Ahl-ul-Bid´ah Watazuiwa Kunywa Kwenye Hodhi Ya Mtume (´alayhis-Salaam)

2- Hodhi Mwandishi anasema “Wala hodhi”, hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kumethibiti kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ana hodhi: “Urefu wake ni (mwendo wa) mwezi na upana wake ni mwezi. Maji yake ni meupe kuliko maziwa na matamu kuliko asali. Vikombe vyake ni wingi wa idadi ya nyota mbinguni.” Ummah wake utakunywa humo na atazuiwa kila Mubtadiy´, mzushi na kila aliyeritadi. Yule aliyeritadi atazuiwa na wala Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hatomtaka. Atapouliza kwa nini wamerudishwa? Ataambiwa: “Hawakuacha kuwa wenye kuritadi katika ´Aqiydah zao.” Katika sifa ya pili ataambiwa: “Hakika wewe hujui waliyozusha baada yako.” Kila aliyezusha Bid´ah katika Dini; kama Mu´tazilah, Khawaarij, Shiy´ah na mapote mengine ya upotevu ambayo yalizusha katika Dini yasiyokuwemo watazuiwa na hodhi siku ya Qiyaamah. Kila mzushi na aliyeritadi atazuiawa. Hakuna wataoachwa kunywa humo isipokuwa watu waliokuwa na imani ya kweli waliothibiti katika imani duniani na wakafa juu yake, hawa ndio wataachwa na kunywa ndani ya hodhi mara moja na hawatohisi kiu baada ya hapo kamwe. Hii ndio hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule aliyeshikamana bara bara na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) duniani na akazitendea kazi, ataachiwa hodhi na atakunywa kwenye hodhi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule aliyepuuza Sunnah na akazusha Bid´ah au akaritadi kutoka katika Dini yake, atazuiwa na kufukuzwa kutoka kwenye hodhi hali ya kuwa atakuwa na haja kubwa ya maji. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 166-167

2- Hodhi

Mwandishi anasema “Wala hodhi”, hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kumethibiti kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ana hodhi:

“Urefu wake ni (mwendo wa) mwezi na upana wake ni mwezi. Maji yake ni meupe kuliko maziwa na matamu kuliko asali. Vikombe vyake ni wingi wa idadi ya nyota mbinguni.”

Ummah wake utakunywa humo na atazuiwa kila Mubtadiy´, mzushi na kila aliyeritadi. Yule aliyeritadi atazuiwa na wala Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hatomtaka. Atapouliza kwa nini wamerudishwa? Ataambiwa:

“Hawakuacha kuwa wenye kuritadi katika ´Aqiydah zao.”

Katika sifa ya pili ataambiwa:

“Hakika wewe hujui waliyozusha baada yako.”

Kila aliyezusha Bid´ah katika Dini; kama Mu´tazilah, Khawaarij, Shiy´ah na mapote mengine ya upotevu ambayo yalizusha katika Dini yasiyokuwemo watazuiwa na hodhi siku ya Qiyaamah. Kila mzushi na aliyeritadi atazuiawa. Hakuna wataoachwa kunywa humo isipokuwa watu waliokuwa na imani ya kweli waliothibiti katika imani duniani na wakafa juu yake, hawa ndio wataachwa na kunywa ndani ya hodhi mara moja na hawatohisi kiu baada ya hapo kamwe. Hii ndio hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Yule aliyeshikamana bara bara na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) duniani na akazitendea kazi, ataachiwa hodhi na atakunywa kwenye hodhi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule aliyepuuza Sunnah na akazusha Bid´ah au akaritadi kutoka katika Dini yake, atazuiwa na kufukuzwa kutoka kwenye hodhi hali ya kuwa atakuwa na haja kubwa ya maji.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 166-167


  • Kitengo: Uncategorized , Aakhirah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 22nd, February 2014