Allaah Hafikiriwi – Viumbe Wake Ndio Wenye Kufikiriwa

Kwa hivyo haijuzu kufikiria Dhati ya Allaah. Ufikiriaji unakuwa katika viumbe vya Allaah ambavyo vinatolea dalili juu ya ukamilifu wa Uwezo Wake. Mtu akifikiria Dhati ya Allaah na namna ya Sifa na namna ya Majina Yake hakuna njia ya kufahamu hilo na haiwezekani kwa mtu akazunguka [kwa ujuzi] chochote katika hayo. Hivyo haijuzu kufikiria namna ya Dhati ya Allaah na namna ya Sifa Zake (Subhaanahu). Ufikiriaji unakuwa kwa viumbe Vyake ambavyo vinatolea dalili juu ya Uwezo Wake. Juu ya uumbaji wa mbingu, ardhi, mwanaadamu na viumbe mbali mbali, ni dalili ya ukamilifu wa Muumbaji Aliyeviumba na uwepo Wake na kwamba juu ya kila kitu ni Muweza na Anaviendesha vile Atakavyo. Mwandishi: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn Ibn Qudaamah al-Maqdisiy Chanzo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=878&size=2h&ext=.rm

Kwa hivyo haijuzu kufikiria Dhati ya Allaah. Ufikiriaji unakuwa katika viumbe vya Allaah ambavyo vinatolea dalili juu ya ukamilifu wa Uwezo Wake. Mtu akifikiria Dhati ya Allaah na namna ya Sifa na namna ya Majina Yake hakuna njia ya kufahamu hilo na haiwezekani kwa mtu akazunguka [kwa ujuzi] chochote katika hayo. Hivyo haijuzu kufikiria namna ya Dhati ya Allaah na namna ya Sifa Zake (Subhaanahu). Ufikiriaji unakuwa kwa viumbe Vyake ambavyo vinatolea dalili juu ya Uwezo Wake. Juu ya uumbaji wa mbingu, ardhi, mwanaadamu na viumbe mbali mbali, ni dalili ya ukamilifu wa Muumbaji Aliyeviumba na uwepo Wake na kwamba juu ya kila kitu ni Muweza na Anaviendesha vile Atakavyo.

Mwandishi: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn Ibn Qudaamah al-Maqdisiy
Chanzo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=878&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Tawhiyd
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 31st, March 2014