Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) Ndio Mujaddid Wa Kwanza

´Allaamah Muhammad al-Jaamiy: Mujaddid wa kwanza aliyeujadidi Uislamu ni Abu Bakr asw-Swiddiyq. Fahamu hili ewe kijana. Abu Bakr alisimama msimamo imara kuwapiga vita wenye kuritadi, na kuwapiga vita wenye kukataa kutoa Zakaah, na kulitoa jeshi la Usaamah. Kama isingelikuwa Allaah kisha kwa aliyosimama kwayo Abu Bakr; kuacha ktuoa Zakaah, kisha ikafuatia na kuacha Swawm na kuacha Hajj mpaka Uislamu ukamalizika. Lakini Allaah Kamuwafikisha mtu huyu - pamoja na upole na ulaini wake - akasimama imara na akawakhalifu Maswahabah wote na kuwaambia "hapana" akiwemo ´Umar pia. Mtu ambaye alikuwa mkali katika Dini. ´Umar ambaye alikuwa ni ´Umar kweli. Akichukua Shaytwaan njia huichukua naye, akamkhalifu Abu Bakr na kumwambia: "Ee Abu Bakr, vipi utawaua watu nao wanasema: "ash-Hadu anlaa ilaaha illa Allaah, wa anna Muhammad Rasuulu Allaah." Abu Bakr akawakhalifu Maswahabah wote ambao walichukua pendekezo hili. Kwa mnasaba huu, [tunatumia fursa hii kwa kusema pia ya kwamba] mashauriano sio lazima. Abu Bakr ndio Mujaddid wa kwanza.

´Allaamah Muhammad al-Jaamiy:

Mujaddid wa kwanza aliyeujadidi Uislamu ni Abu Bakr asw-Swiddiyq. Fahamu hili ewe kijana. Abu Bakr alisimama msimamo imara kuwapiga vita wenye kuritadi, na kuwapiga vita wenye kukataa kutoa Zakaah, na kulitoa jeshi la Usaamah. Kama isingelikuwa Allaah kisha kwa aliyosimama kwayo Abu Bakr; kuacha ktuoa Zakaah, kisha ikafuatia na kuacha Swawm na kuacha Hajj mpaka Uislamu ukamalizika. Lakini Allaah Kamuwafikisha mtu huyu – pamoja na upole na ulaini wake – akasimama imara na akawakhalifu Maswahabah wote na kuwaambia “hapana” akiwemo ´Umar pia. Mtu ambaye alikuwa mkali katika Dini. ´Umar ambaye alikuwa ni ´Umar kweli. Akichukua Shaytwaan njia huichukua naye, akamkhalifu Abu Bakr na kumwambia: “Ee Abu Bakr, vipi utawaua watu nao wanasema: “ash-Hadu anlaa ilaaha illa Allaah, wa anna Muhammad Rasuulu Allaah.” Abu Bakr akawakhalifu Maswahabah wote ambao walichukua pendekezo hili. Kwa mnasaba huu, [tunatumia fursa hii kwa kusema pia ya kwamba] mashauriano sio lazima. Abu Bakr ndio Mujaddid wa kwanza.