Allaah Ana Mikono Miwili Na Yote Ni Ya Kulia

268 - Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhumaa) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Kitu cha kwanza Allaah ('Azza wa Jalla) Kuumba, ni kalamu. Aliichukua kwa Mkono Wake wa kulia - na Mikono Yake yote miwili ni ya kulia – Akaandika kuwepo kwa dunia, ´amali za wenye kutenda, ya uchaji Allaah na ya uasi." 269 - 'Abdullah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Siku ya Qiyaamah, wale ambao ni waadilifu watakuwa upande wa Mkono wa kulia wa Allaah ('Azza wa Jalla) - na Mikono Yake yote ni miwili - juu ya mimbari ya nuru." 270 - 'Abdullaah bin Salaam (Radhiya Allaah 'anhu) kasema katika Hadiyth yake ndefu: "Kisha akasema: "Aadam, chagua!" Akasema: "Mola, nachagua Mkono Wako wa kulia na Mikono Yako yote ni ya kulia.” Akaunyoosha na huko akaona watoto wake katika watu wa Peponi. Akasema: "Mola, ni kina nani hawa?" Akasema: “Ni watoto wako hadi Siku ya Qiyaamah ambao Nimeamua Kuumba kwa watu wa Peponi.”” Mwandishi: Imaam Abu Bakr al-Ajurriy Chanzo: ash-Shari´ah, uk. 329-330 Daar al-Kitaab al-´Arabiy

268 – Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Kitu cha kwanza Allaah (‘Azza wa Jalla) Kuumba, ni kalamu. Aliichukua kwa Mkono Wake wa kulia – na Mikono Yake yote miwili ni ya kulia – Akaandika kuwepo kwa dunia, ´amali za wenye kutenda, ya uchaji Allaah na ya uasi.”

269 – ‘Abdullah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Siku ya Qiyaamah, wale ambao ni waadilifu watakuwa upande wa Mkono wa kulia wa Allaah (‘Azza wa Jalla) – na Mikono Yake yote ni miwili – juu ya mimbari ya nuru.”

270 – ‘Abdullaah bin Salaam (Radhiya Allaah ‘anhu) kasema katika Hadiyth yake ndefu:

“Kisha akasema: “Aadam, chagua!” Akasema: “Mola, nachagua Mkono Wako wa kulia na Mikono Yako yote ni ya kulia.” Akaunyoosha na huko akaona watoto wake katika watu wa Peponi. Akasema: “Mola, ni kina nani hawa?” Akasema: “Ni watoto wako hadi Siku ya Qiyaamah ambao Nimeamua Kuumba kwa watu wa Peponi.””

Mwandishi: Imaam Abu Bakr al-Ajurriy
Chanzo: ash-Shari´ah, uk. 329-330
Daar al-Kitaab al-´Arabiy


  • Kitengo: Uncategorized , Mikono ya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013