al-Barbahaariy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah

Mapokezi haya yote ambayo umesikia lakini hayaingii akilini mwako, ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Mioyo ya waja iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah (´Azza wa Jalla).” "Kwa hakika Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Hushuka chini kwenye mbingu ya chini." "Hushuka siku ya ´Arafah." "Hakutoachwa kutupwa [watu na mawe] Motoni mpaka hapo Allaah (´Azza wa Jalla) Atapoweka Mguu Wake juu yake.” Kauli ya Allaah (Ta´ala) kwa waja Wake: “Ukinijia Mimi, ntakujia kwa kasi.” "Kwa hakika Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Hushuka siku ya 'Arafah." "Kwa hakika Allaah Kamuumba Aadam kwa sura Yake." “Nilimuona Mola Wangu kwa sura nzuri kabisa.” Na Hadiyth mfano wa hizo, ni lazima kwako kujisalimisha, kuzithibitisha, usijiingize katika namna na uwe ni mwenye kuzifurahia na kutosheka nazo. Usizifasiri kwa matamanio yako. Kwa hakika ni lazima kuamini hili. Yeyote yule ambaye atafasiri chochote katika hizo kwa matamanio yake au kuzikataa, ni Jahmiy. Mwandishi: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (d. 329) Chanzo: Sharh-us-Sunnah, uk. 74-76.

Mapokezi haya yote ambayo umesikia lakini hayaingii akilini mwako, ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Mioyo ya waja iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah (´Azza wa Jalla).”

“Kwa hakika Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Hushuka chini kwenye mbingu ya chini.”

“Hushuka siku ya ´Arafah.”

“Hakutoachwa kutupwa [watu na mawe] Motoni mpaka hapo Allaah (´Azza wa Jalla) Atapoweka Mguu Wake juu yake.”

Kauli ya Allaah (Ta´ala) kwa waja Wake:
“Ukinijia Mimi, ntakujia kwa kasi.”

“Kwa hakika Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Hushuka siku ya ‘Arafah.”

“Kwa hakika Allaah Kamuumba Aadam kwa sura Yake.”

“Nilimuona Mola Wangu kwa sura nzuri kabisa.”

Na Hadiyth mfano wa hizo, ni lazima kwako kujisalimisha, kuzithibitisha, usijiingize katika namna na uwe ni mwenye kuzifurahia na kutosheka nazo. Usizifasiri kwa matamanio yako. Kwa hakika ni lazima kuamini hili. Yeyote yule ambaye atafasiri chochote katika hizo kwa matamanio yake au kuzikataa, ni Jahmiy.

Mwandishi: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (d. 329)
Chanzo: Sharh-us-Sunnah, uk. 74-76.


  • Kitengo: Uncategorized , Kushuka (kuteremka) kwa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013