Mwanamke Mjamzito Anatokwa Na Vitu Vyeupe

Swali: Dada kutoka Ufaransa anauliza. Mwanamke mjamzito anatokwa na kitu cheupe, je ni wajibu kwake kutawadha kwa kila Swalah? ´Allaamah Zayd al-Madkhaliy: Ndio, vikitoka atatawadha. Ikiwa kuteremka kwake kunakatika, vimtokapo atajisafisha kisha atapahifadhi [kwa kuweka kitu kama kitamba n.k.] kisha atawadhe baada ya kuingia wakati halafu aswali. Mwanafunzi: Lakini si damu Shaykh, ni kitu cheupe? ´Allaamah Zayd al-Madkhaliy: Hata kama, ni lazima ajisafishe vinapomtoka na apahifadhi ikiwa ni kitu kinaendelea kumtoka kisha atawadhe baada ya kuingia kwa wakati halafu aswali. Ama ikiwa anapojisafisha vinakwisha [havimtoki], si lazima apahifadhi [kwa kitu] na wala si lazima kutawadha baada ya kuingia wakati, bali atatawadha wakati wowote ikiwa vinakuja na kuisha.

Swali:
Dada kutoka Ufaransa anauliza. Mwanamke mjamzito anatokwa na kitu cheupe, je ni wajibu kwake kutawadha kwa kila Swalah?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ndio, vikitoka atatawadha. Ikiwa kuteremka kwake kunakatika, vimtokapo atajisafisha kisha atapahifadhi [kwa kuweka kitu kama kitamba n.k.] kisha atawadhe baada ya kuingia wakati halafu aswali.

Mwanafunzi:
Lakini si damu Shaykh, ni kitu cheupe?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hata kama, ni lazima ajisafishe vinapomtoka na apahifadhi ikiwa ni kitu kinaendelea kumtoka kisha atawadhe baada ya kuingia kwa wakati halafu aswali. Ama ikiwa anapojisafisha vinakwisha [havimtoki], si lazima apahifadhi [kwa kitu] na wala si lazima kutawadha baada ya kuingia wakati, bali atatawadha wakati wowote ikiwa vinakuja na kuisha.