Vipi Hawa Wapewe Udhuru Ila Hawapewi Udhuru Qubuuriyyuun?

Swali: Wiki iliopita ulisema ya kwamba hakufuru mwenye kupinga kitu katika Majina na Sifa za Allaah, au akawa na kauli ya Huluuliyyah au watu wa Wahdat-ul-Wujuud ikiwa ni mjinga au ni mfuata kichwa mchunga mpaka kwanza asimamishiwe hoja. ´Allaamah al-Fawzaan: Kwa kuwa haya ni katika mambo madogo yanayohitajia ubainifu. Na huenda amefuata kichwa mchunga wengine, kwa kuwa hajui mambo haya. Muulizaji: "Kwa nini hapewi udhuru mtu ambaye si msomi katika waabudu makaburi mpaka kwanza asimamishiwe hoja?." ´Allaamah al-Fawzaan: Mtu ambaye si msomi yuko na anayemuonya, yuko na anayemtiakhofu. Angekuwa hana mtu kabisa, angelipewa udhuru. Lakini yuko na anayemuonya, yuko na anayemtia khofu, anasikia Qur-aan. Lakini yeye hataki hili. Ukimwambia anasema "Hii ni Dini ya wenye misimamo mikali, hii ni Dini ya Mawahabiy."

Swali:
Wiki iliopita ulisema ya kwamba hakufuru mwenye kupinga kitu katika Majina na Sifa za Allaah, au akawa na kauli ya Huluuliyyah au watu wa Wahdat-ul-Wujuud ikiwa ni mjinga au ni mfuata kichwa mchunga mpaka kwanza asimamishiwe hoja.

´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa kuwa haya ni katika mambo madogo yanayohitajia ubainifu. Na huenda amefuata kichwa mchunga wengine, kwa kuwa hajui mambo haya.

Muulizaji:
“Kwa nini hapewi udhuru mtu ambaye si msomi katika waabudu makaburi mpaka kwanza asimamishiwe hoja?.”

´Allaamah al-Fawzaan:
Mtu ambaye si msomi yuko na anayemuonya, yuko na anayemtiakhofu. Angekuwa hana mtu kabisa, angelipewa udhuru. Lakini yuko na anayemuonya, yuko na anayemtia khofu, anasikia Qur-aan. Lakini yeye hataki hili. Ukimwambia anasema “Hii ni Dini ya wenye misimamo mikali, hii ni Dini ya Mawahabiy.”