mtu ambaye si msomi anasema: “Allaah Hakadirii isipokuwa kheri tupu”. Maana ya maneno haya ni kwamba Allaah Hakadirii shari. Shari inakadiriwa pia kama jinsi kheri inakadiriwa vilevile. Wao wanasema hivi kwa kurithi maneno haya. Ni maneno ambayo yanatakiwa kukataliwa. Inatakikana kwa wanafunzi kuwabainishia watu khatari yake. Kauli yao “Allaah Hakadirii isipokuwa kheri tupu” maneno haya ni batili. Yanasemwa na ´Awwaam katika watu na mfano wao.

Allaah (Ta´ala) Ametueleza kwamba ni Yeye ndiye Amekadiria kheri na shari na kwamba Yeye ni ´Aziyz Al-Hakiym, na kwamba juu ya kila kitu ni Mjuzi. Haulizwi juu ya anachokifanya na wao (viumbe) ndio wataulizwa.

Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy
Chanzo: Usuul-us-Sunnah
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=1005&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Qadar
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 28th, March 2014