Adabu Ya Kipande Cha Chakula Kinachoanguka Chini

1862 - Qutaybah alitueleza: Ibn Lahiy'ah alitueleza, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Kama mmoja wenu anakula chakula na kipande cha chakula kikaanguka chini, anatakiwa kukitoa utata na kukila bila ya kumuachia nacho Shaytwaan."   MAELEZO "... anatakiwa kukitoa utata... " - Bi maana kufuta na kutoa kila kinachochukiza kama mchanga, udongo, uchafu na mfano wa hayo. "... bila ya kumuachia nacho Shaytwaan... " - at-Tuurbashtiy amesema: "Kwamba kinaachiwa Shaytwaan ni kwa sababu neema ya Allaah inaenda bure na kwamba mtu anakidharau bila ya haki na kwamba ni katika tabia za wenye kujiona. Mara nyingi huwa ni majivuno ndio yanamzuia mtu kula kipande hicho cha chakula - na kujiona ni katika matendo ya Shaytwaan." an-Nawawiy amesema: "Katika Hadiyth kuna mapendekezo ya kula vipande vya vyakula baada ya kuvitoa uchafu maadamu mahali hapo sio najisi. Endapo chakula kitaanguka mahali pa najisi, mtu analazimika kukiosha ikiwa inawezekana. Ikiwa haiwezekani kukitoa (kitu hicho cha najisi), akitoe na kumpa mnyama bila ya kumuachia nacho Shaytwaan." Mwandishi: Imaam Muhammad bin Iysaa at-Tirmidhiy (d. 279) Chanzo: al-Jaami´ (1862) Maelezo: Imaam Muhammad ´Abdur-Rahmaan al-Mubaarakfuuriy (d. 1353) Chanzo: Tuhfat-ul-Ahwadhiy (5/424-425)

1862 – Qutaybah alitueleza: Ibn Lahiy’ah alitueleza, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Kama mmoja wenu anakula chakula na kipande cha chakula kikaanguka chini, anatakiwa kukitoa utata na kukila bila ya kumuachia nacho Shaytwaan.”
 
MAELEZO

“… anatakiwa kukitoa utata… ” – Bi maana kufuta na kutoa kila kinachochukiza kama mchanga, udongo, uchafu na mfano wa hayo.

“… bila ya kumuachia nacho Shaytwaan… ” – at-Tuurbashtiy amesema:

“Kwamba kinaachiwa Shaytwaan ni kwa sababu neema ya Allaah inaenda bure na kwamba mtu anakidharau bila ya haki na kwamba ni katika tabia za wenye kujiona. Mara nyingi huwa ni majivuno ndio yanamzuia mtu kula kipande hicho cha chakula – na kujiona ni katika matendo ya Shaytwaan.”

an-Nawawiy amesema:

“Katika Hadiyth kuna mapendekezo ya kula vipande vya vyakula baada ya kuvitoa uchafu maadamu mahali hapo sio najisi. Endapo chakula kitaanguka mahali pa najisi, mtu analazimika kukiosha ikiwa inawezekana. Ikiwa haiwezekani kukitoa (kitu hicho cha najisi), akitoe na kumpa mnyama bila ya kumuachia nacho Shaytwaan.”

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Iysaa at-Tirmidhiy (d. 279)
Chanzo: al-Jaami´ (1862)
Maelezo: Imaam Muhammad ´Abdur-Rahmaan al-Mubaarakfuuriy (d. 1353)
Chanzo: Tuhfat-ul-Ahwadhiy (5/424-425)


  • Kitengo: Uncategorized , Chakula
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 20th, January 2014