Allaah Huongea Kwa Sauti Ya Kusikika

Kuhusiana na Sauti ya Allaah, imepokelewa na 'Abdullaah bin Unays kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ya kwamba amesema: "Ataita kwa Sauti inayosikika na wote walio karibu na mbali: “Mimi ndiye Maalik (Mfalme)! Mimi ndiye Maalik!”” Imepokewa na Ahmad na maimamu wengine. al-Bukhaariy kataja hii kama dalili yenye nguvu. Ibn Mas'uud kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Wakati Allaah Anatamka kwa Wahyi, wakaazi wa mbinguni wanasikia Sauti Yake kama mnyororo dhidi ya jiwe na wanasujudu." Kusema kwamba herufu na sauti hutoka kwa nje ya njia tu ni batili na haliwezekani. Allaah (Ta´ala) Kasema: يوم نقول لجهنم هل امتلأت وتقول هل من مزيد ”Siku tutapoiambia Jahannamu: ”Je! Umejaa?” Nayo itasema: “Je! Kuna ziada?”” Kaeleza kwamba mbingu na dunia vimesema: أتينا طائعين “Njooni mkiwa mmetii (kwa khiari) au kukirihika.” Maneno haya hayatoki si nje ya njia wala si kwenye eneo. Vile vile, imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwamba ule mguu wa sumu ulizungumza naye na kwamba jiwe na mti vilimtolea Salaam . Mwandishi: Imaam Swiddiyq Hasan Khaan Chanzo: Qatf-uth-Thamar, uk. 84-85

Kuhusiana na Sauti ya Allaah, imepokelewa na ‘Abdullaah bin Unays kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Ataita kwa Sauti inayosikika na wote walio karibu na mbali: “Mimi ndiye Maalik (Mfalme)! Mimi ndiye Maalik!”” Imepokewa na Ahmad na maimamu wengine. al-Bukhaariy kataja hii kama dalili yenye nguvu.

Ibn Mas’uud kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:
“Wakati Allaah Anatamka kwa Wahyi, wakaazi wa mbinguni wanasikia Sauti Yake kama mnyororo dhidi ya jiwe na wanasujudu.”

Kusema kwamba herufu na sauti hutoka kwa nje ya njia tu ni batili na haliwezekani. Allaah (Ta´ala) Kasema:
يوم نقول لجهنم هل امتلأت وتقول هل من مزيد
”Siku tutapoiambia Jahannamu: ”Je! Umejaa?” Nayo itasema: “Je! Kuna ziada?””

Kaeleza kwamba mbingu na dunia vimesema:

أتينا طائعين
“Njooni mkiwa mmetii (kwa khiari) au kukirihika.”

Maneno haya hayatoki si nje ya njia wala si kwenye eneo. Vile vile, imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwamba ule mguu wa sumu ulizungumza naye na kwamba jiwe na mti vilimtolea Salaam .

Mwandishi: Imaam Swiddiyq Hasan Khaan
Chanzo: Qatf-uth-Thamar, uk. 84-85


  • Kitengo: Uncategorized , Sauti ya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013