Sunnah Iliyosahaulika Ya Kuswali Kwa Viatu

Ama Shari´ah yetu inaruhusu kuswali kwa viatu na khufu [soksi za ngozi] kama alivyosali Mtume (swalla Allaahu alayhi wa sallam). Bali kufanya hivyo ni Sunnah. Kwa kauli yake Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Jitofautisheni na mayahudi, hakika wao haswali kwa viatu vyao." Sunnah ni kujitofautisha na mayahudi kwa hilo na kumuiga Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliekuwa akiswali kwa viatu vyake. Hivyo ni juu ya Muislamu anapoingia msikitini avue viatu na khufu zake na aziweke sehemu ya viatu... Na ikiwa ni visafi hakuna ubaya akaswali navyo msikitini ikiwa ni [msikiti wa] udongo. Lakini akivua viatu vyake huenda vikawa na udongo mwingi utaochafua msikiti au kuwaudhi wenye kuswali, hili ni bora zaidi na si lazima. Ama khufu hapana ikiwa alipangusa juu yake, aswali nazo. Kwa kuwa akizivua wudhuu wake unabatilika. Ikiwa alizivaa akiwa na twahara, asizivue bali aswali nazo. Lakini asiingie nazo mpaka kwanza aziangalie na aondoshe ikiwa zina maudhi [uchafu] mpaka aswali nazo akiamini kuwa ni safi. Ikiwa alikuja akiwa na twahara naye ana viatu, akipenda atavivua na kuviweka nafasi yake na akipenda ataacha [kuvua]. Na ikiwa atavua kwa murua watu wasije kumvamia na kumkataza au vina udongo, hili ni bora na kujiweka mbali na utata. La sivyo asli ni kuwa inajuzu kuswali na viatu hata ikiwa pamesafishwa - ikiwa viatu vyote ni visafi, hakuna ubaya kwa hilo kwa kumuiga Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini leo kutokana misikiti ilivyofasifishwa wakiona mtu kavaa viatu na khofu ikiwavina udongo au uchafu nk, watu humkataza na huenda wakamvamia kutokana na ujinga wao... Ikiwa atavivua mtu na kuweka sehemu nyingine, hili ni bora kutokana na ujinga wa watu leo...

Ama Shari´ah yetu inaruhusu kuswali kwa viatu na khufu [soksi za ngozi] kama alivyosali Mtume (swalla Allaahu alayhi wa sallam). Bali kufanya hivyo ni Sunnah. Kwa kauli yake Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Jitofautisheni na mayahudi, hakika wao haswali kwa viatu vyao.”

Sunnah ni kujitofautisha na mayahudi kwa hilo na kumuiga Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliekuwa akiswali kwa viatu vyake. Hivyo ni juu ya Muislamu anapoingia msikitini avue viatu na khufu zake na aziweke sehemu ya viatu… Na ikiwa ni visafi hakuna ubaya akaswali navyo msikitini ikiwa ni [msikiti wa] udongo. Lakini akivua viatu vyake huenda vikawa na udongo mwingi utaochafua msikiti au kuwaudhi wenye kuswali, hili ni bora zaidi na si lazima. Ama khufu hapana ikiwa alipangusa juu yake, aswali nazo. Kwa kuwa akizivua wudhuu wake unabatilika. Ikiwa alizivaa akiwa na twahara, asizivue bali aswali nazo. Lakini asiingie nazo mpaka kwanza aziangalie na aondoshe ikiwa zina maudhi [uchafu] mpaka aswali nazo akiamini kuwa ni safi. Ikiwa alikuja akiwa na twahara naye ana viatu, akipenda atavivua na kuviweka nafasi yake na akipenda ataacha [kuvua]. Na ikiwa atavua kwa murua watu wasije kumvamia na kumkataza au vina udongo, hili ni bora na kujiweka mbali na utata. La sivyo asli ni kuwa inajuzu kuswali na viatu hata ikiwa pamesafishwa – ikiwa viatu vyote ni visafi, hakuna ubaya kwa hilo kwa kumuiga Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini leo kutokana misikiti ilivyofasifishwa wakiona mtu kavaa viatu na khofu ikiwavina udongo au uchafu nk, watu humkataza na huenda wakamvamia kutokana na ujinga wao… Ikiwa atavivua mtu na kuweka sehemu nyingine, hili ni bora kutokana na ujinga wa watu leo…