Ahl-us-Sunnah Kila Andiko Lililothibiti Wanalifanyia Kazi

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema: Kuamini Qadar, kheri na shari yake na kusadikisha Ahaadiyth juu yake na kuziamini. Haisemwi: “Kwa nini?” “Vipi?” Inachotakiwa ni kusadikisha hilo na kuamini Huu ndio msimamo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Msimamo wao juu ya maandiko yote kwa jumla, kila andiko ambalo limethibiti katika Kitabu cha Allaah na Hadiyth Swahiyh za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao wanafuata uongofu wa Salaf wanakubali hilo na wanakimbilia kulifunza na kulifanyia kazi Muqtadhwa yake. Hili ni kwa kila andiko, sawa ikiwa ni katika mlango wa I´tiqaad au milango mingine katika milango ya elimu. Katika hayo ni maandiko ambayo yalithibiti juu ya Qadar. Makadirio ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) juu ya mambo yote. Wanayaamini maandiko ambayo yalithibiti katika mlango huu mkubwa ambao wamepotea ndani yake waliyopotea katika mapote maangamivu. Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy Chanzo: Usuul-us-Sunnah Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=1005&size=2h&ext=.rm

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

Kuamini Qadar, kheri na shari yake na kusadikisha Ahaadiyth juu yake na kuziamini. Haisemwi: “Kwa nini?” “Vipi?” Inachotakiwa ni kusadikisha hilo na kuamini

Huu ndio msimamo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Msimamo wao juu ya maandiko yote kwa jumla, kila andiko ambalo limethibiti katika Kitabu cha Allaah na Hadiyth Swahiyh za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao wanafuata uongofu wa Salaf wanakubali hilo na wanakimbilia kulifunza na kulifanyia kazi Muqtadhwa yake. Hili ni kwa kila andiko, sawa ikiwa ni katika mlango wa I´tiqaad au milango mingine katika milango ya elimu. Katika hayo ni maandiko ambayo yalithibiti juu ya Qadar. Makadirio ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) juu ya mambo yote. Wanayaamini maandiko ambayo yalithibiti katika mlango huu mkubwa ambao wamepotea ndani yake waliyopotea katika mapote maangamivu.

Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy
Chanzo: Usuul-us-Sunnah
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=1005&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 28th, March 2014