Uwajibu Wa Kupiga Radd Vipote Na Makundi Yanayokwenda Kinyume Na Manhaj Ya Salaf

Shaykh Abu ´Abdul-Haaliym ´Abdul-Haadiy: Kama alivyosema ´Allaamah Ibnul Qayyim (Rahimahu Allaah) na Salaf na maimamu kuhusu kutahadharisha watu na Bid´ah na watu wa Bid´ah. Kwa nini? Kwa kuwa madhara ya Bid´ah na kuiharibu dini ni mabaya na ni jambo la wajibu katika mambo ya uwajibu mkubwa na ni Jihaad kubwa. Kasema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah): “Hakika kutahadharisha watu na maimamu wa Bid´ah kwa watu wakukhalifu Qur-aan na Sunnah au ´Ibaadah zinazokhalifu Qur-aan na Sunnah, kubainisha hali zao na kutahadharisha Ummah dhidi yao ni wajibu kutahadharisha watu na Ahl-ul-Bid´ah.” Ni wajibu juu yako ewe mja wa Allaah kutadharisha watu dhidi ya watu wa bid´ah. Anasema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah): "Hakika kubainisha hali zao, na kuhadharisha Ummah dhidi yao ni wajibu kwa makubaliano ya wanachuoni." Kulisemwa kuambiwa Ahmad bin Hanbal: "Mtu anafunga, anaswali na kufanya I´itikaaf - yaani anafunga Swawm za sunnah, Swalah za sunnah na kufanya I´itikaaf, je ni bora au [mtu mwenye] kuwaongelea watu wa Bid´ah? Akasema: "Akisimama na kuswali na kufanya I´itikaaf ni faida yake yeye mwenyewe, na akiongelea watu wa Bid´ah faida ni ya Waislamu na hili ndio bora zaidi". Na ni wajibu kwa maulamaa wa ummah kutahadharisha watu dhidi ya watu wa Bid´ah na watu wa Ahwaa (matamanio), kwa kuwa ni Jihaad enyi waja wa Allaah, bali ni katika aina nzuri ya Jihaad katika njia ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Kasema Imaam al-Baghawiy katika Sharh-us-Sunnah: "Katwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mgawanyiko wa Ummah huu na kujitokeza Ahwaa na Bid´ah na kuokoka kwa yule atakayefuata Sunnah zake na Sunnah za Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum)". Waislamu wajue wakimuona mtu kashikamana na kitu katika Ahwaa na Bid´ah, au anachukia kitu katika Sunnah huku akiamini hivyo, mtu huyo inatakiwa kumhama (kumsusa) na kujiweka naye mbali kabisa na amuache sawa awe hai au maiti, asimtolee Salaam atapokutana nae, wala asimjibu atapoanza (kukutolea yeye Salaam), mpaka hapo atapoacha Bid´ah zake na kurejea katika haki... Na makatazo ya kumsusa ndugu yako zaidi ya siku tatu katika yaliyotokea baina ya watu wawili, hili halihusiana na mambo ya haki ya dini. Watu wengi wanadhani kuwa kumhama mtu hata ikiwa kwa watu wa Bid´ah, isizidi siku tatu. Maana ya Hadiyth si hii, fahamu Hadiyth hii vizuri. "Si halali kwa muumini kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu." Hili si kwa watu wa Bid´ah na Ahwaa. Bali hili linahusiana wakati watu wawili wanapo kwaruzana katika mambo ya kidunia au ya kawaida tu... Baina yako wewe na yeye. Ama watu wa Bid´ah na watu wa Ahwaa, wanasusiwa sawa waliohai na waliokufa mpaka watubie kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Na kwa hili anasema Imaam al-Baghawiy: "Kuwasusia watu wa Bid´ah na matamanio ni jambo la daima (milele) mpaka hapo watapotubia." Na si siku tatu, mambo gani siku tatu? Bali ni wajibu kwako kuwahama (kuwasusia) daima mpaka watapotubie, khasa ikiwa ni wale vigogo wa Bid´ah na Ahwaa. Hapa enyi ndugu, lazima tutanabahishe mambo mawili. Tusiwabadi´ na ku-Tafsiyq khasa kama wafanyavyo baadhi ya vijana wanapoona mtu katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kaanguka katika