Uharamu Wa Kumuozesha Binti Na Mwanaume Kafiri Asiyeswali

Imaam Ibn ´Uthaymiyn: Mwenye kuacha Swalah ni kafiri hata kama atakubali kuwa ni faradhi. Kwa Kauli ya Allaah (Ta´ala): فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ الصَّلاَةَ وَآتَوُاْ الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ "Basi wakitubu na wakashika Swalah na wakatoa Zakaah, basi ni ndugu zenu katika Dini." (09:11) Na kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Hakika Baina ya mtu na shirki, na kufru, ni kuacha Swalah." Na kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Ahadi [mafungamano] baina yetu na baina yao [makafiri] ni Swalah, atakayeiacha atakuwa amekufuru." Na kasema ´Abdullaah bin Shaqiyq (Radhiya Allaahu ´anhu): “Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) hawakuwa wakiona ´amali yoyote nyingine mtu akiiacha anakuwa kafiri isipokuwa Swalah”. Na kufuru hii iliyokuja kwa anaeacha Swalah katika Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ni kufuru kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu inayowajibisha kuuawa duniani na ´Aakhirah kudumishwa Motoni. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu kuwaua viongozi [watawala] wa jeuri na dhuluma. Je, wauawe? Akasema "Msiwaue ikiwa wanaswali." Kakataza kuwaua wakiswali. Na hii ni dalili ya kujuzu kuwaua wakiacha Swalah. Na wala haijuzu kuwaua viongozi isipokuwa mpaka wakikufuru. Na kutokana na hili haijuzu kwa yeyote kumuozesha binti yake au kwa yule anayemsimamia mwanaume [mchumba] asiyemwamini Allaah na Mtume wake, wala kumuozesha yule anayefanya maskhara na Allaah, Mtume wake, Qur-aan au Dini Yake. Na wala haijuzu kumuozesha yule asiyeswali. Kwa kuwa watu wote hawa ni makafiri. Na makafiri haihalaliki kuwaozesha wanawake waumini. Anasema Allaah (Ta´ala) kuhusiana na Muhaajiraat: فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ "Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini." (60:10) Ataemuozesha Muislamu na kafiri, ndoa ni batili mwanamke si halali [kwa mwanaume huyo]; bali ni ajinabi kwake. Maingiliano yao ni Haramu kwa kuwa anamwingilia mwanamke ambaye si mke wake katika Kitabu cha Allaah. Wanatoa hoja baadhi ya watu wakisema "tunamuozesha huenda Allaah Akamuongoza". Twasema hatuna elimu ya Mustaqbal bali sisi tunajikalifisha na ya sasa. Maadamu kwa sasa si Muislamu, haijuzu kumuozesha hata akiwa ni katika makabila makubwa, sharafu tukufu, tajiri na mwenye mali nyingi. Mcheni Allaah enyi waja wa Allaah na wachagulieni mabanati zenu - chunguzeni Dini ya mchumbiaji kabla ya kukubali. Na msifanye hamu yenu kubwa ikawa mali hakika mali inakuja na inaenda. Ni matajiri wangapi wamekuwa mafakiri, na ni mafakiri wangapi wamekuwa matajiri. Mtapomjibia mchumbiaji kisha ikawabainikia [baadaye] Dini yake imepinda hakuna ubaya kwenu mkamrudishia hilo na wala msimuozeshe. Kwa kuwa amri iko mikononi mwenu maadamu ndoa haijatimia. Hali kadhalika lau itabainika [baadaye] kuwa ni mwenye tabia mbaya na hamkumridhia kuwa mume; hakuna ubaya mkamrudishia ombi lake hata kama ni baada ya kukubali.

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Mwenye kuacha Swalah ni kafiri hata kama atakubali kuwa ni faradhi. Kwa Kauli ya Allaah (Ta´ala):

فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ الصَّلاَةَ وَآتَوُاْ الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ
“Basi wakitubu na wakashika Swalah na wakatoa Zakaah, basi ni ndugu zenu katika Dini.” (09:11)

Na kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Baina ya mtu na shirki, na kufru, ni kuacha Swalah.”

Na kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ahadi [mafungamano] baina yetu na baina yao [makafiri] ni Swalah, atakayeiacha atakuwa amekufuru.”

Na kasema ´Abdullaah bin Shaqiyq (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hawakuwa wakiona ´amali yoyote nyingine mtu akiiacha anakuwa kafiri isipokuwa Swalah”.

Na kufuru hii iliyokuja kwa anaeacha Swalah katika Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ni kufuru kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu inayowajibisha kuuawa duniani na ´Aakhirah kudumishwa Motoni.

Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu kuwaua viongozi [watawala] wa jeuri na dhuluma. Je, wauawe? Akasema “Msiwaue ikiwa wanaswali.” Kakataza kuwaua wakiswali. Na hii ni dalili ya kujuzu kuwaua wakiacha Swalah.

Na wala haijuzu kuwaua viongozi isipokuwa mpaka wakikufuru.

Na kutokana na hili haijuzu kwa yeyote kumuozesha binti yake au kwa yule anayemsimamia mwanaume [mchumba] asiyemwamini Allaah na Mtume wake, wala kumuozesha yule anayefanya maskhara na Allaah, Mtume wake, Qur-aan au Dini Yake. Na wala haijuzu kumuozesha yule asiyeswali. Kwa kuwa watu wote hawa ni makafiri. Na makafiri haihalaliki kuwaozesha wanawake waumini. Anasema Allaah (Ta´ala) kuhusiana na Muhaajiraat:

فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ
“Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini.” (60:10)

Ataemuozesha Muislamu na kafiri, ndoa ni batili mwanamke si halali [kwa mwanaume huyo]; bali ni ajinabi kwake. Maingiliano yao ni Haramu kwa kuwa anamwingilia mwanamke ambaye si mke wake katika Kitabu cha Allaah. Wanatoa hoja baadhi ya watu wakisema “tunamuozesha huenda Allaah Akamuongoza”. Twasema hatuna elimu ya Mustaqbal bali sisi tunajikalifisha na ya sasa. Maadamu kwa sasa si Muislamu, haijuzu kumuozesha hata akiwa ni katika makabila makubwa, sharafu tukufu, tajiri na mwenye mali nyingi.

Mcheni Allaah enyi waja wa Allaah na wachagulieni mabanati zenu – chunguzeni Dini ya mchumbiaji kabla ya kukubali. Na msifanye hamu yenu kubwa ikawa mali hakika mali inakuja na inaenda. Ni matajiri wangapi wamekuwa mafakiri, na ni mafakiri wangapi wamekuwa matajiri. Mtapomjibia mchumbiaji kisha ikawabainikia [baadaye] Dini yake imepinda hakuna ubaya kwenu mkamrudishia hilo na wala msimuozeshe. Kwa kuwa amri iko mikononi mwenu maadamu ndoa haijatimia. Hali kadhalika lau itabainika [baadaye] kuwa ni mwenye tabia mbaya na hamkumridhia kuwa mume; hakuna ubaya mkamrudishia ombi lake hata kama ni baada ya kukubali.