al-Qaradhwaawiy Kuhusu Demokrasia Na Uhuru

Yuusuf al-Qaradhwaawiy anasema: ”Tunatakiwa kushikamana na Demokrasia na tutapigana kwa ajili yayo (hiyo Demokrasia). Sisi tunataka nchi ya Demokrasia ambayo ni Uhuru. Kasema pia: ”Kwa hakika, hakuna dawa kwa Ummah huu isipokuwa mpaka kwa Uhuru (Demokrasia). Kama nilivyotangulia kusema katika baadhi ya barnamiji zangu, mimi ninaipa kipaumbele Uhuru (Demokrasia) juu ya kutekeleza Shari´ah ya Kiislamu. Haiwezekani kutekeleza Shari´ah ya Kiislamu na Uhuru (Demokrasia) inakosekana. Swali La Kwanza: Ipi hukumu kwa anayesema kuweka Demokrasia ni katika dharurah na mambo ya muhimu katika zama hizi, la sivyo tutafikwa na yaliyoifika Iraq? ´Allaamah al-Fawzaan: Demokrasia ni madhehebu ya makafiri. Na waislamu Allaah Hakuwapa haja ya kitu kama hichi. Wao wako na uadilifu, uadilifu wa Kiungu. Wana uadilifu wa Kiungu. Hawana haja ya "Demokrasia" kama wasemavyo. Wanadanganya, hakuna Demokrasia. Hawana ila chuma na moto (unyama). Wahana Demokrasia. Huu ni uongo mtupu. Katika Uislamu kuna kitu kinachoitwa uadilifu - wa liLlaahil Hamd. Ama wanayodai na kujivunia, si sahihi. Hawana chochote ila chuma na moto, na kushambulia manyumba na kushambulia wale wasioafikiana na matakwa yao. Tunawaambia wale wanaosema kuna "Demokrasia", iko wapi Demokrasia Afghanistan? Iko wapi Demokrasia Palestina? Iko wapi Demokrasia mnayosema? Iko wapi Demokrasia Chechenia? Iko wapi? Iko wapi Demokrasia? Mnashambulia miji yote na watu wake. Mnaua watoto, wanawake, wazee na watu wote wanapokhalifu amri zenu. Iko wapi Demokrasia? Swali La Pili: Tunasikia siku hizi ya kwamba Uislamu unaruhusu Uhuru wa kuamini. Na wanatumia Kauli ya Allaah: “Hapana kulazimisha katika Dini.” (al-Baqarah 02 : 256) Je, hili ni sahihi? ´Allaamah al-Fawzaan: Huku ni kumsemea Allaah (Ta´ala) uongo. Uislamu haukuja na Uhuru wa kuamini. Uislamu umekuja kukataza Shirki na Kufuru. Na kupigana vita na washirikina. Na lau Uislamu ungelikuwa umekuja na Uhuru wa kuamini, watu wa wasingelikuwa na haja ya kutumiwa Mitume, kutumwa Vitabu. Na watu wasingelikuwa na haja ya kufanya Hajj na kupigana katika njia ya Allaah. Kila mmoja angelifuata matamanio yake. Kila mmoja angelikuwa Huru. Hapana! Allaah Anasema: ”Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” (adh-Dhaariyat 51 : 56) Hakusema: ”... ili kila mmoja afuate matamanio yake.” Kasema: ”... ila waniabudu Mimi.” (adh-Dhaariyat 51 : 56) Kasema Allaah (Ta´ala): ”Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah na Dini iwe ya Allaah pekee.” (al-Baqarah 02 : 193) Yule anayekataa kumuabudu Allaah, apigwe vita. Asiachwe! Mpaka arudi katika Dini au auawe. Uislamu haukuja na uhuru wa Dini za Kufuru na Mulhidah. Huku ni kumsemea Allaah (Ta´ala) uongo. Vinginevyo, kwa nini Allaah Katuma Mitume na Akateremsha Vitabu na Akaweka katika Shari´ah Jihaad na Akawajibisha huduud na adhabu. Yote haya ni kwa ajili ya kulinda watu na Itikadi batili na maoni potevu. Ili kuwalinda kwa kuwa ni waja wa Allaah. Ni wajibu wamuabudu Allaah Mmoja asiyekuwa na mshirika. Au (wakikataa) ichukuliwe kutoka kwao Ujira uliyowekwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama Kauli Yake Allaah (Ta´ala): “Hapana kulazimisha katika Dini.” (al-Baqarah 02 : 256) Maana yake si kwamba mtu kuwa na Uhuru wa rai. Maana yake ni kwamba sisi hatuwezi kumlazimisha mtu Dini kuingia kwenye moyo wake. Hili hakuna anaeliweza isipokuwa Allaah. ”Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye.” (al-Qaswas 28 : 56) Uongofu wa nyoyo uko kwenye Mikono ya Allaah, na haupitiki kwa kulazimisha, unapitika kwa khiyari. Lakini sisi tunapigana vita na makafiri na washirikina. Allaah Katuamrisha hilo. Tunaamrisha mema na kukataza maovu. Tunawabainishia watu (Dini ya Kiislamu). Na hatuwaambia: ”Hapana kulazimisha katika Dini.” (al-Baqarah 02 : 256) Hatuwalazimishi watu kuingia katika Dini, lakini ni wajibu kwetu kuwabainishia Dini na kumuadhibu anayeiacha Dini hii. Ama mtu huyo kuongoka ndani ya moyo wake, hakuna awezae hili ila Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ndio maana ya: ”Hapana kulazimisha katika Dini.” (02:256) Ni kama mfano wa Kauli Yake: Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye.” (al-Qaswas 28 : 56) Na Yule Aliyesema: ”Hapana kulazimisha katika Dini.” (al-Baqarah 02 : 256) Ndie huyo huyo Aliyesema: ”Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah na Dini iwe ya Allaah pekee.” (02:193) Kwa nini unachukua Aayah moja unaacha nyingine?!