Bid´ah moja kwa moja wanamhukumu kuwa ni mtu wa Bid´ah na yuko hivi na vile, ku-Tafsiyq, na Kumbadi´ na kumhama, hapana ewe mja wa Allaah! Si kila mwenye kutumbukia katika Bid´ah, Bid´ah huanguka juu yake. Anaweza kutumbukia katika Bid´ah naye ni mjinga hajui, anaweza kutumbukia katika Bid´ah naye kalazimishwa hilo, kama jinsi baadhi ya vijana wameanguka na Jamaa´at-ut-Tabliygh, al-Ikhwaan Muflisuun wakawadanganya huku wakidhani kuwa wako katika haki. Ni juu yako kuwabainishia kuwa wako katika Bid´ah, na kwamba kitendo ambacho wakoemo ni Bid´ah. Uwabainishie kwa dalili katika Qur-aan na Sunnah za Mtume wa Allaah. Ama (baada ya kumfikishia) akaleta kiburi na ukaidi, huyu ndiye Mubtadi´ah (mtu wa Bid´ah). Mtu wa Bid´ah ni mtu ambaye kaanguka katika Bid´ah akanasihiwa lakini akaleta kiburi na ukaidi. Na si (kumhukumu) kabla hujamsimamishia haki ewe mja wa Allaah. Ama kwa yule anayekubali haki, tutamshika mkono na dini ni nasaha kama ilivyokuja katika Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na anasema Imaam ash-Shawkaaniy katika Fathiyl Qadiyr katika Tafsiri Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa): وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّى يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلاَ تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَى مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ “Na unapowaona wanaoziingilia Aayah zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Nakama Shaytwaan akikusahaulisha, basi baada yakutanabahi usikae pamoja na watu madhaalimu.” (06:68) Anasema (Rahimahu Allaah) - fahamu Aayah hii vizuri na uzingatie maana yake nayo ni Aayah kubwa. Anasema Imaam ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) kama ilivyo katika kitabu Fathiyl Qadiyr: "Katika Aayah hii kuna mawaidha makubwa kwa yule mwenye kukaa na watu wa Bid´ah." Kama wasemavyo baadhi ya vijana leo, tunaangalia maslahi na madhara (kabla ya kuwasusa watu wa Bid´ah); yako wapi maslahi? Je, ni wewe mwenye kujua maslahi na madhara? Mwenye kujua maslahi na madhara ni maulamaa ewe mja wa Allaah, ewe mja wa Allaah acha kucheza, acha kucheza ewe mja wa Allaah. Vijana wengi wanasema, tunaangalia maslahi na madhara - anakaa na watu wa Bid´ah, anatembea na watu wa Bid´ah, anacheka na watu wa Bid´ah na anasema: "Ni kwa ajili ya maslahi na madhara" Maslahi na madhara hayakadiriwi na wewe!! Ni maulamaa wangapi waliokuwa katika Sunnah, kwa kukaa kwao na watu wa Bid´ah na watu wa Hawaa wamepotea na hili lipo ewe mja wa Allaah. Ni watu wangapi katika wale wanaodai kuwa wana elimu walipoanza kukaa na watu wa Hawaa na wakajichanga nao wamepotea, kama ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq, ´Adnaan ´Ar´uur na wengine wengi katika makundi haya na katika watu hawa wanaodai kuwa wana elimu - wamepotea katika Manhaj kwa kukaa nao na watu wa Bid´ah na wamekuwa na wao sasa wanalingania watu katika Bid´ah. Hivyo ni lazima tufahamu Aayah hii kuna mawaidha makubwa kwa ambaye anakaa na watu wa Bid´ah ambao wanageuza Maneno ya Allaah na wanafanya mchezo na Kitabu Chake na Sunnah za Mtume na wanazikejeli kwa matamanio yao ya kipotofu na Bid´ah zao chafu. Basi ikiwa mtu hawezi kuwakataza na kubadilisha walioemo, basi angalau kwa uchache mtu aache kukaa nao na hilo ni jambo rahisi kwako, jiweke mbali na watu wa Bid´ah na hilo ni rahisi kwako na si gumu.

