Aina Za Khul´

Khul´ (mwanamke kujivua katika ndoa) iko aina tatu: 1- Inayoruhusiwa. Ina maana mwanamke anamchukia mume wake na anachelea kutotimiza haki zake na kushika mipaka ya Allaah katika kumtii Allah. Allaah (Ta´ala) Amesema: "Mtakapokhofu kuwa wote wawili (mume na mke) hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah; basi hakuna dhambi juu yao katika atakachojikombolea kwacho mke." (02:229) al-Bukhaariy amepokea na isnadi yake: Mke wa Thaabit bin Qays alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: "Ewe Mtume wa Allaah! Sina lolote la kumtuhumu Thaabit si katika Dini wala tabia isipokuwa tu nachelea kutotimiza haki zake katika Uislamu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: "Je, utamrudishia shamba lake?" Akasema: "Ndio. Akamrudishia nalo na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuamrisha kutengana naye." Vilevile mwanamke akawa na haja ya kutengana naye, na hilo analifikia tu kwa mbadala. 2- Inayochukizwa. Ina maana Khul´ pasina sababu yoyote wakati hali baina ya mke na mume ni nzuri. Marafiki zetu wanaonelea kuwa inachukizwa. Allaah (Ta´ala) Amesema: "Lakini wakitoa chochote wenyewe katika mahari yao kwa khiari zao, basi kuleni kwa raha na muruwa." (04:04) Kutoka katika kauli ya Ahmad mtu anaweza kufahamu pia kwamba ni haramu na si sahihi. Amesema: Khul´ ni kama Hadiyth ya Sahlah; alimchukia mume wake na akamrudishia mahari. Hii ndio Khul´. Dalili ya hilo ni Kauli Yake (Ta´ala): "Mtakapokhofu kuwa wote wawili (mume na mke) hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah; basi hakuna dhambi juu yao katika atakachojikombolea kwacho mke." (02:229) Thawbah ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: "Mwanamke akimuomba Talaka mume wake pasina neno[1], hatonusa harufu ya Pepo." (Abu Daawuud (2226). al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh. (Swahiyh Sunan Abiy Daawuud (2/17) Imepokelewa na Abu Daawuud. 3- Haramu. Ina maana ya kwamba mume anamkandamiza mwanamke na kumdulumu haki zake ili aweze kuomba Talaka. Hili ni haramu. Allaah (Ta´ala) Amesema: "Na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa." (04:19) Mume hastahiki kupewa badala hii akitengana naye katika hali hii na kupata badala, kwa kuwa mwanamke amelazimishwa kumpa hilo. Kwa hivyo hastahiki hilo. ---------------- (1) Imaam al-´Adhiymaabaadiy (Rahimahu Allaah) amesema: "Bila ya uzito wowote wenye kumlazimisha kuomba Talaka." (´Awn-ul-Ma´buud Sharh Sunan Abiy Daawuud (6/220))

Khul´ (mwanamke kujivua katika ndoa) iko aina tatu:

1- Inayoruhusiwa. Ina maana mwanamke anamchukia mume wake na anachelea kutotimiza haki zake na kushika mipaka ya Allaah katika kumtii Allah. Allaah (Ta´ala) Amesema:

“Mtakapokhofu kuwa wote wawili (mume na mke) hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah; basi hakuna dhambi juu yao katika atakachojikombolea kwacho mke.” (02:229)

al-Bukhaariy amepokea na isnadi yake:

Mke wa Thaabit bin Qays alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia:

“Ewe Mtume wa Allaah! Sina lolote la kumtuhumu Thaabit si katika Dini wala tabia isipokuwa tu nachelea kutotimiza haki zake katika Uislamu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Je, utamrudishia shamba lake?” Akasema: “Ndio. Akamrudishia nalo na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuamrisha kutengana naye.”

Vilevile mwanamke akawa na haja ya kutengana naye, na hilo analifikia tu kwa mbadala.

2- Inayochukizwa. Ina maana Khul´ pasina sababu yoyote wakati hali baina ya mke na mume ni nzuri.

Marafiki zetu wanaonelea kuwa inachukizwa. Allaah (Ta´ala) Amesema:

“Lakini wakitoa chochote wenyewe katika mahari yao kwa khiari zao, basi kuleni kwa raha na muruwa.” (04:04)

Kutoka katika kauli ya Ahmad mtu anaweza kufahamu pia kwamba ni haramu na si sahihi. Amesema:

Khul´ ni kama Hadiyth ya Sahlah; alimchukia mume wake na akamrudishia mahari. Hii ndio Khul´.

Dalili ya hilo ni Kauli Yake (Ta´ala):

“Mtakapokhofu kuwa wote wawili (mume na mke) hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah; basi hakuna dhambi juu yao katika atakachojikombolea kwacho mke.” (02:229)

Thawbah ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke akimuomba Talaka mume wake pasina neno[1], hatonusa harufu ya Pepo.” (Abu Daawuud (2226). al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh. (Swahiyh Sunan Abiy Daawuud (2/17)

Imepokelewa na Abu Daawuud.

3- Haramu. Ina maana ya kwamba mume anamkandamiza mwanamke na kumdulumu haki zake ili aweze kuomba Talaka. Hili ni haramu. Allaah (Ta´ala) Amesema:

“Na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa.” (04:19)

Mume hastahiki kupewa badala hii akitengana naye katika hali hii na kupata badala, kwa kuwa mwanamke amelazimishwa kumpa hilo. Kwa hivyo hastahiki hilo.

—————-
(1) Imaam al-´Adhiymaabaadiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Bila ya uzito wowote wenye kumlazimisha kuomba Talaka.” (´Awn-ul-Ma´buud Sharh Sunan Abiy Daawuud (6/220))


  • Author: Imaam Ibn Qudaamah al-Maqdisiy. al-Kaafiy (3/141-143) - al-Maktab al-Islaamiy, 1408/1988
  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 21st, January 2014