Ahl-ul-Bid´ah Tu Ndio Wanamchukia Ibn Baaz, al-Albaaniy Na Ibn ´Uthaymiyn

as-Swaabuuniy amekufa katikati ya karne ya 500. Hata baada yake waliishi maimamu wa Uislamu na wanachuoni kama wanachuoni wa Jerusalemu (Maqaadisah), Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim, adh-Dhahabiy, Ibn Kathiyr na wengine wengi ambao waliitumikia Sunnah na kuopandisha bendera yake. Baada yao akaja Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) na wanafunzi zake. Kundi hili halitokatika kamwe kwa mujibu wa maneno ya mkweli na mwaminifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hakutoacha siku zote kuendelea kuwepo kwa kundi katika Ummah wangu lenye kunusuriwa katika haki. Halitodhuriwa na wale wenye kuwapinga na kwenda kinyume nao mpaka amri ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) ije.” Mtu ana mfumo gani ikiwa anamchukia Ibn Taymiyyah na Ibn ´Abdil-Wahhaab (Rahimahumaa Allaah)? Mtu ana mfumo gani ikiwa anamchukia Ibn Baaz, al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn na watu mfano wao? Ni katika Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal bila ya shaka. Unaweza kuona jinsi makundi yanaacha kuwatakia rahmah. Wanawachukia na kwenda kinyume nao na mfumo wao. Kituo chao ni kituo cha Ahl-ul-Bid´ah. Tunawapenda wanachuoni hawa kwa sababu wamehifadhi na kufikisha Sunnah na ´Aqiydah. Wameipigania. Allaah Awarahamu! Tunasimama katika upande wao na tunawapenda. Kuwachukia ni alama ya Ahl-ul-Bid´ah. Kadhalika watu waliokuja baada yao ambao wana mfumo wao. Ni Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal ndio wanawachukia. Mzungumzaji: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy Chanzo: Sharh ´Aqiydat-is-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 349 Toleo la: 13-07-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

as-Swaabuuniy amekufa katikati ya karne ya 500. Hata baada yake waliishi maimamu wa Uislamu na wanachuoni kama wanachuoni wa Jerusalemu (Maqaadisah), Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim, adh-Dhahabiy, Ibn Kathiyr na wengine wengi ambao waliitumikia Sunnah na kuopandisha bendera yake. Baada yao akaja Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) na wanafunzi zake. Kundi hili halitokatika kamwe kwa mujibu wa maneno ya mkweli na mwaminifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakutoacha siku zote kuendelea kuwepo kwa kundi katika Ummah wangu lenye kunusuriwa katika haki. Halitodhuriwa na wale wenye kuwapinga na kwenda kinyume nao mpaka amri ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) ije.”

Mtu ana mfumo gani ikiwa anamchukia Ibn Taymiyyah na Ibn ´Abdil-Wahhaab (Rahimahumaa Allaah)?

Mtu ana mfumo gani ikiwa anamchukia Ibn Baaz, al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn na watu mfano wao? Ni katika Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal bila ya shaka. Unaweza kuona jinsi makundi yanaacha kuwatakia rahmah. Wanawachukia na kwenda kinyume nao na mfumo wao. Kituo chao ni kituo cha Ahl-ul-Bid´ah.

Tunawapenda wanachuoni hawa kwa sababu wamehifadhi na kufikisha Sunnah na ´Aqiydah. Wameipigania. Allaah Awarahamu! Tunasimama katika upande wao na tunawapenda. Kuwachukia ni alama ya Ahl-ul-Bid´ah. Kadhalika watu waliokuja baada yao ambao wana mfumo wao. Ni Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal ndio wanawachukia.

Mzungumzaji: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Chanzo: Sharh ´Aqiydat-is-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 349
Toleo la: 13-07-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 13th, July 2014