Allaah Hushuka Kila Usiku Kwa Ajili Yako – Vipi Walala?

12- Katika tabaka ya dunia inasimbulia kwa fadhla Zake inafarajika milango ya mbinguni na inafunguliwa milango 13- Anasema “Alaa”, kuna anayeomba maghfirah nimsamehe na anayeomba kheri na ruzuku apewe -------------------- MAELEZO Kauli ya mwandishi “inasimbulia kwa fadhla Zake”, Anasema (Subhaanahu wa Ta´ala): “Je, kuna mwenye kuniomba nimpe?” Hii ni neema na fadhila kutoka kwa Allaah. Anasema: “Je, kuna anayeniomba maghfirah nimsamehe? Je, kuna anayeniomba msamaha nimsamehe?” Hizi zote ni kutokana na fadhila Zake (Subhanaahu wa Ta´ala). Anawaonesha waja Waje karama na ukarimu Wake. Kwa ajili hii, imependekezwa kwa Muislamu kuamka mwisho wa usiku pale ambapo kumebaki theluthi ya mwisho ya usiku, awe macho akiswali na huku akiomuomba Allaah na Amtake maghfirah. Hakika ni wakati wa kukubaliwa kwa Du´aa. Asilale katika wakati kama huu na akaikoseshea nafsi yake kama wanavofanya wengi katika waliokoseshwa ambao wanakesha usiku, inapofika mwisho wa usiku ndio wanaenda kulala mpaka wanapitwa na Swalah ya faradhi ambayo ni al-Fajr. Huku ni kunyimwa na tunaomba kinga kwa Allaah. Inatakikana kwa Muislamu alale mapema na ajizoweze mwenyewe ili aweze kuwa anasimama mwishoni mwa usiku. Akiizoweza nafsi yake hili atazowea. Ama akiendekeza uvivu na kulala, itamkuwia vigumu hata kuamka katika Swalah ya al-Fajr. Inatakikana kwa Musilamu asipitwe na fursa hii na wito wa Allaah umkute yuko macho. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema katika sifa za waja Wake wamchao: كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ “Walikuwa wakilala kidogo katika usiku (wakifanya ‘ibaadah). Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah.” (adh-Dhaariyaat:17-18) Akasema tena: وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ “... na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.” (al-´Imraan:17) Kufanya istighfaar wakati wa alfajiri kuna umaalum wake tofauti na nyakati zingine. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 102-103

12- Katika tabaka ya dunia inasimbulia kwa fadhla Zake

inafarajika milango ya mbinguni na inafunguliwa milango

13- Anasema “Alaa”, kuna anayeomba maghfirah nimsamehe

na anayeomba kheri na ruzuku apewe

——————–

MAELEZO

Kauli ya mwandishi “inasimbulia kwa fadhla Zake”, Anasema (Subhaanahu wa Ta´ala):

“Je, kuna mwenye kuniomba nimpe?”

Hii ni neema na fadhila kutoka kwa Allaah. Anasema:

“Je, kuna anayeniomba maghfirah nimsamehe? Je, kuna anayeniomba msamaha nimsamehe?”

Hizi zote ni kutokana na fadhila Zake (Subhanaahu wa Ta´ala). Anawaonesha waja Waje karama na ukarimu Wake.

Kwa ajili hii, imependekezwa kwa Muislamu kuamka mwisho wa usiku pale ambapo kumebaki theluthi ya mwisho ya usiku, awe macho akiswali na huku akiomuomba Allaah na Amtake maghfirah. Hakika ni wakati wa kukubaliwa kwa Du´aa. Asilale katika wakati kama huu na akaikoseshea nafsi yake kama wanavofanya wengi katika waliokoseshwa ambao wanakesha usiku, inapofika mwisho wa usiku ndio wanaenda kulala mpaka wanapitwa na Swalah ya faradhi ambayo ni al-Fajr. Huku ni kunyimwa na tunaomba kinga kwa Allaah. Inatakikana kwa Muislamu alale mapema na ajizoweze mwenyewe ili aweze kuwa anasimama mwishoni mwa usiku. Akiizoweza nafsi yake hili atazowea. Ama akiendekeza uvivu na kulala, itamkuwia vigumu hata kuamka katika Swalah ya al-Fajr. Inatakikana kwa Musilamu asipitwe na fursa hii na wito wa Allaah umkute yuko macho. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema katika sifa za waja Wake wamchao:

كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
“Walikuwa wakilala kidogo katika usiku (wakifanya ‘ibaadah). Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah.” (adh-Dhaariyaat:17-18)

Akasema tena:

وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ
“… na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.” (al-´Imraan:17)

Kufanya istighfaar wakati wa alfajiri kuna umaalum wake tofauti na nyakati zingine.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 102-103


  • Kitengo: Uncategorized , Kushuka (kuteremka) kwa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 16th, February 2014