al-Muzaniy Kuhusu Kumuona Allaah

Siku ya Qiyaamah [waumini] watamuona Mola Wao. Hawatopata usumbufu wowote kwa hilo na wala hawatoweka shaka. Himidi ni Zake kwa neema Yake nyuso zao zitang´ara na watamwangalia. Watabaki katika neema ya daima: لا يمسهم فيها نصب وما هم منها بمخرجين “Haitowagusa humo machofu nao humo hawatotolewa (watadumu milele).” مثل الجنة التي وعد المتقون تجري من تحتها الأنهار أكلها دآئم وظلها تلك عقبى الذين اتقوا وعقبى الكافرين النار "Mfano wa Jannah ambayo wameahidiwa wenye taqwa, (Pepo) inapita chini yake mito. Matunda yake ni ya kudumu, na (pia) kivuli chake. Hiyo ndiyo hatima (njema) ya wale waliokuwa na taqwa. Na hatima (mbaya) ya makafiri ni Moto.” Wakanushaji watazuiliwa kumuona Mola Wao. Wataunguzwa Motoni: ترى كثيرا منهم يتولون الذين كفروا لبئس ما قدمت لهم أنفسهم أن سخط الله عليهم وفي العذاب هم خالدون “Utawaona wengi miongoni mwao (Mayahudi katika mji wa Mtume) wanawafanya marafiki wale waliokufuru. Ubaya ulioje kwa yale waliyotanguliziwa na nafsi zao, (nayo ni) kuwa Allaah Amewaghadhibikia, na katika adhabu wao watadumu milele.” والذين كفروا لهم نار جهنم لا يقضى عليهم فيموتوا ولا يخفف عنهم من عذابها كذلك نجزي كل كفور "Na wale waliokufuru watapata (adhabu ya moto wa) Jahannam. Hawatahukumiwa (mauti) ili wafe, na wala hawatakhafifishiwa adhabu yake. Hivyo ndivyo Tunavyomlipa kila mwenye kukufuru mno.” Isipokuwa tu wale ambao Atataka kuwarehemu miongoni mwa wale waliokuwa wakimuabudu. Mwandishi: Imaam Ismaa´iyl bin Yahyaa al-Muzaniy (d. 264) Chanzo: as-Sunnah, uk. 43

Siku ya Qiyaamah [waumini] watamuona Mola Wao. Hawatopata usumbufu wowote kwa hilo na wala hawatoweka shaka. Himidi ni Zake kwa neema Yake nyuso zao zitang´ara na watamwangalia. Watabaki katika neema ya daima:

لا يمسهم فيها نصب وما هم منها بمخرجين
“Haitowagusa humo machofu nao humo hawatotolewa (watadumu milele).”

مثل الجنة التي وعد المتقون تجري من تحتها الأنهار أكلها دآئم وظلها تلك عقبى الذين اتقوا وعقبى الكافرين النار
“Mfano wa Jannah ambayo wameahidiwa wenye taqwa, (Pepo) inapita chini yake mito. Matunda yake ni ya kudumu, na (pia) kivuli chake. Hiyo ndiyo hatima (njema) ya wale waliokuwa na taqwa. Na hatima (mbaya) ya makafiri ni Moto.”

Wakanushaji watazuiliwa kumuona Mola Wao. Wataunguzwa Motoni:

ترى كثيرا منهم يتولون الذين كفروا لبئس ما قدمت لهم أنفسهم أن سخط الله عليهم وفي العذاب هم خالدون
“Utawaona wengi miongoni mwao (Mayahudi katika mji wa Mtume) wanawafanya marafiki wale waliokufuru. Ubaya ulioje kwa yale waliyotanguliziwa na nafsi zao, (nayo ni) kuwa Allaah Amewaghadhibikia, na katika adhabu wao watadumu milele.”

والذين كفروا لهم نار جهنم لا يقضى عليهم فيموتوا ولا يخفف عنهم من عذابها كذلك نجزي كل كفور
“Na wale waliokufuru watapata (adhabu ya moto wa) Jahannam. Hawatahukumiwa (mauti) ili wafe, na wala hawatakhafifishiwa adhabu yake. Hivyo ndivyo Tunavyomlipa kila mwenye kukufuru mno.”
Isipokuwa tu wale ambao Atataka kuwarehemu miongoni mwa wale waliokuwa wakimuabudu.

Mwandishi: Imaam Ismaa´iyl bin Yahyaa al-Muzaniy (d. 264)
Chanzo: as-Sunnah, uk. 43


  • Kitengo: Uncategorized , Kuonekana kwa Allaah siku ya Qiyaamah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013