Salaf Walitahadharisha Sana Juu Ya Ahl-ul-Bid´ah, Nasi Tunafanya Hivo

Upande wa pili wa ndururu wa maneno haya yatakuwa ni maneno ya Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah). Watu wengi bila shaka watakasirika na kutukosoa kwa sababu tunawazungumzia watu wa Bid´ah na kuwaacha watenda madhambi kama wanywa pombe na wengineo. Mosi ni kuwa hatukuwaacha watu hawa na himdi zote ni za Allaah. Mawaidha yetu yanathibitisha hilo kwamba tunawakataza. Pili tutatilia uzito mkubwa kupambana na Ahl-ul-Bid´ah na kuwasimamia kidete mpaka Allaah (´Azza wa Jall) azime mwangaza wao. Tunamuomba Allaah (´Azza wa Jall) atusaidie na tufanikiwe. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema: "Kwa hiyo Salaf na maimamu waliyakemea kwa ukali na wakatahadharisha juu ya watu wa Bid´ah katika kila kona ya dunia. Walitahadharisha sana kabisa fitina yao na wakatilia uzito mkubwa katika hilo kuliko walivyotilia uzito machafu, dhuluma na unyanyasaji. Kwa sababu madhara ya Bid´ah na kuiharibu dini na vipingamizi vyake ni vikubwa." Madaarij-us-Saalikiyn (1/372). Mzungumzaji: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym Chanzo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 70-71 Toleo la: 30.03.2016 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Upande wa pili wa ndururu wa maneno haya yatakuwa ni maneno ya Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah). Watu wengi bila shaka watakasirika na kutukosoa kwa sababu tunawazungumzia watu wa Bid´ah na kuwaacha watenda madhambi kama wanywa pombe na wengineo.

Mosi ni kuwa hatukuwaacha watu hawa na himdi zote ni za Allaah. Mawaidha yetu yanathibitisha hilo kwamba tunawakataza.

Pili tutatilia uzito mkubwa kupambana na Ahl-ul-Bid´ah na kuwasimamia kidete mpaka Allaah (´Azza wa Jall) azime mwangaza wao. Tunamuomba Allaah (´Azza wa Jall) atusaidie na tufanikiwe.

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kwa hiyo Salaf na maimamu waliyakemea kwa ukali na wakatahadharisha juu ya watu wa Bid´ah katika kila kona ya dunia. Walitahadharisha sana kabisa fitina yao na wakatilia uzito mkubwa katika hilo kuliko walivyotilia uzito machafu, dhuluma na unyanyasaji. Kwa sababu madhara ya Bid´ah na kuiharibu dini na vipingamizi vyake ni vikubwa.” Madaarij-us-Saalikiyn (1/372).

Mzungumzaji: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
Chanzo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 70-71
Toleo la: 30.03.2016
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 30th, March 2016