Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) Ndiye Mbora Wa Maswahabah

Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) ndiye mbora katika Makhaliyfah. Allaah Amemsifu kwa Kauli Yake: وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنكُمْ وَالسَّعَةِ أَن يُؤْتُوا أُولِي الْقُرْبَىٰ “Na wala wasiape wale (waliojaaliwa kuwa ni) wenye fadhila miongoni mwenu na wasaa (katika maisha) kuwa hawatowapa (msaada, swadaqah) jamaa wa karibu.” (an-Nuur:22) Aayah hii imeteremka kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati alipoapa kwamba hatompa Mistwaah bin Uthaathah kitu katika mali. Alikuwa ni ndugu yake na akimhudumia. Pindi alipodanganyika kutokana na wale waliomsema kwa ubaya, akawasadikisha na akaongea nao. Abu Bakr akamkasirikia na akaapa kuwa hatompa tena. Allaah Akawa Ameteremsha Aayah hii: ”Na wala wasiape”, yaani asiape: “... wenye fadhila”. Akamsifu Abu Bakr kwamba yeye ni Ulul-Fadhwl. Katika Aayah nyingine: إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ “Msipomnusuru (Mtume), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa wale waliokufuru akiwa wa pili katika wawili (na wapili wake ni Abu Bakr).” (at-Tawbah:40) Ni kina nani watu hawa wawili? Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Abu Bakr. Hili ni kwa Ijmaa´: إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ “... alipomwambia swahibu yake.” (at-Tawbah:40) Akamthibitishia usuhuba wake kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Abu Bakr ndio mbora katika Maswahabah. Kama linavosadikisha hilo Hadiyth Swahiyh katika al-Bukhaariy na (vitabu) vinginevyo. Mbora katika Ummah huu ni Abu Bakr. Hilo ni kutokana na kuwa kwake mbele katika Uislamu na kumnusuru kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kulazimiana naye. Na wakati alipokufa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Ummah ulikubaliana kumchagua Abu Bakr. Na wakati waliporitadi wenye kuritadi katika waarabu, mtu ambaye alisimama kidete dhidi yao na kuwapiga vita ni Abu Bakr, mpaka Allaah Akaithibitisha Dini hii na kuwazima walioritadi. Fadhila zake ni nyingi (Radhiya Allaahu ´anhu). Vilevile anaitwa asw-Swiddiyq. Daraja ya wakweli ni baada ya Mitume. Anasema (Ta´ala): وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا “Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii, na asw-Swiddiqiyna na Mashahidi na (waja) wema, na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki (zake).” (an-Nisaa:69) “asw-Swiddiyq” ni mtu mkweli sana na aliyepindukia katika ukweli. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mtu huendelea kusema ukweli na kujitahidi kuendelea hivyo hadi itarekodiwa na Allaah kuwa ni mkweli.” Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 116-118

Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) ndiye mbora katika Makhaliyfah. Allaah Amemsifu kwa Kauli Yake:

وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنكُمْ وَالسَّعَةِ أَن يُؤْتُوا أُولِي الْقُرْبَىٰ
“Na wala wasiape wale (waliojaaliwa kuwa ni) wenye fadhila miongoni mwenu na wasaa (katika maisha) kuwa hawatowapa (msaada, swadaqah) jamaa wa karibu.” (an-Nuur:22)

Aayah hii imeteremka kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati alipoapa kwamba hatompa Mistwaah bin Uthaathah kitu katika mali. Alikuwa ni ndugu yake na akimhudumia. Pindi alipodanganyika kutokana na wale waliomsema kwa ubaya, akawasadikisha na akaongea nao. Abu Bakr akamkasirikia na akaapa kuwa hatompa tena. Allaah Akawa Ameteremsha Aayah hii:

”Na wala wasiape”, yaani asiape:

“… wenye fadhila”. Akamsifu Abu Bakr kwamba yeye ni Ulul-Fadhwl. Katika Aayah nyingine:

إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ
“Msipomnusuru (Mtume), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa wale waliokufuru akiwa wa pili katika wawili (na wapili wake ni Abu Bakr).” (at-Tawbah:40)

Ni kina nani watu hawa wawili?

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Abu Bakr. Hili ni kwa Ijmaa´:

إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ
“… alipomwambia swahibu yake.” (at-Tawbah:40)

Akamthibitishia usuhuba wake kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Abu Bakr ndio mbora katika Maswahabah. Kama linavosadikisha hilo Hadiyth Swahiyh katika al-Bukhaariy na (vitabu) vinginevyo. Mbora katika Ummah huu ni Abu Bakr. Hilo ni kutokana na kuwa kwake mbele katika Uislamu na kumnusuru kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kulazimiana naye. Na wakati alipokufa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Ummah ulikubaliana kumchagua Abu Bakr. Na wakati waliporitadi wenye kuritadi katika waarabu, mtu ambaye alisimama kidete dhidi yao na kuwapiga vita ni Abu Bakr, mpaka Allaah Akaithibitisha Dini hii na kuwazima walioritadi. Fadhila zake ni nyingi (Radhiya Allaahu ´anhu).

Vilevile anaitwa asw-Swiddiyq. Daraja ya wakweli ni baada ya Mitume. Anasema (Ta´ala):

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا
“Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii, na asw-Swiddiqiyna na Mashahidi na (waja) wema, na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki (zake).” (an-Nisaa:69)

“asw-Swiddiyq” ni mtu mkweli sana na aliyepindukia katika ukweli. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtu huendelea kusema ukweli na kujitahidi kuendelea hivyo hadi itarekodiwa na Allaah kuwa ni mkweli.”

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 116-118


  • Kitengo: Uncategorized , Maswahabah wa kiume
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 17th, February 2014