Udhuru Kwa Sababu Ya Ujinga (01)

Imaam al-Albaaniy: Si sahihi kusema kuwa mtu anapewa udhuru kwa ujinga moja kwa moja. Wala si sahihi kusema kuwa hapewi udhuru moja kwa moja. Yote mawili ni makosa. Suala hili linahitaji ufafanuzi. Yule anayeishi katika mazingira ya Kiislamu wanaofahamu Uislamu ufahamu uliyo sahihi, kisha kukapatikana mtu ambaye ni mjinga kuhusiana na ´Aqiydah ya Kiislamu ilihali mtu huyu anaishi katika mazingira haya, mtu huyu hapewi udhuru. Mtu mwingine anayeishi katika mazingira ambayo sio ya Kiislamu, mazingira ya kufuru na upotofu kwa mfano Ulaya na Amerika, kisha akasilimu - huyu anapewa udhuru kwa ujinga wake. Kwa kuwa mazingira anayoishi hayawezi kumsaidia kujifunza na kuacha kuwa kutokuwa mjinga. Halafu wacha tutoe mfano ambao ni kinyume na ile sura ya kwanza ambapo tulisema kuwa mtu anaishi kwenye mazingira ya Kiislamu ambapo wanafahamu Uislamu ufahamu wa sahihi. Huyu hapewi udhuru. Hivi tunabadilisha sura na kusema mtu anayeishi kwenye jamii ya Kiislamu ambapo wengi wao wamekwenda kinyume na ´Aqiydah sahihi. Mtu huyu pia anakuwa ni mwenye kupewa udhuru kwa kuwa hakupata mazingira ambapo ni ya Kiislamu [yenye ufahamu] sahihi ambayo yanachangia moja kwa moja na ´Aqiydah sahihi. Yaani anakuwa hana haja ya kujifunza masomo hususan kwa kuwa mazingira yote yamejaa kwa ´Aqiydah sahihi.

Imaam al-Albaaniy:

Si sahihi kusema kuwa mtu anapewa udhuru kwa ujinga moja kwa moja. Wala si sahihi kusema kuwa hapewi udhuru moja kwa moja. Yote mawili ni makosa. Suala hili linahitaji ufafanuzi. Yule anayeishi katika mazingira ya Kiislamu wanaofahamu Uislamu ufahamu uliyo sahihi, kisha kukapatikana mtu ambaye ni mjinga kuhusiana na ´Aqiydah ya Kiislamu ilihali mtu huyu anaishi katika mazingira haya, mtu huyu hapewi udhuru. Mtu mwingine anayeishi katika mazingira ambayo sio ya Kiislamu, mazingira ya kufuru na upotofu kwa mfano Ulaya na Amerika, kisha akasilimu – huyu anapewa udhuru kwa ujinga wake. Kwa kuwa mazingira anayoishi hayawezi kumsaidia kujifunza na kuacha kuwa kutokuwa mjinga. Halafu wacha tutoe mfano ambao ni kinyume na ile sura ya kwanza ambapo tulisema kuwa mtu anaishi kwenye mazingira ya Kiislamu ambapo wanafahamu Uislamu ufahamu wa sahihi. Huyu hapewi udhuru. Hivi tunabadilisha sura na kusema mtu anayeishi kwenye jamii ya Kiislamu ambapo wengi wao wamekwenda kinyume na ´Aqiydah sahihi. Mtu huyu pia anakuwa ni mwenye kupewa udhuru kwa kuwa hakupata mazingira ambapo ni ya Kiislamu [yenye ufahamu] sahihi ambayo yanachangia moja kwa moja na ´Aqiydah sahihi. Yaani anakuwa hana haja ya kujifunza masomo hususan kwa kuwa mazingira yote yamejaa kwa ´Aqiydah sahihi.