Mwenye Kusema Kuwa Imaam al-Albaaniy Ni Myahudi

Hili ni swali la ajabu sana sijawahi kusikia maishani mwangu, anasema: Imamu Msikitini kwetu anasema kuwa al-Albaniy ni Myahudi. Mimi nadhani mtu huyu ni mmoja katika watu wawili: - Ima hamjui ni nani al-Albaaniy - Na ima ni Shaytwaan mgonjwa. Hatoki katika watu hawa wawili. Muinuko wa al-Albaaniy haukuinuka kwa kuwa ni al-Albaaniy peke yake, hapana. Kainuka kwa na kupanda daraja, na dunia kukithiri kumtaja, kwa kulinda kwake Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wallaahi, kisha wallaahi, kisha wallaahi, hata mapua yetu yakishindiliwa katika vumbi - sijui katika zama hizi aliyezilinda Sunnah za Mustwafaa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kwa 1/10 kwa juhudi alizoweka. Ni ushuhuda nitaoulizwa mbele ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Mtu huyu aliishi karibu miaka 90. Miaka yote hii alikuwa ni mwenye kuzilinda Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah Akanyanyua utajo wake katika Athaar, na katika minbar - minbar ya Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunasemwa: "[Hadiyth hii] kaisahihisha al-Albaaniy, kaidhoofisha al-Albaaniy na pia kasema ni Hasan." Tunamshukuru Allaah (Subhaahahu wa Ta´ala) kwa fadhila hii ambayo Allaah Katuneemesha kwa huduma hii ya kulinda Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika zama hizi ambayo wamekuwa wachache wenye kujishughulisha na fani hii, fani ya Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) msamaha mkubwa kwa Mola Wake (Tabaaraka wa Ta´ala). Na mtu huyu atakutana na Mola Wake na atakutana na malipo yake kwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) ikiwa hatotubia kwa hili.

Hili ni swali la ajabu sana sijawahi kusikia maishani mwangu, anasema: Imamu Msikitini kwetu anasema kuwa al-Albaniy ni Myahudi.

Mimi nadhani mtu huyu ni mmoja katika watu wawili:
– Ima hamjui ni nani al-Albaaniy
– Na ima ni Shaytwaan mgonjwa.

Hatoki katika watu hawa wawili. Muinuko wa al-Albaaniy haukuinuka kwa kuwa ni al-Albaaniy peke yake, hapana. Kainuka kwa na kupanda daraja, na dunia kukithiri kumtaja, kwa kulinda kwake Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Wallaahi, kisha wallaahi, kisha wallaahi, hata mapua yetu yakishindiliwa katika vumbi – sijui katika zama hizi aliyezilinda Sunnah za Mustwafaa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kwa 1/10 kwa juhudi alizoweka. Ni ushuhuda nitaoulizwa mbele ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala).

Mtu huyu aliishi karibu miaka 90. Miaka yote hii alikuwa ni mwenye kuzilinda Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah Akanyanyua utajo wake katika Athaar, na katika minbar – minbar ya Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunasemwa: “[Hadiyth hii] kaisahihisha al-Albaaniy, kaidhoofisha al-Albaaniy na pia kasema ni Hasan.”

Tunamshukuru Allaah (Subhaahahu wa Ta´ala) kwa fadhila hii ambayo Allaah Katuneemesha kwa huduma hii ya kulinda Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika zama hizi ambayo wamekuwa wachache wenye kujishughulisha na fani hii, fani ya Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) msamaha mkubwa kwa Mola Wake (Tabaaraka wa Ta´ala). Na mtu huyu atakutana na Mola Wake na atakutana na malipo yake kwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) ikiwa hatotubia kwa hili.