Mtu Anapolipa Swalah, Atoe Adhana Na Kukimu?

Swali: Atakayepitiwa na Swalah aadhini (kwanza) atapokumbuka (kisha ndo aswali)? Imaam Ibn Baaz: Ataadhini ikiwa wakati wake umetoweka, ama ikiwa bado wakati wake uko watu wamesha adhini, inatosha. Yeye itabidi akimu tu. Ama akiamka baada ya jua kuchomoza, Sunnah ni yeye aadhini kisha ndo akimu Swalah. Muulizaji: Ikiwa ni Swalah ya alfajiri na hakukumbuka ila mpaka baada ya Swalah ya ´Ishaa? Imaam Ibn Baaz: Atapoikumbuka ataiswali. Muulizaji: Je atarudi kuswali tena Dhuhr na ´Aswr? Imaam Ibn Baaz: Hapana halipi kitu. Atalipa tu (ile ile aliyosahau) wakati atakumbuka.

Swali:
Atakayepitiwa na Swalah aadhini (kwanza) atapokumbuka (kisha ndo aswali)?

Imaam Ibn Baaz:
Ataadhini ikiwa wakati wake umetoweka, ama ikiwa bado wakati wake uko watu wamesha adhini, inatosha. Yeye itabidi akimu tu. Ama akiamka baada ya jua kuchomoza, Sunnah ni yeye aadhini kisha ndo akimu Swalah.

Muulizaji:
Ikiwa ni Swalah ya alfajiri na hakukumbuka ila mpaka baada ya Swalah ya ´Ishaa?

Imaam Ibn Baaz:
Atapoikumbuka ataiswali.

Muulizaji:
Je atarudi kuswali tena Dhuhr na ´Aswr?

Imaam Ibn Baaz:
Hapana halipi kitu. Atalipa tu (ile ile aliyosahau) wakati atakumbuka.