Matatizo Ya Ahl-ul-Bid´ah Na Ahl-us-Sunnah

Imaam Ibn Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema: "Hali kadhalika mzushi yuko dhidi ya Sunniy kwa sababu anamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na halinganishi Sunnah na maoni ya wanaume wala na kitu kingine kinachoenda kinyume nayo." Mzushi humkosoa Sunniy kwa sababu ya kushikamana kwake na Sunnah, kama alivyoamrisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanakosoa kwa sababu ya hili. Lakini hawajikosoi wenyewe kwa kutendea kazi Bid´ah na mambo mepya na kutendea kazi maoni ya wanaume hata kama yatakuwa yanaenda kinyume na Sunnah na ni makosa. Wanayafuata hivo hivo. Wanasema kuwa masuala haya yana tofauti. Ukisema jambo fulani ni haramu wao wanasema kuwa suala hili lina tofauti. Ukisema jambo fulani ni wajibu wao wanasema kuwa suala hili lina tofauti. Kwa sababu jambo fulani lina tofauti ndio tuifuate? Tunatakiwa kufuata dalili: فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ "Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume." (04:59) وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ "Lolote lile mlilokhitilafiana, basi hukumu yake ni kwa Allaah." (42:10) Tunatakiwa kulinganisha tofauti na dalili; yale yanayoafikiana na dalili tunayachukua na yale yanayoenda kinyume na dalili tunayaacha hata kama ni mwanachuoni mkubwa ndiye aliye na maoni hayo. Wanachuoni wanaweza kukosea. Hawakukingwa na kukosea. Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (20) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighasah-12-2-1435-01.mp3 Toleo la: 17.04.2016 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Imaam Ibn Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hali kadhalika mzushi yuko dhidi ya Sunniy kwa sababu anamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na halinganishi Sunnah na maoni ya wanaume wala na kitu kingine kinachoenda kinyume nayo.”

Mzushi humkosoa Sunniy kwa sababu ya kushikamana kwake na Sunnah, kama alivyoamrisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanakosoa kwa sababu ya hili. Lakini hawajikosoi wenyewe kwa kutendea kazi Bid´ah na mambo mepya na kutendea kazi maoni ya wanaume hata kama yatakuwa yanaenda kinyume na Sunnah na ni makosa. Wanayafuata hivo hivo. Wanasema kuwa masuala haya yana tofauti. Ukisema jambo fulani ni haramu wao wanasema kuwa suala hili lina tofauti. Ukisema jambo fulani ni wajibu wao wanasema kuwa suala hili lina tofauti. Kwa sababu jambo fulani lina tofauti ndio tuifuate? Tunatakiwa kufuata dalili:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ
“Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.” (04:59)

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ
“Lolote lile mlilokhitilafiana, basi hukumu yake ni kwa Allaah.” (42:10)

Tunatakiwa kulinganisha tofauti na dalili; yale yanayoafikiana na dalili tunayachukua na yale yanayoenda kinyume na dalili tunayaacha hata kama ni mwanachuoni mkubwa ndiye aliye na maoni hayo. Wanachuoni wanaweza kukosea. Hawakukingwa na kukosea.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (20) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighasah-12-2-1435-01.mp3
Toleo la: 17.04.2016
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 17th, April 2016