Allaah Kuwa Na Viumbe Vyake Haina Maana Anachanganyika Nao Kimwili

Hanbal bin Ishaaq kasema katika kitabu "as-Sunnah": "Nilimwambia Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal: "Nini manaa ya Maneno ya Allaah: وهو معكم أين ما كنتم "Naye yupamoja nanyi popote mlipo.” ألم تر أن الله يعلم ما في السماوات وما في الأرض ما يكون من نجوى ثلاثة إلا هو رابعهم ولا خمسة إلا هو سادسهم ولا أدنى من ذلك ولا أكثر إلا هو معهم أين ما كانوا ثم ينبئهم بما عملوا يوم القيامة إن الله بكل شيء عليم "Kwani huoni kwamba Allaah Anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu isipokua Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano isipokuwa Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, isipokuwa Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Qiyaamah Atawaambia waliyoyatenda. Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila kitu.” Akajibu: "Ni elimu yake. Anajua yaliyofichikana na ya dhahiri. Anajua na kushuhudia yote. Anajua yale yaliyofichikana. Mola Wetu Yuko juu ya ´Arshi bila ya mpaka wala namna gani. Kursiy Yake imeizunguka mbingu na ardhi." Imaam Ahmad akafafanua maana ya “Ma'iyyah” [kuwa Kwake pamoja na viumbe Vyake], kwa ufafanuzi katika " ar-Radd 'alaa al-Jahmiyyah". Ma´iyyah imetajwa katika Qur-aan kwa njia ya jumla, kama ilivyo katika Aayah hizi mbili, na kwa njia maalum, kama ilivyo katika Aayah ifuatayo: إن الله مع الذين اتقوا والذين هم محسنون "Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni Muhsinuwn (wema).” قال لا تخافا إنني معكما أسمع وأرى “(Allaah) Akasema: “Msikhofu; hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.” لا تحزن إن الله معنا "Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.” Ingekuwa maana yake kwamba Yeye yuko pamoja na kila kitu kwa Dhati Yake, sura hii ya jumla ingegongana na ile ya maalum. Ni jambo linalojulikana ya kwamba Kauli ya Allaah: لا تحزن إن الله معنا "Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.” ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Abu Bakr kinyume na maadui zao makafiri. Hali kadhalika Kauli Yake: إن الله مع الذين اتقوا والذين هم محسنون "Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni Muhsinuwn (wema).” ni maalum kwa wale watendao mema na mazuri kinyume na madhalimu na wafanyao madhambi. Neno Ma'iyyah si katika kiarabu wala Qur-aan halina maana ya kuchanganyika kimwili kati ya dhati mbili. Mfano wa hilo ni Kauli ya Allaah: محمد رسول الله والذين معه "Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na waliopamoja naye... " فأولئك مع المؤمنين "Basi hao watakuwa pamoja na Waumini... “ اتقوا الله وكونوا مع الصادقين " Mcheni Allaah na kuweni pamoja na As-Swaadiqiyn (wakweli)!" Na kuna dalili nyingi mfano wa hizi. Ndio maana ni jambo lisilowezekana Kauli ya Allaah: وهو معكم أين ما كنتم "Naye yu pamoja nanyi popote mlipo.” ikawa na maana ya kwamba Dhati Yake imechanganyika na dhati ya viumbe. Isitoshe, Kaanza Aayah kwa kuongelea kuhusu elimu na kaimalizia kwa kuongelea kuhusu elimu. Hivyo basi, muktadha unathibitisha ya kwamba Anamaanisha ya kuwa ana elimu ya viumbe Vyake. Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah Chanzo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 127

Hanbal bin Ishaaq kasema katika kitabu “as-Sunnah”:

“Nilimwambia Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal: “Nini manaa ya Maneno ya Allaah:

وهو معكم أين ما كنتم
“Naye yupamoja nanyi popote mlipo.”

ألم تر أن الله يعلم ما في السماوات وما في الأرض ما يكون من نجوى ثلاثة إلا هو رابعهم ولا خمسة إلا هو سادسهم ولا أدنى من ذلك ولا أكثر إلا هو معهم أين ما كانوا ثم ينبئهم بما عملوا يوم القيامة إن الله بكل شيء عليم
“Kwani huoni kwamba Allaah Anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong’ono wa watu watatu isipokua Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano isipokuwa Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, isipokuwa Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Qiyaamah Atawaambia waliyoyatenda. Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila kitu.”

Akajibu:

“Ni elimu yake. Anajua yaliyofichikana na ya dhahiri. Anajua na kushuhudia yote. Anajua yale yaliyofichikana. Mola Wetu Yuko juu ya ´Arshi bila ya mpaka wala namna gani. Kursiy Yake imeizunguka mbingu na ardhi.”

Imaam Ahmad akafafanua maana ya “Ma’iyyah” [kuwa Kwake pamoja na viumbe Vyake], kwa ufafanuzi katika ” ar-Radd ‘alaa al-Jahmiyyah”. Ma´iyyah imetajwa katika Qur-aan kwa njia ya jumla, kama ilivyo katika Aayah hizi mbili, na kwa njia maalum, kama ilivyo katika Aayah ifuatayo:

إن الله مع الذين اتقوا والذين هم محسنون
“Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni Muhsinuwn (wema).”

قال لا تخافا إنني معكما أسمع وأرى
“(Allaah) Akasema: “Msikhofu; hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.”

لا تحزن إن الله معنا
“Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.”

Ingekuwa maana yake kwamba Yeye yuko pamoja na kila kitu kwa Dhati Yake, sura hii ya jumla ingegongana na ile ya maalum. Ni jambo linalojulikana ya kwamba Kauli ya Allaah:

لا تحزن إن الله معنا
“Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.”

ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na Abu Bakr kinyume na maadui zao makafiri. Hali kadhalika Kauli Yake:

إن الله مع الذين اتقوا والذين هم محسنون
“Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni Muhsinuwn (wema).”

ni maalum kwa wale watendao mema na mazuri kinyume na madhalimu na wafanyao madhambi.
Neno Ma’iyyah si katika kiarabu wala Qur-aan halina maana ya kuchanganyika kimwili kati ya dhati mbili. Mfano wa hilo ni Kauli ya Allaah:

محمد رسول الله والذين معه
“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na waliopamoja naye… ”

فأولئك مع المؤمنين
“Basi hao watakuwa pamoja na Waumini… “

اتقوا الله وكونوا مع الصادقين
” Mcheni Allaah na kuweni pamoja na As-Swaadiqiyn (wakweli)!”

Na kuna dalili nyingi mfano wa hizi. Ndio maana ni jambo lisilowezekana Kauli ya Allaah:

وهو معكم أين ما كنتم
“Naye yu pamoja nanyi popote mlipo.”

ikawa na maana ya kwamba Dhati Yake imechanganyika na dhati ya viumbe. Isitoshe, Kaanza Aayah kwa kuongelea kuhusu elimu na kaimalizia kwa kuongelea kuhusu elimu. Hivyo basi, muktadha unathibitisha ya kwamba Anamaanisha ya kuwa ana elimu ya viumbe Vyake.

Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Chanzo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 127


  • Kitengo: Uncategorized , Allaah kuwa pamoja na viumbe Vyake
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013