Shaykh Abu ´Abdul-Haaliym ´Abdul-Haadiy:

Kama alivyosema ´Allaamah Ibnul Qayyim (Rahimahu Allaah) na Salaf na maimamu kuhusu kutahadharisha watu na Bid´ah na watu wa Bid´ah. Kwa nini? Kwa kuwa madhara ya Bid´ah na kuiharibu dini ni mabaya na ni jambo la wajibu katika mambo ya uwajibu mkubwa na ni Jihaad kubwa. Kasema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

“Hakika kutahadharisha watu na maimamu wa Bid´ah kwa watu wakukhalifu Qur-aan na Sunnah au ´Ibaadah zinazokhalifu Qur-aan na Sunnah, kubainisha hali zao na kutahadharisha Ummah dhidi yao ni wajibu kutahadharisha watu na Ahl-ul-Bid´ah.”

Ni wajibu juu yako ewe mja wa Allaah kutadharisha watu dhidi ya watu wa bid´ah.
Anasema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

“Hakika kubainisha hali zao, na kuhadharisha Ummah dhidi yao ni wajibu kwa makubaliano ya wanachuoni.”

Kulisemwa kuambiwa Ahmad bin Hanbal:

“Mtu anafunga, anaswali na kufanya I´itikaaf – yaani anafunga Swawm za sunnah, Swalah za sunnah na kufanya I´itikaaf, je ni bora au [mtu mwenye] kuwaongelea watu wa Bid´ah? Akasema: “Akisimama na kuswali na kufanya I´itikaaf ni faida yake yeye mwenyewe, na akiongelea watu wa Bid´ah faida ni ya Waislamu na hili ndio bora zaidi”.
Na ni wajibu kwa maulamaa wa ummah kutahadharisha watu dhidi ya watu wa Bid´ah na watu wa Ahwaa (matamanio), kwa kuwa ni Jihaad enyi waja wa Allaah, bali ni katika aina nzuri ya Jihaad katika njia ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Kasema Imaam al-Baghawiy katika Sharh-us-Sunnah:

“Katwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mgawanyiko wa Ummah huu na kujitokeza Ahwaa na Bid´ah na kuokoka kwa yule atakayefuata Sunnah zake na Sunnah za Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum)”.

Waislamu wajue wakimuona mtu kashikamana na kitu katika Ahwaa na Bid´ah, au anachukia kitu katika Sunnah huku akiamini hivyo, mtu huyo inatakiwa kumhama (kumsusa) na kujiweka naye mbali kabisa na amuache sawa awe hai au maiti, asimtolee Salaam atapokutana nae, wala asimjibu atapoanza (kukutolea yeye Salaam), mpaka hapo atapoacha Bid´ah zake na kurejea katika haki…

Na makatazo ya kumsusa ndugu yako zaidi ya siku tatu katika yaliyotokea baina ya watu wawili, hili halihusiana na mambo ya haki ya dini. Watu wengi wanadhani kuwa kumhama mtu hata ikiwa kwa watu wa Bid´ah, isizidi siku tatu. Maana ya Hadiyth si hii, fahamu Hadiyth hii vizuri.

“Si halali kwa muumini kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu.”

Hili si kwa watu wa Bid´ah na Ahwaa. Bali hili linahusiana wakati watu wawili wanapo kwaruzana katika mambo ya kidunia au ya kawaida tu… Baina yako wewe na yeye. Ama watu wa Bid´ah na watu wa Ahwaa, wanasusiwa sawa waliohai na waliokufa mpaka watubie kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa).

Na kwa hili anasema Imaam al-Baghawiy:

“Kuwasusia watu wa Bid´ah na matamanio ni jambo la daima (milele) mpaka hapo watapotubia.”
Na si siku tatu, mambo gani siku tatu? Bali ni wajibu kwako kuwahama (kuwasusia) daima mpaka watapotubie, khasa ikiwa ni wale vigogo wa Bid´ah na Ahwaa.

