Wale Wanaowapaka Mafuta Makafiri Na Kujipendekeza Kwao Na Dini Yao

´Allaamah al-Fawzaan: Haitoshelezi kwako wewe unampwekesha Allaah kwa ´Ibaadah na wala humshirikishi. Haitoshi hili! Ni lazima mpaka ujiweke mbali kabisa na washirikina na uamini ya kwamba wako katika upotofu. Ama ukisema sina nao kitu, huu ni uhuru wa kuabudu na kila mmoja ana Itikadi yake. Tunakwambia huu ni upotevu. Allaah Katuamrisha kujiweka mbali (kuwatenga) washirikina na dini yao. "Nami si katika washirikina.” (06:79) "Na pale Ibrahiym alipomwambia baba yake na Qawm yake: "Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu, Isipokuwa yule Aliyeniumba, kwani Yeye Ataniongoa." (43:26-27) Niko mbali (najitenga). "Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahiym na wale walio kuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: "Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Allaah. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Allaah peke yake." (60:04) Hii ndio Dini ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam) ambayo tumeamrishwa kuifuata. Kumejitokeza watu katika zama hizi katika wapakanaji mafuta, wanasema hapana msiwakate washirikina, wao wana Dini yao na wewe una Dini yako. Wanasema Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kasema: "Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu." (109:06) Kasema hivi kwa ajili ya kuwakata, na si kwa ajili ya kujiweka salama nao na kila mmoja abaki na Dini yake, hapana! Huku ni kwa ajili ya kujitenga na wao na dini yao. Sio kwa ajili ya kukubali (kuachana) na waliyomo na sisi tubaki kwa tuliomo, kila mmoja abaki na Dini yake, hapana! Hili si sahihi.

´Allaamah al-Fawzaan:

Haitoshelezi kwako wewe unampwekesha Allaah kwa ´Ibaadah na wala humshirikishi. Haitoshi hili! Ni lazima mpaka ujiweke mbali kabisa na washirikina na uamini ya kwamba wako katika upotofu. Ama ukisema sina nao kitu, huu ni uhuru wa kuabudu na kila mmoja ana Itikadi yake. Tunakwambia huu ni upotevu. Allaah Katuamrisha kujiweka mbali (kuwatenga) washirikina na dini yao.

“Nami si katika washirikina.” (06:79)

“Na pale Ibrahiym alipomwambia baba yake na Qawm yake: “Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu, Isipokuwa yule Aliyeniumba, kwani Yeye Ataniongoa.” (43:26-27)

Niko mbali (najitenga).

“Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahiym na wale walio kuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Allaah. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Allaah peke yake.” (60:04)

Hii ndio Dini ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam) ambayo tumeamrishwa kuifuata. Kumejitokeza watu katika zama hizi katika wapakanaji mafuta, wanasema hapana msiwakate washirikina, wao wana Dini yao na wewe una Dini yako. Wanasema Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kasema:

“Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.” (109:06)

Kasema hivi kwa ajili ya kuwakata, na si kwa ajili ya kujiweka salama nao na kila mmoja abaki na Dini yake, hapana! Huku ni kwa ajili ya kujitenga na wao na dini yao. Sio kwa ajili ya kukubali (kuachana) na waliyomo na sisi tubaki kwa tuliomo, kila mmoja abaki na Dini yake, hapana! Hili si sahihi.