Vipi Tutajua Ni Lipi Kundi lililookoka Na Moto?

Firqat-un-Naajiyah [Kundi lililookoka] sifa zake zinajulikana, wala haitakikani kwetu kuuliza, au kujitoa wenyewe au kuwatoa wengine [katika kundi liliookoka]. Je Ash´ariyyah, Maaturiydiyyah, Mu´tazilah au mapote mengine ni katika kundi lililookoka? Wewe jua kwanza sifa za kundi lililookoka kisha utaamua mwenyewe ni lipi. Kundi lililookoka ni lile ambalo limo katika yale waliokuwemo Maswahabah, kwani kheri zote zinapatikana katika mfumo wao. Na kufuata watu wema ni katika [mfumo] wa waliotangulia, na kusogelea Bid´ah ni katika [mfumo] wa waliokuja baadae. Salaf [Maswahabah] kheri zote ziko kwao, wao ndo Jamaa´ah, wao ndo Firqat-un-Naajiyah [Kundi lililookoka]. Na atakaepita njia yao huyo ni Salafiy. Msisahau unasibisho huu! Nyinyi mnaitwa Salafiyyuun, yaani mnajinasibisha na Salaf [wema waliotangulia]. Kwa kuwa mmewafuata katika Manhaj [mfumo] wao. Na ataekwenda kinyume na mfumo wao, huyo [anaitwa] Khalafiy.

Firqat-un-Naajiyah [Kundi lililookoka] sifa zake zinajulikana, wala haitakikani kwetu kuuliza, au kujitoa wenyewe au kuwatoa wengine [katika kundi liliookoka]. Je Ash´ariyyah, Maaturiydiyyah, Mu´tazilah au mapote mengine ni katika kundi lililookoka? Wewe jua kwanza sifa za kundi lililookoka kisha utaamua mwenyewe ni lipi. Kundi lililookoka ni lile ambalo limo katika yale waliokuwemo Maswahabah, kwani kheri zote zinapatikana katika mfumo wao. Na kufuata watu wema ni katika [mfumo] wa waliotangulia, na kusogelea Bid´ah ni katika [mfumo] wa waliokuja baadae.

Salaf [Maswahabah] kheri zote ziko kwao, wao ndo Jamaa´ah, wao ndo Firqat-un-Naajiyah [Kundi lililookoka]. Na atakaepita njia yao huyo ni Salafiy. Msisahau unasibisho huu! Nyinyi mnaitwa Salafiyyuun, yaani mnajinasibisha na Salaf [wema waliotangulia]. Kwa kuwa mmewafuata katika Manhaj [mfumo] wao. Na ataekwenda kinyume na mfumo wao, huyo [anaitwa] Khalafiy.