Maandamano Ni Fujo Na Uharibifu, Sio Katika Uisamu

Swali La Kwanza: Je, maandamano na mgomo ni katika Jihaad? Imaam Ibn Baaz: Hapana! Hili ni makosa, ni makosa, ni makosa! Hii ni fitina na shari. Haijuzu! Swali La Pili: Allah Akujaze khayr. Muulizaji anauliza. Je, maandamano ya wanaume na wanawake dhidi ya mtawala na kiongozi ni katika njia za kufanya Da´wah? Na kwa yule atakaekufa katika hali hii (kafa) shahidi katika njia ya Allaah? Imaam Ibn Baaz: Sionelei kama maandamano ya wanaume na wanawake ndio suluhisho. Bali hili linasababisha matatizo mengi, maovu, na baadhi ya watu wanaonewa, na wengine wanaonewa bila ya haki yoyote. Lakini kununi za Kishari´ah (zinazofaa kutumiwa) ni kuandikiana, kupeana nasaha na kusaidiana katika khayr. Yatendeke katika hali nzuri. Katika hali hii wasogelewe wanachuoni, Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wanaowafuata kwa wema. Kuandikiane na pawepo mijadala ya kupeana nasaha kwa wale waliyokosea, watawala, wafalme na viongozi. Yote haya yatendeke bila ya kutangaza hadharani katika mimbari - huyu kafanya hivi na vile na mfano wa hayo. Allaahu Musta-´aan.

Swali La Kwanza:
Je, maandamano na mgomo ni katika Jihaad?

Imaam Ibn Baaz:
Hapana! Hili ni makosa, ni makosa, ni makosa! Hii ni fitina na shari. Haijuzu!

Swali La Pili:
Allah Akujaze khayr. Muulizaji anauliza. Je, maandamano ya wanaume na wanawake dhidi ya mtawala na kiongozi ni katika njia za kufanya Da´wah? Na kwa yule atakaekufa katika hali hii (kafa) shahidi katika njia ya Allaah?

Imaam Ibn Baaz:
Sionelei kama maandamano ya wanaume na wanawake ndio suluhisho. Bali hili linasababisha matatizo mengi, maovu, na baadhi ya watu wanaonewa, na wengine wanaonewa bila ya haki yoyote.

Lakini kununi za Kishari´ah (zinazofaa kutumiwa) ni kuandikiana, kupeana nasaha na kusaidiana katika khayr.

Yatendeke katika hali nzuri. Katika hali hii wasogelewe wanachuoni, Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wanaowafuata kwa wema.

Kuandikiane na pawepo mijadala ya kupeana nasaha kwa wale waliyokosea, watawala, wafalme na viongozi. Yote haya yatendeke bila ya kutangaza hadharani katika mimbari – huyu kafanya hivi na vile na mfano wa hayo. Allaahu Musta-´aan.