al-Halabiy, Muhammad Hassan, ´Ar´uur Na al-Maghraawiy

Kuna kariri kila wakati maswali kuhusu [´Aliy] al-Halabiy na sisi tunayajibu. Tunapoulizwa tunajibu, wala haijuzu kwetu kunyamaza kimya. al-Halabiy hadi sasa hajajirejea katika umoja wa Dini ya The Amman Message na kauli kuhusu umoja wa Dini, udugu wa Dini, usawa wa Dini na ni wajibu kuhukumu kwa FN. Hajajirejea katika moja katika hilo wala hata kwa hefuri. Anawasifia watu wa Bid´ah na Hizbiyyuun na kusema kuwa Muhammad Hassan ni Salafiy, ´Adnaan ´Ar´uur ni Salafiy, al-Maghraawiy ni Salafiy na fulani ni Salafiy. Na hawa watu wameongelewa na wanachuoni na kubainisha makosa yao. Na yeye anaendelea hadi hivi leo kuwatetea. Bali hadi kwenye maandamano alikuwa akiendelea kumsifia Muhammad Hassan. Na baada ya hapo nikaona makala aliposema "mimi niliwapa idhini wanafunzi kumradi." Mashaa Allaah na ilihali wewe ndiye uliyemsifia. Je, si wajibu kwako kumradi khasa ukizingatia kuwa wewe ndiye uliyemsifia? Je si wajibu kwako kumradi? Ninawauliza nyinyi kwa Jina la Allaah mtu ambaye kamsifia mtu na kumtakasa, na baada ya hapo kakaa kimya na kusema eti niliwaambia wengine wamradi. Hili lakubalika? Hili halikubaliki. Wewe mwenyewe binafsi ambaye uliwashughulisha watu na kuwapoteza kwa kumsifia huyu Khaarijiy, Mubtadi´ mpotofu ambaye alijigamba kwa uasi, maandamano ambayo yalikuwa na mchanganyiko wa wanawake na wanaume, akajigamba jinsi alivyotoka yeye na mke wake hadi na watoto wake. Kisha unasema Khalas nimekwishatoa idhini ya kumradi. Haya ni maneno, kamwe kabisa. Haya ni maneno ya mfanya ujanja. Sisi hatwendi namna hii. Wewe ndiye uliyemsifu na wewe ndiye wajibu kwako kubainisha hali yake.

Kuna kariri kila wakati maswali kuhusu [´Aliy] al-Halabiy na sisi tunayajibu. Tunapoulizwa tunajibu, wala haijuzu kwetu kunyamaza kimya. al-Halabiy hadi sasa hajajirejea katika umoja wa Dini ya The Amman Message na kauli kuhusu umoja wa Dini, udugu wa Dini, usawa wa Dini na ni wajibu kuhukumu kwa FN. Hajajirejea katika moja katika hilo wala hata kwa hefuri.

Anawasifia watu wa Bid´ah na Hizbiyyuun na kusema kuwa Muhammad Hassan ni Salafiy, ´Adnaan ´Ar´uur ni Salafiy, al-Maghraawiy ni Salafiy na fulani ni Salafiy. Na hawa watu wameongelewa na wanachuoni na kubainisha makosa yao. Na yeye anaendelea hadi hivi leo kuwatetea. Bali hadi kwenye maandamano alikuwa akiendelea kumsifia Muhammad Hassan. Na baada ya hapo nikaona makala aliposema “mimi niliwapa idhini wanafunzi kumradi.” Mashaa Allaah na ilihali wewe ndiye uliyemsifia. Je, si wajibu kwako kumradi khasa ukizingatia kuwa wewe ndiye uliyemsifia? Je si wajibu kwako kumradi? Ninawauliza nyinyi kwa Jina la Allaah mtu ambaye kamsifia mtu na kumtakasa, na baada ya hapo kakaa kimya na kusema eti niliwaambia wengine wamradi. Hili lakubalika? Hili halikubaliki. Wewe mwenyewe binafsi ambaye uliwashughulisha watu na kuwapoteza kwa kumsifia huyu Khaarijiy, Mubtadi´ mpotofu ambaye alijigamba kwa uasi, maandamano ambayo yalikuwa na mchanganyiko wa wanawake na wanaume, akajigamba jinsi alivyotoka yeye na mke wake hadi na watoto wake. Kisha unasema Khalas nimekwishatoa idhini ya kumradi. Haya ni maneno, kamwe kabisa. Haya ni maneno ya mfanya ujanja. Sisi hatwendi namna hii. Wewe ndiye uliyemsifu na wewe ndiye wajibu kwako kubainisha hali yake.