Makafiri wote ni maadui wa Allaah

Sisi tunamshuhudisha Allaah kwa yale aliyosema: ya kwamba kila kafiri basi ni adui wa Allaah na kwamba kila kafiri ni adui wetu. Haya ni kwa dalili ya Qur-aan:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ

“Enyi walioamini! Msifanye adui Wangu na adui wenu kuwa wapenzi na marafiki.”[1]

Ni vipi watu hawa ambao Allaah ameshuhudia kuwa ni maadui na sisi vilevile tunashuhudia kuwa ni maadui tutafurahia sikukuu zao? Ni vipi tutazieneza kati ya watoto, wake wetu na wanawake wetu? Lakini si jengine isipokuwa huku ni kufa kwa mioyo, kuyeyuka kibinafsi na kuwafuata watu kichwa mchunga ndio jambo lililofanya mambo kama haya kuyaona ni mepesi kwetu.

[1] 60:01

Mzungumzaji: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Chanzo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (33) http://binothaimeen.net/content/698
Tarehe: 11-11-2017
Mfasiri: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Faida Mbalimbali
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 11th, November 2017