Yuusuf al-Qaradhwaawiy anasema:
”Tunatakiwa kushikamana na Demokrasia na tutapigana kwa ajili yayo (hiyo Demokrasia). Sisi tunataka nchi ya Demokrasia ambayo ni Uhuru.

Kasema pia:
”Kwa hakika, hakuna dawa kwa Ummah huu isipokuwa mpaka kwa Uhuru (Demokrasia). Kama nilivyotangulia kusema katika baadhi ya barnamiji zangu, mimi ninaipa kipaumbele Uhuru (Demokrasia) juu ya kutekeleza Shari´ah ya Kiislamu. Haiwezekani kutekeleza Shari´ah ya Kiislamu na Uhuru (Demokrasia) inakosekana.

Swali La Kwanza:
Ipi hukumu kwa anayesema kuweka Demokrasia ni katika dharurah na mambo ya muhimu katika zama hizi, la sivyo tutafikwa na yaliyoifika Iraq?

´Allaamah al-Fawzaan:
Demokrasia ni madhehebu ya makafiri. Na waislamu Allaah Hakuwapa haja ya kitu kama hichi. Wao wako na uadilifu, uadilifu wa Kiungu. Wana uadilifu wa Kiungu. Hawana haja ya “Demokrasia” kama wasemavyo. Wanadanganya, hakuna Demokrasia. Hawana ila chuma na moto (unyama). Wahana Demokrasia. Huu ni uongo mtupu. Katika Uislamu kuna kitu kinachoitwa uadilifu – wa liLlaahil Hamd.

Ama wanayodai na kujivunia, si sahihi. Hawana chochote ila chuma na moto, na kushambulia manyumba na kushambulia wale wasioafikiana na matakwa yao. Tunawaambia wale wanaosema kuna “Demokrasia”, iko wapi Demokrasia Afghanistan? Iko wapi Demokrasia Palestina? Iko wapi Demokrasia mnayosema? Iko wapi Demokrasia Chechenia? Iko wapi? Iko wapi Demokrasia? Mnashambulia miji yote na watu wake. Mnaua watoto, wanawake, wazee na watu wote wanapokhalifu amri zenu. Iko wapi Demokrasia?

