Tahadhari Na Makundi Ya Umbea!

Imaam Ibn ´Uthaymiyn: Katika Taqwa (Ucha Mungu) mtu afanye bidii kubwa ya kuongoza waja wa Allaah kwa kusambaza elimu sahihi kutoka kwenye Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwabainishia njia ya Maswahabah na waliowafuata kwa wema na kuwafundisha watu kwa lile alilofundisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema: "Katika Uislamu mzuri wa mtu ni kuacha yale yasiyomuhusu." (at-Tirmidhiy (2318)." Utapomuona mtu yuko katika njia ya Allaah (´Azza wa Jalla) na anajishughulisha na yanayomuhusu na kujali tu yale yanayomkurubisha kwa Allaah, jua ya kwamba hilo ni kutokana na Uislamu wake mzuri. Na utapomuona mtu yeye hujali mambo ambayo hayana haja na yeye na hayamuhusu na muda wake mwingi unakwenda katika maneno ya kipumbavu (yaani ya umbea) na maswali mengi, jua ya kwamba hilo ni kutokana na upungufu wa Uislamu wake. Hivyo kakataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno ya kipumbavu (yani umbea) na maswali mengi. Kwa kuwa hilo linapoteza muda. Na mtu akishikwa na maradhi haya, hupoteza muda wake mwingi. Hukaa kwa huyu na kuanza kuuliza kumepitika nini, fulani kasema nini. Halafu huenda kwa wapili, watatu na wanne kuuliza tu. Hivyo hupoteza muda wake na muda wa wengine. Lakini ingelikuwa mtu anajali tu yale yanayomuhusu... Hakuna ubaya kuuliza kukitokea haja (dharurah) ya hilo, atauliza kilichopitika na kinachoendela katika jamii kwa lengo la kuyafanyia kazi na kuondosha madhara. Lengo isiwe kwa ajili ya kusengenya wengine au kusababisha mfarakano. Kama hali jinsi ilivyo kwa baadhi ya watu leo. Baadhi ya watu wana nia nzuri. Lakini masikini wamepatwa na maradhi haya, hivyo hujishughulisha tu na umbea, na fulani kasema nini na fulani kasema nini na kundi hili na lile limesema nini. Haulizi kwa ajili ya kuondosha maradhi na mfarakano. Anauliza kwa ajili ya kutaka kusengenya au anataka awe kama wasemavyo watoto: "Wewe uko pamoja na hawa hapa au wale kule!" Haya makundi makundi na vipote hayajulikani ila kwa watoto wadogo. Hivyo ninawahusia kukitenga mbali kabisa na mambo haya. Kwa kuwa hayana maslahi yoyote zaidi ya kupoteza muda. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kakataza kuharibu pesa na wakati kwa umbea na maswali mengi.

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Katika Taqwa (Ucha Mungu) mtu afanye bidii kubwa ya kuongoza waja wa Allaah kwa kusambaza elimu sahihi kutoka kwenye Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwabainishia njia ya Maswahabah na waliowafuata kwa wema na kuwafundisha watu kwa lile alilofundisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Katika Uislamu mzuri wa mtu ni kuacha yale yasiyomuhusu.” (at-Tirmidhiy (2318).”

Utapomuona mtu yuko katika njia ya Allaah (´Azza wa Jalla) na anajishughulisha na yanayomuhusu na kujali tu yale yanayomkurubisha kwa Allaah, jua ya kwamba hilo ni kutokana na Uislamu wake mzuri. Na utapomuona mtu yeye hujali mambo ambayo hayana haja na yeye na hayamuhusu na muda wake mwingi unakwenda katika maneno ya kipumbavu (yaani ya umbea) na maswali mengi, jua ya kwamba hilo ni kutokana na upungufu wa Uislamu wake. Hivyo kakataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno ya kipumbavu (yani umbea) na maswali mengi. Kwa kuwa hilo linapoteza muda. Na mtu akishikwa na maradhi haya, hupoteza muda wake mwingi. Hukaa kwa huyu na kuanza kuuliza kumepitika nini, fulani kasema nini. Halafu huenda kwa wapili, watatu na wanne kuuliza tu. Hivyo hupoteza muda wake na muda wa wengine. Lakini ingelikuwa mtu anajali tu yale yanayomuhusu…

Hakuna ubaya kuuliza kukitokea haja (dharurah) ya hilo, atauliza kilichopitika na kinachoendela katika jamii kwa lengo la kuyafanyia kazi na kuondosha madhara. Lengo isiwe kwa ajili ya kusengenya wengine au kusababisha mfarakano. Kama hali jinsi ilivyo kwa baadhi ya watu leo. Baadhi ya watu wana nia nzuri. Lakini masikini wamepatwa na maradhi haya, hivyo hujishughulisha tu na umbea, na fulani kasema nini na fulani kasema nini na kundi hili na lile limesema nini. Haulizi kwa ajili ya kuondosha maradhi na mfarakano. Anauliza kwa ajili ya kutaka kusengenya au anataka awe kama wasemavyo watoto:

“Wewe uko pamoja na hawa hapa au wale kule!”

Haya makundi makundi na vipote hayajulikani ila kwa watoto wadogo. Hivyo ninawahusia kukitenga mbali kabisa na mambo haya. Kwa kuwa hayana maslahi yoyote zaidi ya kupoteza muda. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kakataza kuharibu pesa na wakati kwa umbea na maswali mengi.


  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (66 A)
  • Kitengo: Uncategorized , Mchanganyiko
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 19th, October 2013