al-Halabiy Na ´Ar´uur Na Umoja Wa Dini Zote

Usidanganyike na makala ya ´Aliy al-Halabiy ambapo anamfanyia Takfiyr yule mwenye kusema kwamba dini zote inatakiwa ziwe na umoja. Ana sura nyingi. Aliwafanyia Takfiyr watu hawa hapo kabla. Wakati toleo la The Amman Message, ambayo ilikuwa na wito wa umoja wa dini, udugu, uhuru wa dini, usawa wa dini na upotevu mwingine, lilipotoka akasifu gazeti hilo, akalazimisha hilo na kuonelea kuwa linafafanua Uislamu na kuwakilisha ukati na kati wa Uislamu. Wakati Salafiyyuun walipokemea upotevu huu akautetea yeye na kundi lake vikali. Wakawatukana wale waliokemea upotevu huu na wakasifu utetezi na watetezi. Isitoshe akasifu wale wenye kunusuru upotevu huu ambao kwa kiasi kikubwa ndani yake kuna Raafidhwah, Suufiyyah wapindaji na wanasekula. Mpaka hivi leo hajajirejea juu ya hilo. Hivi karibuni ´Adnaan ´Ar´uur amefanya wito hadharani katika uhuru wa dini.[1] Hili halikumtikisa al-Halabiy. Kana kwamba hakukupitika chochote. Uhakika wa mambo ni kwamba alishiriki pamoja naye katika moja ya semina kwenye chaneli ya Wisaal baada ya jambo hili lililofanywa hadharani. Kwa hali hiyo, je, kweli mtu amwamini al-Halabiy wakati anapomfanyia Takfiyr yule mwenye kuita katika uhuru wa dini? --------------------- (1) http://www.wanachuoni.com/content/%C2%B4allaamah-al-luhaydaan-kuhusu-kauli-ya-al-%C2%B4ar%C2%B4uur-kushikamana-na-kamba-ya-allaah Mwandishi: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy Chanzo: Bayaan maa fiy Naswiyhati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 207 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Usidanganyike na makala ya ´Aliy al-Halabiy ambapo anamfanyia Takfiyr yule mwenye kusema kwamba dini zote inatakiwa ziwe na umoja. Ana sura nyingi. Aliwafanyia Takfiyr watu hawa hapo kabla. Wakati toleo la The Amman Message, ambayo ilikuwa na wito wa umoja wa dini, udugu, uhuru wa dini, usawa wa dini na upotevu mwingine, lilipotoka akasifu gazeti hilo, akalazimisha hilo na kuonelea kuwa linafafanua Uislamu na kuwakilisha ukati na kati wa Uislamu.

Wakati Salafiyyuun walipokemea upotevu huu akautetea yeye na kundi lake vikali. Wakawatukana wale waliokemea upotevu huu na wakasifu utetezi na watetezi. Isitoshe akasifu wale wenye kunusuru upotevu huu ambao kwa kiasi kikubwa ndani yake kuna Raafidhwah, Suufiyyah wapindaji na wanasekula. Mpaka hivi leo hajajirejea juu ya hilo.

Hivi karibuni ´Adnaan ´Ar´uur amefanya wito hadharani katika uhuru wa dini.[1] Hili halikumtikisa al-Halabiy. Kana kwamba hakukupitika chochote. Uhakika wa mambo ni kwamba alishiriki pamoja naye katika moja ya semina kwenye chaneli ya Wisaal baada ya jambo hili lililofanywa hadharani. Kwa hali hiyo, je, kweli mtu amwamini al-Halabiy wakati anapomfanyia Takfiyr yule mwenye kuita katika uhuru wa dini?

———————
(1) http://www.wanachuoni.com/content/%C2%B4allaamah-al-luhaydaan-kuhusu-kauli-ya-al-%C2%B4ar%C2%B4uur-kushikamana-na-kamba-ya-allaah

Mwandishi: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Chanzo: Bayaan maa fiy Naswiyhati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 207
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-´Ar´uur, ´Adnaan
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 10th, April 2014