Maadhimisho Ya Maulidi Yanapingana Na Qur-aan, Sunnah Na Matendo Ya Salaf

ar-Rifaa'iy kasema kuwa maadhimisho ya Maulidi hayapingani na Qur-aan, Sunnah na Ijmaa´ ya Waislamu, hata kama yamekuja baada ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na kufa kwa Maswahabah wake. Kwa hiyo, mtu hawezi kusema ya kwamba tendo hili ni la kulaumiwa kwa seuze tusiseme ya kuwa ni dhambi na kuwa ni Bid´ah ovu. Maadhimisho ya Maulidi ni Bid´ah katika Uislamu na maadhimisho yake yanapingana na Qur-aan, Sunnah na matendo ya Waislamu tangu wakati wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) hadi karne ya 600. Yanapingana na Qur-aan pale ambapo Allaah Anamuamrisha mja Wake kufuata yale Aliyoteremsha na hapana mwingine badala Yake. Allaah (Ta´ala) Anasema: اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ”Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu (Qur-aan na Sunnah) na wala msifuate badala Yake (Allaah), awliyaa (marafiki wapenzi, walinzi wanaokuamrisheni kufru, shirki). Ni machache mnayoyakumbuka.” (07:03) Maadhimisho ya Maulidi yanaingia katika makatazo haya ya jumla yaliyotajwa katika Aayah hii tukufu. Si Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) hakuamrisha kitendo hichi. Yule ambaye kaamrisha hili, ni yule ambaye kalizusha, yaani ni mfalme wa Arbil. Wale ambao wanasherehekea Maulidi wanamfuata mfalme wa Arbil na wanafanya yale Aliyokataza Allaah pale wanapofuata wengine badala Yake. أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ “Je, wanao washirika waliowaamuru (Shari’ah ya) Dini ambayo Allaah Hakuitolea idhini?” (42:21) Sherehe ya Maulidi inaingia katika makatazo haya ya jumla yaliyokatazwa katika Aayah hii tukufu. Allaah (Ta´ala) Hakuweka kitendo hichi katika Shari´ah. Ni mfalme Arbil ndio kaiweka. Wale wenye kusherehekea Maulidi wanafuata sheria ambayo Allaah Hakuitolea idhini. Isitoshe, maadhimisho ya Maulidi yanapingana pia na Sunnah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: “Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifah wangu waongofu baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Na tahadharini na mambo mepya ya kuzusha, kwa hakika kila jambo lenye kuzushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotofu.” Maadhimisho ya Maulidi sio katika Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Makhalifah wake. Kitendo hichi ni katika mambo yaliyozushwa na hivyo yanaingia katika yale ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) aliyokataza. Maadhimisho ya Maulidi yanapingana hata na matendo ya Waislamu kwa miaka 600. Ni jambo linalojulikana ya kwamba ilikuwa ni mfalme wa Arbil ndio mtu wa kwanza kuyasherehekea Maulidi. Aliyafanya Maulidi kuwa sherehe ya kuadhimishwa kila mwaka. Yalizushwa mwisho wa karne ya sita au mwanzo wa karne ya saba. Kabla ya hili ilikuwa ni kitendo kisichojulikana kwa Waislamu. Lau kama kungekuwepo mazuri yoyote katika kitendo hichi basi Maswahabah wangeliyafanya. Hakuna watu waliokuwa na hima katika matendo mazuri kama Maswahabah. Hakuna mtu yeyote katika Ummah huu ampendae Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kama Maswahabah. Hakuna mtu yeyote ashikamanae na kufuata Sunnah zake kama Maswahabah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema kuwa kundi lililookoka ni lile linalofuata yale ambayo yeye na Maswahabah wake wanayofuata. Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy ar-Radd al-Qawiy, uk. 122-123

ar-Rifaa’iy kasema kuwa maadhimisho ya Maulidi hayapingani na Qur-aan, Sunnah na Ijmaa´ ya Waislamu, hata kama yamekuja baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kufa kwa Maswahabah wake. Kwa hiyo, mtu hawezi kusema ya kwamba tendo hili ni la kulaumiwa kwa seuze tusiseme ya kuwa ni dhambi na kuwa ni Bid´ah ovu.

Maadhimisho ya Maulidi ni Bid´ah katika Uislamu na maadhimisho yake yanapingana na Qur-aan, Sunnah na matendo ya Waislamu tangu wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hadi karne ya 600. Yanapingana na Qur-aan pale ambapo Allaah Anamuamrisha mja Wake kufuata yale Aliyoteremsha na hapana mwingine badala Yake. Allaah (Ta´ala) Anasema:

اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ
”Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu (Qur-aan na Sunnah) na wala msifuate badala Yake (Allaah), awliyaa (marafiki wapenzi, walinzi wanaokuamrisheni kufru, shirki). Ni machache mnayoyakumbuka.” (07:03)

Maadhimisho ya Maulidi yanaingia katika makatazo haya ya jumla yaliyotajwa katika Aayah hii tukufu. Si Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hakuamrisha kitendo hichi. Yule ambaye kaamrisha hili, ni yule ambaye kalizusha, yaani ni mfalme wa Arbil. Wale ambao wanasherehekea Maulidi wanamfuata mfalme wa Arbil na wanafanya yale Aliyokataza Allaah pale wanapofuata wengine badala Yake.

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ
“Je, wanao washirika waliowaamuru (Shari’ah ya) Dini ambayo Allaah Hakuitolea idhini?” (42:21)

Sherehe ya Maulidi inaingia katika makatazo haya ya jumla yaliyokatazwa katika Aayah hii tukufu. Allaah (Ta´ala) Hakuweka kitendo hichi katika Shari´ah. Ni mfalme Arbil ndio kaiweka. Wale wenye kusherehekea Maulidi wanafuata sheria ambayo Allaah Hakuitolea idhini. Isitoshe, maadhimisho ya Maulidi yanapingana pia na Sunnah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifah wangu waongofu baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Na tahadharini na mambo mepya ya kuzusha, kwa hakika kila jambo lenye kuzushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotofu.”

Maadhimisho ya Maulidi sio katika Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na Makhalifah wake. Kitendo hichi ni katika mambo yaliyozushwa na hivyo yanaingia katika yale ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliyokataza.

Maadhimisho ya Maulidi yanapingana hata na matendo ya Waislamu kwa miaka 600. Ni jambo linalojulikana ya kwamba ilikuwa ni mfalme wa Arbil ndio mtu wa kwanza kuyasherehekea Maulidi. Aliyafanya Maulidi kuwa sherehe ya kuadhimishwa kila mwaka. Yalizushwa mwisho wa karne ya sita au mwanzo wa karne ya saba. Kabla ya hili ilikuwa ni kitendo kisichojulikana kwa Waislamu. Lau kama kungekuwepo mazuri yoyote katika kitendo hichi basi Maswahabah wangeliyafanya. Hakuna watu waliokuwa na hima katika matendo mazuri kama Maswahabah. Hakuna mtu yeyote katika Ummah huu ampendae Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kama Maswahabah. Hakuna mtu yeyote ashikamanae na kufuata Sunnah zake kama Maswahabah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema kuwa kundi lililookoka ni lile linalofuata yale ambayo yeye na Maswahabah wake wanayofuata.

Mwandishi: ‘Allaamah Hamuud bin ‘Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 122-123


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013