Allaah Kamuumba Aadam Kwa Mkono Wake

271 - Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Allaah ('Azza wa Jalla) Kamuumba Aadam ('alayhis-Salaam) kwa Mkono Wake siku ya Ijumaa. Akampulizia roho kutoka Kwake na Akaamrisha Malaika wamsujudie." 272 – Inatakiwa kuwaambia Jahmiyyah ambao wanapinga kwamba Allaah ('Azza wa Jalla) kamuumba Aadam kwa Mkono Wake: "Nyinyi hamuamini Qur-aan. Mmeikanusha Sunnah na mmekwenda kinyume na Ijmaa´. " 273 – Ambayo Qur-aan imethibitisha, Kaamrisha Allaah ('Azza wa Jalla) Malaika kumsujudia Aadam. Wote wakafanya isipokuwa tu Ibliys. Allaah ('Azza wa Jalla) Kasema kuhusu Ibliys: قال يا إبليس ما منعك أن تسجد لما خلقت بيدي أستكبرت أم كنت من العالين “(Allaah) Akasema: “Ee Ibliys! Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa Mikono Yangu? Je, umetakabari, au umekuwa miongoni mwa waliojitukuza?” 274 – Ibliys akaingiwa na wivu kwa kuwa (Allaah) Alimuumba Aadam kwa Mikono Yake tofauti na yeye. 275 - Wakati Muusa alikutana na Aadam na wakaanza kujadili, akasema Muusa kumwambia Aadam: "Wewe ndiye Aadam, baba yetu. Allaah Kakuumba kwa Mkono Wake, Akakupulizia roho kutoka Kwake na Akaamrisha Malaika kukusujudia." Hapa anaongelea Muusa kupitia hatua ambazo Allaah Alikuwa nazo hususan na Aadam, tofauti na wengine. Yule anayekanusha hili, ni kafiri. Kisha akamjibu Aadam na kusema: "Je, ni wewe Muusa, ambaye Allaah Kakuchagua kwa ujumbe Wake na kwa Maneno Yake (kwa kuongea nawe), Kakuandikia Tawraat kwa Mkono Wake na ambaye umesoma Tawraat?" 276 - Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Aadam na Muusa walijadiliana. Muusa akamwambia: "Aadam, Allaah Kakuumba kwa Mkono Wake, Akakupulizia roho kutoka Kwake, Akaamrisha Malaika wakusujudie na akakuacha ueshi Peponi." 277 – Hoja ya Muusa kwa Aadam ilikuwa ni kwamba Allaah Kamuumba kwa Mkono Wake. Kwa upande mwingine, hoja ya Aadam kwa Muusa kwamba Allaah Kaandika Tawraat kwa Mkono Wake. 278 - Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhumaa) Kasema: "Allaah ('Azza wa Jalla) Kamteua Ibraahiym kwa urafiki wa karibu (Khullah), Muusa kwa kuongea naye na Muhammad kwa muono – Swalah na salaam ziwe juu yao." Mwandishi: Abu Bakr al-Ajurriy Chanzo: ash-Shari´ah, uk. 331-334 Daar al-Kitaab al-´Arabiy

271 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:
“Allaah (‘Azza wa Jalla) Kamuumba Aadam (‘alayhis-Salaam) kwa Mkono Wake siku ya Ijumaa. Akampulizia roho kutoka Kwake na Akaamrisha Malaika wamsujudie.”

272 – Inatakiwa kuwaambia Jahmiyyah ambao wanapinga kwamba Allaah (‘Azza wa Jalla) kamuumba Aadam kwa Mkono Wake:
“Nyinyi hamuamini Qur-aan. Mmeikanusha Sunnah na mmekwenda kinyume na Ijmaa´. ”

273 – Ambayo Qur-aan imethibitisha, Kaamrisha Allaah (‘Azza wa Jalla) Malaika kumsujudia Aadam. Wote wakafanya isipokuwa tu Ibliys. Allaah (‘Azza wa Jalla) Kasema kuhusu Ibliys:
قال يا إبليس ما منعك أن تسجد لما خلقت بيدي أستكبرت أم كنت من العالين
“(Allaah) Akasema: “Ee Ibliys! Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa Mikono Yangu? Je, umetakabari, au umekuwa miongoni mwa waliojitukuza?”

274 – Ibliys akaingiwa na wivu kwa kuwa (Allaah) Alimuumba Aadam kwa Mikono Yake tofauti na yeye.

275 – Wakati Muusa alikutana na Aadam na wakaanza kujadili, akasema Muusa kumwambia Aadam:
“Wewe ndiye Aadam, baba yetu. Allaah Kakuumba kwa Mkono Wake, Akakupulizia roho kutoka Kwake na Akaamrisha Malaika kukusujudia.”

Hapa anaongelea Muusa kupitia hatua ambazo Allaah Alikuwa nazo hususan na Aadam, tofauti na wengine. Yule anayekanusha hili, ni kafiri. Kisha akamjibu Aadam na kusema:
“Je, ni wewe Muusa, ambaye Allaah Kakuchagua kwa ujumbe Wake na kwa Maneno Yake (kwa kuongea nawe), Kakuandikia Tawraat kwa Mkono Wake na ambaye umesoma Tawraat?”

276 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:
“Aadam na Muusa walijadiliana. Muusa akamwambia: “Aadam, Allaah Kakuumba kwa Mkono Wake, Akakupulizia roho kutoka Kwake, Akaamrisha Malaika wakusujudie na akakuacha ueshi Peponi.”

277 – Hoja ya Muusa kwa Aadam ilikuwa ni kwamba Allaah Kamuumba kwa Mkono Wake. Kwa upande mwingine, hoja ya Aadam kwa Muusa kwamba Allaah Kaandika Tawraat kwa Mkono Wake.

278 – Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) Kasema:
“Allaah (‘Azza wa Jalla) Kamteua Ibraahiym kwa urafiki wa karibu (Khullah), Muusa kwa kuongea naye na Muhammad kwa muono – Swalah na salaam ziwe juu yao.”

Mwandishi: Abu Bakr al-Ajurriy
Chanzo: ash-Shari´ah, uk. 331-334
Daar al-Kitaab al-´Arabiy


  • Kitengo: Uncategorized , Mikono ya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013