Shaytwaan Anapenda Sherehe Ya Maulidi

Shaytwaan hufurahia maadhimisho ya Maulidi wakati Bid´ah zote ni katika matendo na upambiaji wa Shaytwaan. Hakuna shaka ya kwamba Shaytwaan hufurahia Waislamu kufanya Bid´ah anazowachochea. Ibn-ul-Jawziy kapokea ya kwamba Sufyaan ath-Thawriy kasema: "Ibliys anapenda Bid´ah zaidi kuliko dhambi. Mtu hutubia kwa dhambi tofauti na Bid´ah." Dalili ya kuwa Bid´ah zote katika Dini ni katika matendo ya Shaytwaan ni kwamba Allaah (Ta´ala) Katueleza ya kuwa Shaytwaan kasema: وَلَأُضِلَّنَّهُمْ ”Na hakika nitawapoteza.” (04:119) Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Na shari ya mambo ni [mambo] ya kuzua, na kila Bid´ah ni upotofu." Aayah na Hadiyth Swahiyh zinatoa dalili kwamba Bid´ah za Dini ni katika upotofu wa Shaytwaan. Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy ar-Radd al-Qawiy, uk. 24-25

Shaytwaan hufurahia maadhimisho ya Maulidi wakati Bid´ah zote ni katika matendo na upambiaji wa Shaytwaan. Hakuna shaka ya kwamba Shaytwaan hufurahia Waislamu kufanya Bid´ah anazowachochea. Ibn-ul-Jawziy kapokea ya kwamba Sufyaan ath-Thawriy kasema:

“Ibliys anapenda Bid´ah zaidi kuliko dhambi. Mtu hutubia kwa dhambi tofauti na Bid´ah.”

Dalili ya kuwa Bid´ah zote katika Dini ni katika matendo ya Shaytwaan ni kwamba Allaah (Ta´ala) Katueleza ya kuwa Shaytwaan kasema:

وَلَأُضِلَّنَّهُمْ
”Na hakika nitawapoteza.” (04:119)

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Na shari ya mambo ni [mambo] ya kuzua, na kila Bid´ah ni upotofu.”

Aayah na Hadiyth Swahiyh zinatoa dalili kwamba Bid´ah za Dini ni katika upotofu wa Shaytwaan.

Mwandishi: ‘Allaamah Hamuud bin ‘Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 24-25


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013