Hapa enyi ndugu, lazima tutanabahishe mambo mawili. Tusiwabadi´ na ku-Tafsiyq khasa kama wafanyavyo baadhi ya vijana wanapoona mtu katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kaanguka katika Bid´ah moja kwa moja wanamhukumu kuwa ni mtu wa Bid´ah na yuko hivi na vile, ku-Tafsiyq, na Kumbadi´ na kumhama, hapana ewe mja wa Allaah! Si kila mwenye kutumbukia katika Bid´ah, Bid´ah huanguka juu yake. Anaweza kutumbukia katika Bid´ah naye ni mjinga hajui, anaweza kutumbukia katika Bid´ah naye kalazimishwa hilo, kama jinsi baadhi ya vijana wameanguka na Jamaa´at-ut-Tabliygh, al-Ikhwaan Muflisuun wakawadanganya huku wakidhani kuwa wako katika haki. Ni juu yako kuwabainishia kuwa wako katika Bid´ah, na kwamba kitendo ambacho wakoemo ni Bid´ah. Uwabainishie kwa dalili katika Qur-aan na Sunnah za Mtume wa Allaah.

Ama (baada ya kumfikishia) akaleta kiburi na ukaidi, huyu ndiye Mubtadi´ah (mtu wa Bid´ah). Mtu wa Bid´ah ni mtu ambaye kaanguka katika Bid´ah akanasihiwa lakini akaleta kiburi na ukaidi. Na si (kumhukumu) kabla hujamsimamishia haki ewe mja wa Allaah. Ama kwa yule anayekubali haki, tutamshika mkono na dini ni nasaha kama ilivyokuja katika Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na anasema Imaam ash-Shawkaaniy katika Fathiyl Qadiyr katika Tafsiri Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّى يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلاَ تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَى مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
“Na unapowaona wanaoziingilia Aayah zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Nakama Shaytwaan akikusahaulisha, basi baada yakutanabahi usikae pamoja na watu madhaalimu.” (06:68)

Anasema (Rahimahu Allaah) – fahamu Aayah hii vizuri na uzingatie maana yake nayo ni Aayah kubwa.
Anasema Imaam ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) kama ilivyo katika kitabu Fathiyl Qadiyr:

“Katika Aayah hii kuna mawaidha makubwa kwa yule mwenye kukaa na watu wa Bid´ah.”

Kama wasemavyo baadhi ya vijana leo, tunaangalia maslahi na madhara (kabla ya kuwasusa watu wa Bid´ah); yako wapi maslahi? Je, ni wewe mwenye kujua maslahi na madhara? Mwenye kujua maslahi na madhara ni maulamaa ewe mja wa Allaah, ewe mja wa Allaah acha kucheza, acha kucheza ewe mja wa Allaah. Vijana wengi wanasema, tunaangalia maslahi na madhara – anakaa na watu wa Bid´ah, anatembea na watu wa Bid´ah, anacheka na watu wa Bid´ah na anasema:

“Ni kwa ajili ya maslahi na madhara” Maslahi na madhara hayakadiriwi na wewe!! Ni maulamaa wangapi waliokuwa katika Sunnah, kwa kukaa kwao na watu wa Bid´ah na watu wa Hawaa wamepotea na hili lipo ewe mja wa Allaah. Ni watu wangapi katika wale wanaodai kuwa wana elimu walipoanza kukaa na watu wa Hawaa na wakajichanga nao wamepotea, kama ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq, ´Adnaan ´Ar´uur na wengine wengi katika makundi haya na katika watu hawa wanaodai kuwa wana elimu – wamepotea katika Manhaj kwa kukaa nao na watu wa Bid´ah na wamekuwa na wao sasa wanalingania watu katika Bid´ah.

Hivyo ni lazima tufahamu Aayah hii kuna mawaidha makubwa kwa ambaye anakaa na watu wa Bid´ah ambao wanageuza Maneno ya Allaah na wanafanya mchezo na Kitabu Chake na Sunnah za Mtume na wanazikejeli kwa matamanio yao ya kipotofu na Bid´ah zao chafu.

Basi ikiwa mtu hawezi kuwakataza na kubadilisha walioemo, basi angalau kwa uchache mtu aache kukaa nao na hilo ni jambo rahisi kwako, jiweke mbali na watu wa Bid´ah na hilo ni rahisi kwako na si gumu.