Swali La Pili:
Tunasikia siku hizi ya kwamba Uislamu unaruhusu Uhuru wa kuamini. Na wanatumia Kauli ya Allaah:

“Hapana kulazimisha katika Dini.” (al-Baqarah 02 : 256)

Je, hili ni sahihi?

´Allaamah al-Fawzaan:
Huku ni kumsemea Allaah (Ta´ala) uongo. Uislamu haukuja na Uhuru wa kuamini. Uislamu umekuja kukataza Shirki na Kufuru. Na kupigana vita na washirikina. Na lau Uislamu ungelikuwa umekuja na Uhuru wa kuamini, watu wa wasingelikuwa na haja ya kutumiwa Mitume, kutumwa Vitabu. Na watu wasingelikuwa na haja ya kufanya Hajj na kupigana katika njia ya Allaah. Kila mmoja angelifuata matamanio yake. Kila mmoja angelikuwa Huru. Hapana! Allaah Anasema:

”Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” (adh-Dhaariyat 51 : 56)

Hakusema:
”… ili kila mmoja afuate matamanio yake.”

Kasema:
”… ila waniabudu Mimi.” (adh-Dhaariyat 51 : 56)

Kasema Allaah (Ta´ala):

”Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah na Dini iwe ya Allaah pekee.” (al-Baqarah 02 : 193)

Yule anayekataa kumuabudu Allaah, apigwe vita. Asiachwe! Mpaka arudi katika Dini au auawe. Uislamu haukuja na uhuru wa Dini za Kufuru na Mulhidah. Huku ni kumsemea Allaah (Ta´ala) uongo.

Vinginevyo, kwa nini Allaah Katuma Mitume na Akateremsha Vitabu na Akaweka katika Shari´ah Jihaad na Akawajibisha huduud na adhabu. Yote haya ni kwa ajili ya kulinda watu na Itikadi batili na maoni potevu. Ili kuwalinda kwa kuwa ni waja wa Allaah. Ni wajibu wamuabudu Allaah Mmoja asiyekuwa na mshirika. Au (wakikataa) ichukuliwe kutoka kwao Ujira uliyowekwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama Kauli Yake Allaah (Ta´ala):

“Hapana kulazimisha katika Dini.” (al-Baqarah 02 : 256)

Maana yake si kwamba mtu kuwa na Uhuru wa rai. Maana yake ni kwamba sisi hatuwezi kumlazimisha mtu Dini kuingia kwenye moyo wake. Hili hakuna anaeliweza isipokuwa Allaah.

”Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye.” (al-Qaswas 28 : 56)

Uongofu wa nyoyo uko kwenye Mikono ya Allaah, na haupitiki kwa kulazimisha, unapitika kwa khiyari. Lakini sisi tunapigana vita na makafiri na washirikina. Allaah Katuamrisha hilo. Tunaamrisha mema na kukataza maovu. Tunawabainishia watu (Dini ya Kiislamu). Na hatuwaambia:

”Hapana kulazimisha katika Dini.” (al-Baqarah 02 : 256)

Hatuwalazimishi watu kuingia katika Dini, lakini ni wajibu kwetu kuwabainishia Dini na kumuadhibu anayeiacha Dini hii. Ama mtu huyo kuongoka ndani ya moyo wake, hakuna awezae hili ila Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ndio maana ya:

”Hapana kulazimisha katika Dini.” (02:256)

Ni kama mfano wa Kauli Yake:

Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye.” (al-Qaswas 28 : 56)

Na Yule Aliyesema:
”Hapana kulazimisha katika Dini.” (al-Baqarah 02 : 256)

Ndie huyo huyo Aliyesema:
”Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah na Dini iwe ya Allaah pekee.” (02:193)

Kwa nini unachukua Aayah moja unaacha nyingine?!