al-Ikhwaan al-Muslimuun Hawajui Mfumo Waliomo

Ama usulubu ambao umezoeleka leo. Kusema kuwa fulani ni: "Salafiyyah katika ´Aqiydah na Ikhwaaniyyah katika Manhaj" Huu ni usulubu na istilahi chafu, potofu na yenye kutatiza. Ni nini maana ya Manhaj ya Ikhwaaniyyah? Ni ipi Manhaj ya al-Ikhwaan [al-Muslimuun]? Manhaj ya al-Ikhwaan [al-Muslimuun] wao wenyewe hawawezi kubainisha Manhaj yao. Shaykh Hasan al-Bannaa (Rahimahu Allaah), anaisifu Da´wah yake ya kwamba ni Suufiyyah, Salafiyyah au Ash´ariy. Anaisifu kwa migongano. Hivyo sisi wenyewe hatutajua Manhaj moja apitayo juu yake. Kwa ajili hiyo, watu hawa wenyewe hawajui Manhaj yao. Manhaj yao inaweza kutofautiana kutokea mji hadi mwingine, na hili analijua yule ambaye kaishi katika miji mbali mbali. Utawaona kuwa ni wenye kutofautiana, na huenda wakawa katika mji mmoja. Utaona wana Manhaj za kutofautiana, kila kikundi kina Manhaj yake. Kwa kuwa ni Manhaj potofu. Msizitaabishe nasfi zenu. Huyu kijana amewasomea Bid´ah mpya [ya kusema fulani ni Salafiy Ikhwaaniy] enyi vijana. Ni juu yenu kubakia juu ya haki. Nyinyi mko katika haki na mtaendelea kuwa katika haki In Shaa Allaah.

Ama usulubu ambao umezoeleka leo. Kusema kuwa fulani ni:

“Salafiyyah katika ´Aqiydah na Ikhwaaniyyah katika Manhaj”

Huu ni usulubu na istilahi chafu, potofu na yenye kutatiza. Ni nini maana ya Manhaj ya Ikhwaaniyyah? Ni ipi Manhaj ya al-Ikhwaan [al-Muslimuun]? Manhaj ya al-Ikhwaan [al-Muslimuun] wao wenyewe hawawezi kubainisha Manhaj yao. Shaykh Hasan al-Bannaa (Rahimahu Allaah), anaisifu Da´wah yake ya kwamba ni Suufiyyah, Salafiyyah au Ash´ariy. Anaisifu kwa migongano. Hivyo sisi wenyewe hatutajua Manhaj moja apitayo juu yake. Kwa ajili hiyo, watu hawa wenyewe hawajui Manhaj yao. Manhaj yao inaweza kutofautiana kutokea mji hadi mwingine, na hili analijua yule ambaye kaishi katika miji mbali mbali. Utawaona kuwa ni wenye kutofautiana, na huenda wakawa katika mji mmoja. Utaona wana Manhaj za kutofautiana, kila kikundi kina Manhaj yake. Kwa kuwa ni Manhaj potofu. Msizitaabishe nasfi zenu. Huyu kijana amewasomea Bid´ah mpya [ya kusema fulani ni Salafiy Ikhwaaniy] enyi vijana. Ni juu yenu kubakia juu ya haki. Nyinyi mko katika haki na mtaendelea kuwa katika haki In Shaa Allaah.